Sunday, 25 May 2014

KUTOKA JF: MGOGORO WA EAMWS




  1. Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

    Quote By jmushi1 View Post
    Kutembeza bakuli kuanzia Misri,Saudi, Jordan, Lebanon, Kuwait, Iraki ni

    kushauriana na serikaki za huko bila kuishirikisha serikali ambayo ndo

    kiwanza mpya baada ya uhuru wewe ulitegemea nini.Narudia tena

    mmenifundisha nilichokuwa sikijui na ninakushukuruni sana.Yani hadi

    rais wa Misri akamuagiza makamu wake waishughulikie hiyo issue na

    Tewa halafu mkataka rais wa nchi amchekee huyo mtu? Walichokuwa

    wakitaka kufanya akina Tewa ni hatari kwa usalama wa taifa lolote lile,

    ndo maana hata baadhi ya waislam walijitenga na hiyo EAMWS.
    jmushi,
    Haikuwa hivyo.

    Unahitaji urudi nyuma hadi 1963 Nyerere alipofanya hila ya kuivunja
    EAMWS na njama zile zikapambana na juhudi za Sheikh Hassan bin
    Amir
     na Bilal Rehani Waikela katika mkutano ulofanywa Aga Khan
    Girls.

    Nyerere alishindwa kuivunja EAMWS kipindi kile na ndiyo ilikuwa sababu
    ya Mzee Waikela kuwekwa kizuizini mwaka 1964.

    Kule kizuizini alikuwa pamoja na babu yangu Salum Abdalla katika
    jela ya Uyui, Tabora.

    Nimefurahi umenisoma vyema.

    Ukitoka hapo isome hotuba ya Waikela kwa Nyerere, ''Moto wa
    Waislam.''

    Ukipenda unaweza ukenda tena katika Halmashauri Kuu ya TANU
    mwaka huo huo wa 1963 siku Bi. Titi Mohamed alipowapinga
    Selemani Kitundu na Rajab Diwani kuhusu Aga Khan kisha
    akapambana na Nyerere kwa maneno ile nipe nikupe na Nyerere na
    wale aliokuwa akiwatumia wakashindwa pale Bi. Titi alipomtaja Allah
    mbele ya uso wa Nyerere.

    Hii ilikuwa bado hajapatapo kutokea katika historia fupi ya uhuru wa
    Tanganyika.

    Kama usalama wa taifa ulikuwa unahatarishwa na kuwa na uhusiano na
    nchi za Kiislam mbona wamishionari kutoka Ulaya walikuwa wamejaa
    nchini na wamegawana maeneo kwa miaka mingi tu?

    Hebu angalia hapa chini:

    ''Tanganyika was divided among different Christian organisations
    originating from various European countries. The Catholic Church,
    which is the most influential, was already established in Tanganyika.
    White Fathers were in Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza
    and Bukoba; Holy Ghost Fathers-in Morogoro and Kilimanjaro;
    Benedictine Fathers in Peramiho and Ndanda; Capuchin Fathers-in
    Dar es Salaam; Consolata Fathers-in Iringa and in Meru; Passionist
    Fathers-in Dodoma; Pallotine Fathers-in Mbulu; Maryknoll Fathers-
    in Musoma; and Rosmillian Fathers-in Iringa.[1]''

    Basi uhusiano na Misri ndiyo iwe nchi inahujumiwa?

    Hao unaosema Waislam waliojitenga kweli walijitenga lakini waliojitenga
    walikuiwa mamluki ambao walikuwa wanalipwa na Geofrey Sawaya
    hongo ya shs: 40,000 kwa kichwa kama bei yao ya usaliti.

    Wanajamvi,
    Huyu Sawaya alikuwa ndiyo Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

     
    Aliyesimama wa Mwanzo Kushoto ni Geoffrey Sawaya


    Sasa jiulize ''mgogoro'' wa EAMWS ulimuhusu vipi na nani alimpa fedha
    hizo za kuhonga?

    Mzee Waikela alikataa kupokea magendo yale akiwa na Sawaya wa
    tatu wao Allah Subhana Wataala ndani ya chumba Tabora Hotel na
    Tabora haikujitenga.

    jmushi,
    Nikukumbushe maneno ya Abdulwahid Sykes kwa Tewa Said Tewa
    April 1953 usiku wa kuamkia siku wanakwenda kumpa Nyerere uongozi
    wa TAA kisha waunde TANU?

    Je, ungependa kujua mwisho wa wale wasaliti ulikuwaje?

    Ni kisa ambacho jamvi letu litaburudika kusikia nini Allah aliwapa kabla
    malaika wa mauti hawajawafikia.

    Waliotendwa ni wazee wetu.
    Waliodhulumiwa ni wazee wetu.

    Tuliodhulumiwa ni sisi Waislam.

    Wazee wetu wameondoka duniani lakini walituachia hazina kubwa ya
    nini kilipitikana kabla hawajatangulia mbele ya haki.

    Ndiyo haya leo nakufungulieni hapa msome historia iliyofichwa kwa
    nusu karne.

    Kuna Nyaraka za Waikela alizificha kwa miaka 20 hadi ziliponifikia mimi
    miaka ya 1980.

    Jalada lililokuwa na hizo nyaraka nililipa jina, ''The Blue File,'' kutoka
    na jina la jalada katika mchezo wa senema, ''The Tamarind Seed.''

    Omar Shariff.

    Jalada hilo lilikuwa habari nyeti kuhusu Urusi na makachero wake
    waliokuwa Uingereza enzi za Vita Baridi.

    Fungua hapa bwana jmushi usikize Nyaraka za Waikela:
    http://www.mohammedsaid.com/2014/05/...ga-hassan.html



    Kipindi Maalum Radio Kheri na Radio Quiblaten: Kumbukumbu ya Sheikh Ilunga
    Katika Kipindi Hiki Nilieleza Nyara za Waikela na Umuhimu
    Wake Katika Kuujua Ukweli wa Kuvunjwa kwa EAMWS

    jmushi,Mimi huwa sikasirishwi na kejeli kama unapotumia maneno ya kuudhi,
    ''kutembeza bakuli,'' nk. nk.

    Mimi nimesomeshwa akida za mnakasha na Maalim Haruna (Allah 
    atamlipa In Sha Allah ) kwa Kizungu unaweza kusema, ''The Art of
    Debating.''

    Akisema, ''Silaha yako kubwa ni ile ilm uliyonayo katika somo la mjadala.
    Ukiona unatukanwa basi jua samaki keshameza ndoana na chambo chote.
    Kilichobaki ni kumtia chomboni basi.''

    Kisha akiongeza, ''Aliye na ilm hamkebehi mwenzake. Wanashindana
    kwa hoja tu. Usiwe debe tupu la Kimchembe.''

    (Huyu Kimchembe alikuwa muuza debe kule Gerezani enzi hizo maarufu
    kwa kupiga madebe yake kwa kelele kuita wateja).

    Hii nimesoma labda ni kijana mdogo wa miaka 14/15 hivi.

    Ndugu yangu mimi sina haja ya kukuleta katika ngarawa yangu kwa
    haraka.

    Nataka tuburudike kwanza na hili jamvi litakate.

    Nakusubiri Insha Allah...


    [1]See Kiongozi No. 6, June 1950. For more information on missionary
    penetration in East Africa, see M. Langley& T. Kiggins: A Serving People,Oxford University Press, Nairobi, 1974, p. 19.
    Last edited by Mohamed Said; Today at 00:52.
  2. #437   Report Post    
    Nanren's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 11th May 2009
    Posts : 1,323
    Rep Power : 827



    Likes Received
    456



    Likes Given
    604

    Default

    Quote By Mohamed Said View Post
    Gs-300,
    Haya ya Tanganyika hayajesha anataka tufungue uzi wa Kenya na Uganda.

    Maalim wangu Sheikh Haruna wakati akitusomesha akida za mnakasha
    akisema, ''Chunga mipaka baki ndani ya mipaka, ukitoka nje unavuruga.''

    Nikaja kufundishwa neno wanaita, ''demarcation,'' Chuo Kikuu.

    Nikawa najisemea sasa hii wananifundisha hapa Chuo Kikuu mimi hii mbona
    nimesomeshwa chuoni (madras) na Maalim Haruna?

    Kuna mtu alinikejeli mie na maalim wangu kuwa hivyo vyuo vikifundisha
    mnakasha...

    Juu ya kumwambia kuwa hilo ni moja ya somo katika masomo na kumueleza
    ilm hiyo ni kubwa ni ''art of debating,'' lakini kwa kuwa inatoka katika madras
    kafanya istizai...

    Ndiyo kama usemavyo hawabanduki wala hawapungui jamvini.
    Mie nim- dodge yeye...

    Ama akutukanae hakuchagulii tusi.
    Hata kwenye minakasha ya nyuma ulikwepa swali hivyo hivyo kwa kupitia mafundisho ya huyo mwalimu wako Haruna.
    Hutaki kujibu kilichoua EAMWS nje ya Tanzania kwasababu unachelea uwezekano kuwa kilichoua huko Kenya (Nyerere hakuwepo huko) ndicho kwa ukweli kilichoua huku Tanzania, na kikijulikana, hisia zako za conspiracy ya Nyerere na kanisa katoliki dhidi ya uislam zitabainika kuwa si za kweli.
  3. #438   Report Post    
    Mohamed Said's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 2nd November 2008
    Posts : 5,531
    Rep Power : 66159



    Likes Received
    3899



    Likes Given
    227

    Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

    Quote By Nanren View Post
    Hata kwenye minakasha ya nyuma ulikwepa swali hivyo hivyo kwa kupitia mafundisho ya huyo mwalimu wako Haruna.
    Hutaki kujibu kilichoua EAMWS nje ya Tanzania kwasababu unachelea uwezekano kuwa kilichoua huko Kenya (Nyerere hakuwepo huko) ndicho kwa ukweli kilichoua huku Tanzania, na kikijulikana, hisia zako za conspiracy ya Nyerere na kanisa katoliki dhidi ya uislam zitabainika kuwa si za kweli.
    Nanren,
    Unavyopenda.

    Kwa nini nikushurutishe?
    JF mtu anaingia kwa hiyari yake anatoka kwa hiyari yake.

    Unaandika unachijisikia kuandika.
    Wasikilizaji ndiyo waamuzi wa mwisho.

    Naogopa kuwa debe la Kimchembe.
  4. #439   Report Post    
    JokaKuu's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 31st July 2006
    Posts : 7,969
    Rep Power : 7460



    Likes Received
    3996



    Likes Given
    5430

    Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

    Mohamed Said,

    ..je, unaweza kutuwekea hapa jamii forums hotuba ya Mzee Waikela iliyoitwa "Moto wa Waislamu"?

    ..natanguliza shukrani.
  5. #440   Report Post    
    chipanga's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 17th September 2010
    Location : Dar es Salaam
    Posts : 380
    Rep Power : 569



    Likes Received
    89



    Likes Given
    41

    Default

    Quote By Mohamed Said View Post
    Gs ingia
    www.mohammedsaid.com utakuta taarifa hizo zote. Balozi Abdallah Sued ni
    mtoto wa Sued Kagasheki.
    Mkubwaaa! Nimekukubali kwa kweli, mwanzo nilidhani ni jitihada tu ya ku market kitabu/vitabu vyako lkn kumbe una website kbs kwa kazi hii?! We kiboko! Haya bhana, kila la kheri katika jitahada zako, natumai utafanikiwa katika ulilokusudia mkubwa!
  6. mkito

No comments: