Saturday, 24 May 2014

MZEE KISSINGER MWALIMU WA HISTORIA YA DAR ES SALAAM

Waliosimama wa Tatu Kutoka Kushoto Shariff Junaid
Waliokaa wa Pili Kutoka Kushoto Sheikh Kassim bin Juma na Wapili Yake
ni Ali Mwinyi Tambwe

Mzee Kissinger

Mzee Kissinger ni mwalimu wangu.
Anajua mengi kuhusu Dar es Salaam na historia yake.

Huna utakalomuuliza kuhusu mji huu kuanzia watu mashuhuri na wasio mashuhuri, masheikh na wauumini wa kawaida ikawa yeyee hana la kukusomesha.

Ndiye aliyenisomesha maisha ya Sheikh Kassim Juma na mada niliyoandika katika yale aliyonifunza niliitoa Chuo Kikuu Cha Kenyatta.

Ukipenda kuisoma paper ya Sheikh Kassim ingia hapa:http://www.mohammedsaid.com/2013/12/regional-conference-of-islam-in-eastern.html

Mzee Kissinger alinieleza maisha ya utoto wa Sheikh Kassim akiwa Bagamoyo hadi alipotoroka nyumbani kuja Dar es Salaam kuendelea kusoma chuoni kwa Sheikh Uwesu Mtaa wa Gogo huku Mtaa wa Mchikichi na huku Mtaa wa Narung'ombe na vipi baba yake Sheikh Juma bin Khamis alivyopata tabu kumtafuta na kumkuta kwa Sheikh Uwesu. Sheikh Uwesu alikuwa khalifa wa tarika ya Qadiriyya. Mzee Kissinger ndiye aliyenifungulia mlango nikaingia na kuona maisha ya masheikh waliopita na kunieleza kwa nini hao juu ya kuwa walikuwa na ilm kubwa ya dini hawakuweza kuwa na athari kubwa katika maisha ya wakazi wa Dar es Salaam kama alivyokuwa Sheikh Kassim. Mzee Kissinger alinifungulia pazia na kuniwekea wazi ile ''charisma '' isiyo ya kawaida na ujana wa Sheikh Kassim ulichanganyika na Udarisalama kiasi kuwa aliweza kuingia nyumba yoyote kuanzia Mtaa wa Jangwani, Kariakoo hadi Kiungani, Gerezani kama yake na akakaribishwa na yeye alikuwa mtu wa watu hakubagua shughuli ya mkubwa au mdogo. Popote alipoitwa alifika bila kukosa. Mzee Kissinger  akinifungulia zaidi kuhusu Sheikh Kassim Alinambia kuwa Sheikh Kassim alikuwa jasiri na hii sifa ya ujasiri ni sifa ambayo Mzee Kissinger anase,ma alimsikia  Shariff Junaid akiitaja. Hakumuogopa yeyote na popote aliposimamishwa kusema Sheikh kassim alizungumza bila hofu. Sifa yake kubwa ni kuwa Sheikh Kassim aliwapenda masheikh na masharifu na aliwaadhimisha sana.



Mzee Kissinger ndiye aliyenisomesha habari hizyo hapo chini na kunipa gazeti hilo.



No comments: