Tuesday, 27 May 2014

KUTOKA JF: SHUTUMA YA KUANDIKA HISTORIA UPYA KWA MLENGO WA UISLAM

  1. #565   Report Post    
    Mohamed Said's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 2nd November 2008
    Posts : 5,553
    Rep Power : 66163


    Likes Received
    3946


    Likes Given
    228

    Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

    Quote By WildCard View Post
    Ndugu yangu,

    Akina Ritz & Co wana mradi wa kuandika UPYA historia ya NCHI hii kwa mgongo wa dini yao. Hawataweza kubadili kitu.
    WildCard,
    Hakuna mtu mwenye mradi wowote hapa.

    Hapa jamvini ni kubadilishana mawazo ya nini kilisahauliwa katika
    historia zilizoandikwa.

    Waandishi wengi wameandika historia ya uhuru.

    Edward Barongo, Chuo Cha Kivukoni, John Illife, Kimambo 
    wameandikana wengi bado wataandika.

    Mimi nimeandika historia kama nilivyopokea kwa wazee wangu na hii
    ni toka mwaka 1998 kitabu kilipochapwa London.

    Mwaka wa 2004 kikachapwa Nairobi kwa Kiswahili.

    Sasa hiki kitabu hakiweza kwa leo 2014 kuwa mradi wa mtu yeyote.

    Usifadhaike na habari mpya katika historia ya uhuru wa Tangayika
    huu ndiyo usomi.

    Usomi haugandi (static) kila siku usomi unasonga mbele kwa habari
    na taarifa mpya za uchunguzi.

    Kuwa nimeandika kwa ''mgongo wa dini,'' naam hiyo ndiyo ilikuwa
    ''focus,'' yangu na ndiyo kitu kilichokipa kitabu changu umaarufu.

    Hilo la kubadili historia kitabu changu kimebadilisha historia yote ya
    uhuruwa Tanganyika.

    Si kubadili tu kimeleta raha na msisimko msomaji anapoisoma na pia
    kutembea na Nyerere mguu kwa mguu hatua kwa hatua katika mitaa
    ya Dar es Salaam ya 1950 kaongozana na Shariff Abdallah Attas
    wanakwenda nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey/Sikukuu
    kula chakula cha mchana.

    Haya ndiyo mabadiliko na habari ambazo wengi hawakuwa wanajua.
    Na Nyerere hapo anatokea ofisini kwa Abdul Sykes Kariakoo Market.

    Haya ndiyo mabadiliko wasomaji wameyaona nilipowaambia kuwa
    hiyo ofisi ya Abdul Sykes Kariakoo ndipo mipango yote ikifanyika
    dhidi ya Waingereza.

    Na ofisi nyingine ya harakati za TAA ni ofisi ya Hamza Mwapachu
    pale Ilala Welfare Centre.

    Haya yamefanyika 1950 Nyerere bado hajaja Dar es Salaam.

    Ukipenda kujua zaidi katika mabadiliko haya nifahamishe nitakueleza
    In Sha Allah.
    Last edited by Mohamed Said; Today at 12:30.
    Gs-300 likes this.
  2. mkito

No comments: