Saturday, 7 June 2014

KUTOKA JF: UTATA KATIKA UTAFITI NA UANDISHI WA HISTORIA YA KWELI YA TANU

1.       
Yesterday 19:24
#1324   Report Post    
Mohamed Said's Avatar
JF Senior Expert Memberhttp://www.jamiiforums.com/images/verified.pngArray
Join Date : 2nd November 2008
Posts : 5,674
Rep Power : 66188
Likes Received
4225
Likes Given
231
Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
Quote By WildCard View Post
Faiza,
Al alamaa Mohamed Said kazaliwa 1953.
Yaani ni mdogo wa Jakaya.
 Anayajua hadi ya Sykes Mbuane aloofanya mwaka
1929 na namna alivyotoka kule bondeni.
 Jakaya anachukua Urais wa Nchi hii bila kuijua "historia" hii?


WildCard,
Mimi nimezaliwa tarehe 25 Februari, 1952.

Mimi nimeyajua haya kwanza kwa kuwa hapo nilipozaliwa mie Mtaa wa Kipata ndipo wakiishi Kleist Sykes na wanae wote wamezaliwa hapo na wamekuwa pamoja na wazee wangu.

Karibu ya wote niliokutajia humu wengi wao hiyo ndiyo ilikuwa mitaa yao wakiishi, Zuberi Mtemvu, Mashado Plantan, Saleh Muhsin, Omari Londo na wengine wengi.

Hawa wote ni watu wa TANU.

Wakati naanza utafiti huu hali ya Tanzania ilikuwa ya kutisha huwezi kwenda kwa mtu hivi hivi ukamuuliza, ''Ati mzee nasikia ile TANU ni ''brainchild'' ya Abdul Sykes?''

Atakufukuza nyumbani kwake atajua wewe ''sekuriti,'' umetumwa na Nyerere kumpeleleza.

Lakini mimi kwa ule uzawa wangu na umaarufu wa wazee wangu nikenda hana wasiwasi anajua huyu anafanya utafiti anajisemea, ''Huyu si mtoto wa Said yuko Mlimani naona yuko katika utafiti.''

Si swali la kuwa mkubwa au mdogo ile kujua haya.
Hili la kwanza.

La pili na hili ndilo kubwa kupita yote.

Hadi sasa ukimtoa John Illife mimi ndiyo mtafiti pekee niliyoaminiwa na hizo Nyaraka za Sykes kuzisoma zote na kufanya nakala nikafanya mahojiano ''reordered,'' na Ally Sykes.

Sikuishia hapo nikafanya mahojiano na wazee wengi waliokuwa hai wakati ule hapa Dar es Salaam mmojawapo akiwa Ahmed Rashad Ali.

Nikazungumza na Mzee Maxwell huyu alikuwa Mkenya na rafiki yake Dome Okochi Budohi aliyebaki nyuma Tanganyika hadi miaka ya 1970.

Huyu ndiye aliyeniunganisha na Budohi.

Budohi kadi yake ya TANU ni na. 5.

Nikasafiri hadi Lindi kwa utafiti na nikazungumza na Salum Mpunga na Yusuf Chembera.

Nikasafiri hadi Tabora hapo ndipo nilipozungumza na jopo likiongozwa na Bilal Rehani Waikela na Abdallah Kassongo.

Siku ya mahojiano nilikuwa na wazee takriban 10.

Wakati wa kudai uhuru hawa walikuwa vijana.

Nikatoka Tabora nikenda Tanga kukutana na Sheikh Rashid Sembe, na Mmaka Omari.

Mmaka Omari alikuwa katika Tanga Volunteer Corps (TVC).

Hii ilikuwa kama Bantu Group ya akina Yusuf Bakis na Rashid  ''Officer'' Sisso ya Dar es Salaam.

Huyu Rashid Sisso alikuwa katika mikutano ya TANU akisimama nyuma ya Nyerere kama kivuli chake na Nyerere ndiye aliyempa hilo jina la utani ''Officer.''

Katika ile picha ya kumuaga Nyerere 1955 safari ya kwanza UNO,Rashid Sisso yupo katika picha.

Hapo Tanga ndipo nilipokutana na Mzee Mohamed Kajembe muasisi wa TANU.

Alinipa mshtuko pale alipoingia ndani kwake akaja na ''notebook'' alimoandika vikao vyote vya kwanza vya kuunda TANU wanachama wakiwa wauza nazi soko la Ngamiani, yeye akiwa mmojawapo.

Kutokana na mahojiano ya Rashid Sembe pale Tanga nyumbani kwake Br. 14 nimeandika sura nzima katika kitabu changu, ''The Tanga Strategy.''

Hii ilikuwa siri kubwa na Nyerere hakueleza hadi anaingia kaburini.

Ulikuwa mpango wa kuwaangusha wale waliokuwa hawataki Kura Tatu maarufu kwa pale New Street ni Sheikh Takadir na Mtemvu.

Muhimu katika mkakati huu ni kuwa uongozi wa TANU pamoja na  Nyerere na Elias Kissenge walikwenda Mnyanjani ambako kilifanyika kisomo kikubwa na Qur'an ilisomwa na Sheikh Kombora, mjomba wake Mwalimu Kihere.

Hii inaitwa ''tawaswul.''

Haya yote yalifanywa na wazee wetu kujitupa kwa Allah awanusuru na njama za Waingereza.

Hii ilikuwa 1958 na kulikuwa na hatari ya chama kumeguka pande mbili.

Sheikh Suleiman Takadir na Mtemvu na watu wao upande mmoja na Nyerere upande wa pili.

Hisia za udini kutaka kujua nafasi ya Waislam katika Tanganyika huru zilikuwa zimejitokeza kwa uwazi kabisa kutokana na masharti ya kura tatu.

WildCard,
Huwezi ukaieleza historia ya TANU kama ufanyavyo wewe kwa mistari minne.

Hii historia ni bahari ya kina kirefu.

Sasa Rais Kikwete hawezi kuyajua haya sharti apige goti na apinde mgongo kwa walimu wamsomeshe.

Historia hii haipo katika vitabu vya jopo la Chuo Cha Kivukoni.

Historia hii ilikaa miaka mingi katika vifua vya wazee wetu ikisubiri siku ifike.

Aliniambia Mzee Waikela, ''Mimi nikijua kuwa Allah si dhalim hawezi akaachia dhulma nilijua atakuja mtu siku moja kuiandika.''
Last edited by Mohamed Said; Yesterday at 19:44.
FaizaFoxyTHE BIG SHOW and RockSpider like this.
Quote
2.    Ritz is offline    Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
 By WildCard View Post
Huyo anayekukataza usinijibu hautakii mema mnakasha huu. Atakuwa ananitafutia fatwa.

Halafu Mzee Mohamed, ushahidi wa kujinukuu mwenyewe mgumu kumeza. Hiyo "Muslim leadership in TANU" ni akina nani hao? Ukiangalia wale waasisi wa TANU 17, hapakuwa na Muslim leadership pale. Kiongozi Mkuu wa TANU mwanzo hadi mwisho ni Mwalimu pekee.
WildCard,
Mimi sijinukuu mwenyewe.

Hayo ambayo ninanukuu mengi ni kutoka kitabu changu, ''The Life and Times
of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)the Untold Story of the Muslim Struggle
Against British Colonialism in Tanganyika,'' pamoja na ''paper'' na makala zangu
nilizoandika.

Hili la kwanza.
Pili ikiwa unahisi huamini niandikacho hapana ugomvi watu lazima wahitilafiane.

Tatu.
Hili tatizo la uchaguzi hakika limetokea na ni la kweli kabisa.

Hata hili ikiwa hutapenda kuliamini kwangu mimi ni sawa mradi kuna watu
hapa jamvini wanasoma na naamini wana akili na uwezo wa kutupima mie
na wewe nani mjuzi wa historia hii.

WildCard,
Tatizo lako masikini wewe unatumia moyo.
Mimi waliyofanya haya ni wazee wangu na wamenieleza kila kitu.

Muslim leadership ilikuwapo nyuma ya TANU na ilikuwa na nguvu
kubwa sana.

Nitakupa majina machache.

Alikuwapo Sheikh Hassa bin Amir, Sheikh Nurdin Hussen, Sheikh
Abdallah Iddi Chaurembo, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh
Hashir, Sheikh Mohamed Ramia, Sheikh Issa Nasir, Sheikh
Mohamed Yusuf Badi
 na wengine wengi.

Sasa hii inafanyaje kazi.

Hawa wote walikuwa watu wa tarika na zawiyya na hizi zote zina wafuasi wengi sana na hawa wote walikuwa wakifanya kazi za TANU.

Ndiyo maana ukaona wanachama wa kwanza wa TANU mwaka 1954 Mzee Said Chamwenyewe kawaleta kutoka Rufiji.

Hawa wote walikuwa ni murid wa Tarika Qadiriyya.

Sijui kama haya mambo unayaelewa lakini ukitaka kuyajua kwa undani msome August Nimtz, ''Islam and Politics in East Africa.''

Wewe haya huyajui lakini Nyerere akiyajua vizuri sana.
Hii ndiyo historia jinsi Waingereza walivyoshambuliwa na wazee wetu.

Najua historia hii inachonyota nyoyo zenu lakini mimi sikuiandika kwa  nia mbaya ili nikuadhirini kuwa hamkuwapo.

Haya yangu ilikuwa kueleza historia ya kweli ili mchango wazee wangu urudi kwenye nafasi yake ya heshima na utambulike.

Kuhusu wale waasisi 17 wa TANU.

Abdul na Ally Sykes, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Julius Nyerere na John Rupia hawa ni watu wa Makao Makuu, New Street.

Hawa ni watu 6.

Katika hao 11 waliobaki waliokuwa na athari katika kupambana na wakoloni ni mmoja tu - Saadan Abdu Kandoro kutoka Kanda ya Ziwa.

Wanabaki 10.

Katika hao 10 Japhet Kirilo kilichomuingiza katika waasisi ni Land Meru Case iliyompeleka hadi UNO akifuatana na Earl Seaton kama mkalimani.

Wanabaki 9.
Hapa nitamleta Joseph Kimalando kutoka Moshi.

Aliporudi Moshi hakutaka kufungua ofisi ya TANU akafukuzwa uanachama na Yusuf Olotu akashirikiana na wenzake wakafungua ofisi ya Moshi  mjini.

Unaweza kusoma habari za Yusuf Olotu hapa chini:
YUSUF OLOTU 1927 - 1997: SHUJAA WA KURA TATU, 1958 - Mohamed Said

Tabora kulikuwa na tatizo kama la Moshi.

Germano Pacha hakutaka kufungua matawi ya TANU Western Province akatolewa katika uongozi na nafasi yake akashika Said Ali Maswanya.

Wamebaki 8.

Katika hawa 8 ambae habari zao zinajulikana lau kwa uchache ni za Kasella Bantu na Lameck Bugohe tena baada ya wao wenyewe  kueleza.

WildCard,
Nadhani umeipata picha.

Maalim Haruna alikuwa akisema, ''Kabla hujakwenda Tua Tugawe  kucheza mpira kwanza jifunze danadana.''

(''Tua Tugawe'' ni jina lingine la viwanja vya Mnazi Mmoja).

Kwa kutimia neno danadana Maalim Haruna alikuwa na maana ya kuwa kabla hjenda katika mnakasha kwanza usome ulijue somo lenyewe.

Sasa wewe WildCard unataka kuja kufanya mnakasha historia yenyewe ya TANU unayoitegemea ni ile ya jopo la Kivukoni.

Hii ni hatari ni sawa unajitosa kuvuka mkondo wa Kigamboni na wewe kuogelea hujui wala huna boya la kukusaidia kuelea.

Lazima utazama.

Kwa taarifa yako.
Hadi sasa tuna wasikilizaji 20,000+ and counting...katika uzi huu.
Last edited by Mohamed Said; Yesterday at 17:46.
FaizaFoxy likes this.

2.       WildCard is offline 


JF Senior Expert Memberhttp://www.jamiiforums.com/images/verified.pngArray
Join Date : 2nd November 2008
Posts : 5,674
Rep Power : 66188
Likes Received
4225
Likes Given
231
Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
Quote By pondamali View Post
Dr. Kyaruzi alichaguliwa rais wa TAA 1950 hadi alipohamishwa kikazi nzega 1951.
katika muda mfupi wa urais wake alifanya baadhi ya yafuatayo:
1. Kubadili katiba ili chama kitambulike kisiasa
2. kuunda kamati za kisiasa, 'political steering and enforcement committees'
3. kuwahusisha wana TAA wa nje ya Dar, na kuwapa taarifa zote toka makao makuu.

Mkutano mwingine wa Uchaguzi ulifanyika 1953, Nyerere akachaguliwa kuwa Rais.
Mwaka 1954, TAA ikawa TANU. Tokea hapo unajua nini kilichoendelea. Wazee wa Gerezani na wengineo ikala kwao.
Pondamali,
Mimi nahisi wewe ni mtu mjuzi na tunaweza tukaunogesha huu
mjadala ukawa mzuri sana.

Ikiwa hisia zangu ni sawa nakuomba usihamaki ikakupelekea kutumia
lugha ambapo kwa mtu kama wewe kwa hakika haziwezi kuwa mahala pake mathalan, maneno kama ''ikala kwao.''

Ghadhabu zimekutangulia.

Hiyo si lugha yako hasa nikikusoma kwenye nukta na 2 unavyoandika
Kizungu kilichonyooka.

Turudi kwenye mnakasha.

Hili ndilo tatizo kubwa lililowapata Chuo Cha Kivukoni katika kuiandika historia ya TANU na wengi tatizo hili linawakuta kwa kudhani kuwa
wanaweza kuandika historia hii kutokana na fikra zao.

Wanajamvi,
Huu ndiyo sasa ugonjwa anaougua Pondamali.

Juzi hapa tumesikia ndugu yake Kasella Bantu na maneno yake nami nikampa taarifa kidogo za Kasella Bantu kutoka ''Nyaraka
za Sykes.''


Nikamwambia ikiwa atahitaji taarifa zaidi za mzee wake huyo basi  anifahamishe ili nimuwekee.

Kimya hadi sasa hajarudi.
Nachukulia kwa dhana nzuri labda hajasoma ile post.

Pondamali anaandika kutokana na moyo wake hana rejea moja
kuthibitisha hayo asemayo.

Kyaruzi hakubadili katiba yoyote kwani kazi ya kubadili katiba
ilipoanza yeye mwaka wa 1952 hakuwepo Dar es Salaam.

Aliyeshiriki katika kazi hii ya katiba alikuwa Dk. Michael Lugazia  siyo Dk. Vedasto Kyaruzi.

Hili suala la katiba nilishalieleza hapa jamvini.

Hapakuwa na katiba ya kuandikwa.

TAA walinakili neno kwa neno katiba ya Convention Peoples' Party (CPP) ya Nkrumah.

Kuhusu Political Subcommittee Kyaruzi kashiriki kweli lakini kweli
unadhani kwa wakati ule Kyaruzi, angeweza kumkabili Mufti Sheikh
Hassan bin Amir
 kwa jinsi siasa zilizyokuwa Dar es Salaam ya 1950 kumleta New Street?

Abdul ndiye aliyemleta Sheikh TAA kwa taadhima kubwa.

Au Kyaruzi angeweza kumkabili Said Chaurembo kuzungumzanae
kuhusu siasa na kumtaka aje kuwa mjumbe wa kamati ya siasa?

Dk. Kyaruzi kama si kuungwa mkono na Schneider Plantan yeye
asingeweza kwa nguvu zake kupata uongozi TAA.

Namshauri Pondamali asome Judith Listowel, ''The Making of Tangnayika,'' aone palikuwa na vurugu gani siku ile ya uchaguzi wa Arnautoglo Hall tena mbele ya maofisa Wazungu.

Mengi yalikuwa yanakwenda katika TAA kwa kuwa watu wa Dar es Salaam walikuwa wanamuona Abdulwahid pale si Kyaruzi.

Dk. Kyaruzi alikuwa mgeni.

Akina Sykes walikuwa na historia katika mji wa Dar es Salaam na
watu wakiwaamini toka enzi ya baba yao.

Fedha za kuendesha mambo akitoa Abdul na wenzake.

Nyumba ya kufanyia harakati hizo iliyokuwa na nafasi ilikuwa nyumba ya Abdul.

Ndiyo maana katika uongozi ule wa 1950 ilikuwa lazima na Abdul
awepo.

Dk. Kyaruzi peke yake asingeweza kitu.

Huu ndiyo ukweli wa historia hii ya TANU katika siku zile.

Ntatoka kidogo nje.

Huyu Schneider alikuwa askari wa Kijerumani na Vita ya Kwanza
ya Dunia kapigana dhidi ya Waingereza pamoja na Kleist Sykes.

Schneider alipigwa risasi mguuni vitani akawa anachechemea.

Alikuwa ana chuki kubwa sana na Waingereza kiasi cha kuwa katika
Vita Kuu ya Pili ya Dunia akawa anatembea katika mitaa ya Dar es
Salaam akinadi wazi hadharani kuwa yeye anamuunga mkono Hitler.

Waingereza wakamkamata wakamfunga jela Mwanza na hakutoka hadi vita vilipokwisha mwaka wa 1945.

Schneider ndiye mtu pekee katika historia kumtukana Nyerere
matusi makubwa uso kwa uso tena nyumbani kwake Msasani kwa kumweka kizuizini bila sababu.

''Advantage'' yangu mimi ni kuwa hawa watu mimi ni wazee wangu nikiwajua hadi walivyo na hulka zao kwa hiyo ninapoandika habari zao nakuwa na taarifa ambazo mtu mwingine hana na hii TAA ilikuwa chama walichokiasisi wao.

Mtafiti yeyote ambae anadhani anaweza kuandika historia ya TANU  nje ya Nyaraka za Sykes au nje ya maisha ya wazalendo hawa
atataabika sana.

Nimepita kwingi.

Hakuna nyaraka zaidi ya hizi.
Ikiwa Pondamali unazo nyaraka basi zilete hapa jamvini tunufaike
sote.

Sasa Pondamali kwa kukumalizia nitakuaga kwa nukta tatu.

Moja
Dk. Kyaruzi
 mwenyewe alipata kuandika makala katika gazeti la Rai kueleza mchango wake katika TAA hakusema hayo uliyosema wewe.

Mbili
Dk. Kyaruzi alichosema ni kuwa yeye ndiye  aliyemuachia Nyerere
chama na huu ni uongo dhahiri.

(Bahati mbaya rejea hii hadi sasa sijaiona katika maktaba yangu lakini naitafuta In Sha Allah nikiitia mkononi nitaileta jamvini).

Tatu
Dk. Kyaruzi aliandika kitabu cha maisha yake wakati Nyerere yu hai, mswada ule akawapa Tanzania Publishing House (TPH).

TPH wakakataa kuchapa kitabu kile.
Quote

Nini sababu?

Mimi sikuambiwa sababu lakini naweza kuhisi.

Last edited by Mohamed Said; Yesterday at 13:40.


TAA kwa Nyerere mwaka 1953. Jingine ni kuwa Kyaruzi wala hakuwa rais wa
kwanza wa TAA kwani chama kilianzishwa Dar es Salaam mwaka 1929 kikijulikina
kama African Association na wakati huo Dk Kyaruzi alikuwa bado mtoto mdogo.''

Taazia hii ilikataliwa kuchapwa labda wachapaji hawakutaka kuona yale walosema
yanakuja kupingwa.

Pondamali na wewe nakutia katika kundi la hao wanaoandika mambo ambayo
wao hawayajui.

Dk. Kyaruzi kama nilivyokuonyesha hapo juu hakuwa na muda mrefu katika uongozi
wa TAA kiasi cha kufanya hayo unayodai alifanya.

Kuhusu dai lako kuwa wazee wangu hawakufanya chochote hili wala sijishughulishi
kukujibu kwani ukweli kwa sasa uko wazi.
Shukrani nyingi sana moh said.

Wengi tupo tumetandika jamvi kukusoma.

Hatubanduki hapa.
o    like
faby likes this.
"IF YOUR LEGS CAN'T TAKE YOU TO PRAYER,THEN HOW DO YOU EXPECT THEM TO CARRY YOU TO PARADISE??"
2.    UNTOLD STORY is offline 
5th June 2014 16:28
#1223   Report Post    
UNTOLD STORY's Avatar
MemberArray
Join Date : 25th May 2014
Posts : 17
Rep Power : 305
Likes Received
12
Likes Given
0
Default
Quote By THE BIG SHOW View Post
Moh Said Endelea tupa maarifa mwalimu wangu.
salam: maalim hebu tupe muwangaza huyuu Mzee Sykes ni alikua nani? na asili yake ya wazee wake ni wapi?
o    like
3.     UNTOLD STORY is offline 
5th June 2014 16:41
#1224   Report Post    
UNTOLD STORY's Avatar
MemberArray
Join Date : 25th May 2014
Posts : 17
Rep Power : 305
Likes Received
12
Likes Given
0
Default
Quote By WildCard View Post
Ujumbe na elimu isiyo na vionjo vya DINI naamini inawaingia bara bara. Hivi kwa Kariakoo ya mwaka 1954-1970 ungepiga picha na akina nani?


Kwamba Mwalimu hakuweza kubadili DINI yake kama babazake Abdul kwa kweli anastahili pongezi kwa msimamo huo. Laiti angebadili dini, Mzee Mohamed angemwandika vizuri mno.
Nyerere angelibadili dini haya yote tusingelisubiri Mohammed Said kuyafichua. Nyerere angeyaandika mwenyewe.
o    like
4.    Mohamed Said is online now 
5th June 2014 16:50
#1225   Report Post    
Mohamed Said's Avatar
JF Senior Expert Memberhttp://www.jamiiforums.com/images/verified.pngArray
Join Date : 2nd November 2008
Posts : 5,674
Rep Power : 66188
Likes Received
4225
Likes Given
231
Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

Quote By pondamali View Post
Nina undugu na Mzee Kasella Bantu, ila tuyaache kwa kuwa huo ubinafsi hausaidii.
Waanzilishi wengi walitokea by default. Dr. Kyaruzi ndie alieweka infrastructure ya chama. Hao mnaowaita wazee wenu walikuwa na chama na hawakwenda popote kwa miaka mingi. Hadi watu wa bara walipoongoza ndio changes zikaonekana.
Pondamali,
Nimefurahi kusikia kuwa una udugu na mzee wetu 
Kassella Bantu.

Mimi nilipata mara mbili kukutananae.

Mara ya kwanza nyumbani kwa Chief Abdallah Said Fundikira, Magomeni Mikumi na mara nyingine nyumbani kwake Mzee Kasella BantuMwananyamala.

Kabla ya hapa nilikuwa nimekutana na mzee wetu kwenye Nyaraka za Sykes.
Humo ndimo nilipomsoma na kujaribu kumfahamu kutokana na yale niliyokuwa nayasoma.

Hebu nawe msome mzee wako kutokana na Nyaraka za Sykes hapa chini:

''Ally Sykes allowed me to interview him on many occasions in spite of his busy schedules managing his business from his city center office. He allowed me to consult his own private files, personal letters, diaries and other family records. These records were kept in a safe which I was informed remained untouched for over thirty years. Going through the files I was amazed by Ally Sykes’ obsession with record keeping. Every piece of paper with information was kept, however trifling it may have seemed during the struggle-a 1954 pencil note from Zuberi Mtemvu to Ally Sykes, informing him of a discussion he had with Nyerere about him and TANU; a 1953 money order receipt from Ally Sykesto Japhet Kirilo during the Meru Land Case; an undated copy of the letter from the TAA to Queen Elizabeth signed by the entire executive (the President, Julius Nyerere, Vice-President Abdulwahid Sykes, General Secretary Dome Okochi, Assistant Secretary Dossa Aziz,Treasurer John Rupia, Assistant Treasurer Ally Sykes) congratulating Her Majesty on her coronation; a 1952 letter from Rashid Mfaume Kawawa from Bukoba to Ally Sykes informing him of the political situation in the Lake Region; a 1963 letter from Lady Judith Listowel; letters from Kenneth KaundaJulius Nyerere
Kasella Bantu ... the list is endless.''

Pondamali,
Msome mzee wetu hapa chini tena:

''These were the veteran politicians of the African Association: John Rupia, middle-aged and rich, and 
Kasella Bantu who had studied in South Africa and had experienced violent white rule and its particular variant of apartheid. Kasella Bantu was very critical of the British. In South Africa he had quarreled with one European named Hugh TraceyTracey made a very incriminating confidential report against Bantu’s behaviour to the colonial administration. While working with the Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC), Bantu once again quarreled with a white officer who had called Africans ------. TBC was under the Social Development Department. When Bantu’s case was brought before the commissioner for social development, he referred to Bantu’s earlier report drawn by Tracey in South Africa. The commissioner concluded that Bantu was a troublesome African and he dismissed him from employment.'' [1]

Pondamali,
Haya niliyokuwekea kuhusu 
Kasella Bantu yanatosha au nikuongezee taarifa?


Hugh Tracey
Quote[1] Joseph P. Kasella Bantu to the Honourable the Chief Secretary, 27 th April, 1954. Sykes' Papers.

1.     Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
Quote By WildCard View Post
Mzee Mohamed,
Uliwahi kumwomba Mwalimu ambaye alikuwa hai wakati huo akupatie angalau upande wa pili wa TANU aliokuwa anaifahamu yeye kama RAIS wake wa KWANZA hadi wa MWISHO? Au ulishamhukumu tayari hata bila kumsikiliza!

Mimi sio mtafiti. Lakini, hata kama ningekuwa, nisingetafiti jambo zito la nchi kwa style hii ya kikatili namna hii.

WildCard,
http://www.ru.ac.za/media/rhodesuniversity/content/ilam/images/ht6_350.jpg
Hilo swali ulilouliza nilishaulizwa hapa jamvini na nikalijibu.
Nitakupa jibu na nitakupa na nyongeza.

Baada ya kujulikana kuwa naandika maisha ya Abdulwahid Sykes mmoja wa
vijana wake Nyerere katika watoto wa rafiki yake kipenzi alijitolea kuniombea
miadi (appointment) na Nyerere ili nimhoji.

Huyu jamaa yangu hakurudi tena kwangu hadi hii leo ninavyoandika.

Wakati natafuta publisher wa kitabu changu nilifika hadi Oxford University
Press (OUP) wakausoma mswada na taarifa ya mswada ikaandikwa.

Jibu lao kwangu ni kuwa kitabu ni kizuri sana lakini wao hawatoweza kabisa
kukichapa kwa sababu wao wana uhusiano mzuri na Nyerere na kitabu hiki
kimekwenda kinyume na vile Nyerere alivyokuwa akidhaniwa na wananchi
wake wengi.

Lakini wakaniongezea kitu kingine.

Wanasema wao walipatapo kiumshauri Nyerere kuhusu kuandika maisha
yake na akakataa.

Ikawa sasa nimeepata uhakika kuwa hili jambo la historia ya TANU ni kitu
nyeti kwa baadhi ya watu ikiwa hata OUP wanaogopa kuigisa kazi yangu.

Ndipo nikaelewa kwa nini hata ile historia iliyotaka kuandikwa na Abdul na
Dk. Klerruu haikuweza kukamilika.

Nikajisemea mwenyewe labda ndiyo maana hata yule jamaa yangu aliyetaka
kunifanyia miada na Nyerere hakupatapo kurejea kwangu kuniambia ilikuwaje.

Inawezekana kama anglikuja kwangu kunifahamisha kuwa Nyerere kakataa
kufanyiwa mahojiano kuhusu kitabu cha Abdul Sykes mimi hilo nigeliweka
katika kitabu changu.

Kwa ajili hii basi akona itakuwa salama kwa yeye kukaa kimya.
Na akaae kimya halaumiwi.

WildCard nina mengi sana ya kukueleza lakina kwa hili na tuishie hapa.

Unasema hili jambo la historia ya TANU ni zito.

Kwangu mimi hili ni jambo jepesi sana wala halikunitoa jasho kuliaandika au
kulizungumza.

Hata hao walimu wangu hawakuwa wanahema.

Walikuwa wakilizungumza tena wakati mwingine wakinichekesha wanasema,
''Mohamed unajua Nyerere alikuwa mwembambaaa na kitu kimoja bwana yeye
na Titi walikuwa wanajua kuwakomesha Waingereza utadhani wameambiana
nini waseme. Basi mambo yakinoga vigelegele kutoka kwa akina mama halafu
akina Yusuf Bakis na Sisso wanaingia kati na vimbwanga vyao. Ilikuwa raha
kwelikweli. Hatukupiga risasi hata moja kama Mau Mau. Waingereza wenyewe
wamefunga virago wamerudi kwao.''

Kitaanguka kicheko na mimi nitacheka.

Nyinyi maona uzito kwa kuwa hamna historia.
Kitabu changu kimekuwekeni katika hali ya mfadhaiko hamjui mfanye nini.

Ndiyo haishi maswali.
Nyerere umezungumzanae nk. nk. nk.

Nyerere atakuwa na lipi na yeye kaja 1952?
Mimi nina Nyaraka za Sykes toka 1929.

Nina babu yangu Salum Abdallah, 1947 kaongoza ''general strike''
dhidi ya Waingereza, 1953 yuko katika kamati ya siri ya TAA kuunda
TANU, 1955 rais muasisi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU).

Sikupatapo kuwa na upungufu wa kujua mambo.

Wala kama usemavyo ''style,'' hiyo style wala haina mushkel wowote
na ni aina katika aina nyingi za uandishi wa historia.

Inaitwa, ''Biographical Approach.''

FaizaFoxy 
keshakusomesha kanuni hii lakini wewe kichwa chako kigumu
sana - BAI

Ndipo ninapokueleza usiingie kutaka kuvuka mkondo wa Kigamboni
nawe huna boya wala hujui kuogelea.

Utazama.

Usiyafanyie haraka mambo haya.

Kaa chini, piga goti, pinda mgongo kwa waalimu wakosomeshe ndipo
utajua.

Hii yote walimu wangu wako katika kanzu na bargashia.
Hawa walimu hatari sana.

Ni vibaya sana kulizungumza jambo usilokuwa na ujuzi nalo.
Utajifedhehesha bure.
Last edited by Mohamed Said; Today at 16:32.
wabara and sahim1 like this.



Hugh Tracey
QuoteLast edited by Mohamed Said; 5th June 2014 at 18:54.
pondamaliRitzfaby and 2 others like this.

No comments: