- Mshume Kiyate,
Wakati mwingine mie hupigwa na butwaa khasa.
Yaani kuna mambo Maalim Haruna alikuwa akitufundisha ndiyo leo
nayaona.
Alikuwa anasema, ''Kila yule ajionae kuwa yeye ana nguvu sana basi
kaa ukijua ana kitu anakiogopa. Ukishajua kitu kinachomtia hofu basi
jua kile kibri chake chote Allah kesha kiondoa.''
Mimi nikawa najiuliza.
Hivi mna kitu gani cha kutisha katika maisha ya Abdul Sykes kiasi
juhudi kubwa ije ichukuliwe kumfuta katika historia?
Nikawa najiuliza hivi haya nishuhudiayo ni kweli au niko katika ndoto?
Iko siku ndugu yangu mmoja kaja kunipa habari.
Anasema yeye alikuwa kasimama kwa muuza magazeti Tancot House.
Mara ikaja Volkswagen Kombi ikapaki akashuka mtu akauliza Africa
Events alipooneshwa akayanunua yote.
Hii ilikuwa April 1988.
Ilipofika mwezi Septemba ikiwa miaka 20 kamili imetimia tangu Abdul
Sykes afariki.
Africa Events wakachapa makala ya kumbukumbu ya kifo chake: M.
Said, ‘Founder of a Political Movement: Abdulwahid K. Sykes 1924-
1968’, Africa Events, London September, 1988, pp. 38-41.
Katika makala hii bila kuuma maneno nikaandika nikasema Abdul
Sykes ndiye aliyeunda TANU.
Nikakaa nasubiri kama CCM Dodoma safari hii watakuja na majibu
ya vitisho na fedhuli.
Kimyaaaa!
Dk. Kiwanuka hakunyanyua kalamu kunijibu.
Wala gazeti halikukusanywa.
Kuna watu wakanifata kuniuliza kuhusu historia ya TANU na kwa
nini naandika vile.
Mimi nikawaeleza kuwa mimi sina nia ya kupingana na historia
inayofahamika na ambayo ndiyo rasmi.
Huenda hakika kulikuwa na watu wawili wote wana fikra moja ya
kuunda TANU.
Huyu mmoja yeye historia yake ya kuasisi TANU inafahamika lakini
huyu wa pili yeye ni marehemu, historia yake si wengi wanaijua.
Kwa kuwa mimi historia hii naijua ndiyo nimeamua kuitafiti na
kuiandika ili nayo ijulikane isipotee.
Hili ndilo likawa jibu langu makhsusi kwa kila aliyekuja kuniuliza
kuhusu historia ya Abdul Sykes na TANU.
Sasa ngoja nikurudishe kwa baba yangu, Said Salum Abdallah.
Baba yangu alikuwa Tabora ameshastaafu.
Gazeti lile la Abdul Sykes akalipata.
Basi nasikia alikuwa kila anaepita lazima amwonyeshe picha ya rafiki
yake Abdul ndani ya gazeti kisha amsomee yale niliyoandika.
Akimaliza kumsomea makala ile sasa anasherehesha vipi yeye alijuana
na Abdul vipi Abdul alivyomjulisha kwa Nyerere nyumbani kwake
mwaka 1952 nk. nk.
My old man was really having a good time...
Kama alivyoimba Ray Charles, ''Let the good times roll.''
Mshume Kiyate,
Mimi hivi ndivyo nilivyokuwa nikiwasikia wazee wangu wakihadithia
historia ya uhuru.
Bibi yangu Bi. Zena biti Farijala hero wake yeye alikuwa Harry
Belafonte.
Kwa nini?
Babu yangu alimpeleka kwenda kuona movie: ''Island in the Sun.''
Stori ilikuwa mapambano dhidi ya ukoloni.
Hii ilikuwa 1957.
Google utapata synopsis ya hii movie.
Hii dunia ndogo sana, tena sana.
Niko New York.
Nakaa karibu na Hudson River, Manhattan.
Mwenyeji wangu katika mazungumzo ya hapa na pale tumezungumza
kuhusu wanamuziki wakubwa wa wakati wetu mie nikamkumbuka
Harry Belafonte.
Basi yule bwana akanyoosha kidole akanambia, ''Ukivuka hapo
Hudson River ndiko iliko nyumba ya Harry Belafonte.''
Nikikitazama hiki kitabu namkubuka mke wangu, Zena biti Farijalana movie yake aliyokuwa heshi kuihadithia ya ''Island in the Sun.''
Wakati ule Belafonte alikuwa katoa kitabu cha maisha yake kakipa
jina la ''My Song.''
Ninacho katika maktaba yangu.
Nafyonza Ilm shukran sana Mzee Mohamed Said.
Saturday, 14 June 2014
KUTOKA JF: AFRICA EVENTS NA HISTORIA YA TANU 1988
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment