1. Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia
mbele ya haki
Siyo lazima mtu awe "msemaji" wa familia kutambua kwamba hizo
familia husika wamechafuliwa majina yao kwa kuwahusisha na chuki na udini
uliokubuhu wa Mohamed Said. Nakwambia hivyo from my own perspective as a
neutral outsider, and not necessarily from the perspective of the affected
individuals or families. Kama hawa "walitupwa nje ya historia ya
Kivukoni" kama unavyodai, basi sababu mbadala za kisekulari zipo nyingi
kama Wachangiaji wengine walivyojaribu kuweka wazi hapo nyuma.
Mohd Sewer N Waste,
Mshume Kiyate alikuuliza mbona unakuja na Double ID?
Umekaa kimya hukumjibu.
Pale uliporudi na hii ID ya kunitukana ID hii hiyo ndiyo ilikuwa post
ya kwanza.
Mimi nilikuwa nimeweka post ya kueleza hatari ya kujaribu kumfuta
Abdul Sykes katika historia.
Post ile haikukushughulisha ulichokiona cha maana kwako ni kurudi
jamvini kunitukana.
Si kitu.
Maalim Haruna alikuwa akitufundisha akisema, ''Ukiona mwenzako
katika mnakasha anatumia matusi basi jua ushamshinda kwani hiyo
ni dalili wazi ya ghadhabu na mwenye hoja haghadhibiki.''
Wewe huna hoja, umeghadhibika kwa kushindwa na umeona njia
nyepesi yakuondoa fedheha ya kushindwa ni kunitukana - Mohd
Sewer and Waste.
Mimi siwezi kujibu matusi yako ila nitakueleza wewe na nitalieleza
jamvi yale niyajuayo.
Ilikuwa nia ya Ally Sykes katika miaka ya 1980 kuwapa waandishi
nyaraka zao ili waandike historia ya baba yake, Kleist na ya kaka
yake Abdul ambayo ingelieleza historia ya TANU.
Mimi nilimwambia Ally Sykes kuwa mimi naweza kuandika historia
hiyo.
Nilimpa ''draft'' ya sura moja tena wakati huo sijui hata kutumia
computer kwa hiyo ilikuwa nimeandika kwa mkono.
Ilikuwa mwaka wa 1988.
Ally Sykes alichukua ile sura akendanayo London akampa Mohamed
Mlamali Adam aliyekuwa mhariri wa Africa Events, gazeti lililokuwa
likichapwa London.
Sura hii ilichapwa kama makala katika gazeti la Africa Events toleo
la March/April 1988 kwa kichwa cha habari, ''In Praise of Ancestors.''
Toleo hili ndilo lililokusanywa na kupigwa moto hapa nyumbani.
Hawakutaka watu wasome kile nilichoandika.
Kitendo hiki na jinsi makala ile ilivyopokelewa ilimfanya Ally Sykes
aamini kuwa hakuwa na haja ya kuwaleta waandishi kufanya utafiti
na kuandika historia ile kwani mimi kazi ile nilikuwa naimudu ile kazi.
Sasa nataka nikurudishe katika ''kuchafua na kupaka matope ''legacies''
za Sykes na Aziz.''
Mimi na hao waliochoma moto toleo lile la Africa Events kwa kumtaja
Abdul Sykes na Dossa Azizi na wengineo kama waasisi wa TANU
nani alikuwa kwa hakika anachafua na kupaka matope ''legacy'' ya
koo hizo mbili?
Umezungumza kuhusu chuki.
Kwa haya niliyoyaleta hapa jamvini nawaomba wanajamvi waamue
ni nani mwenye chuki?
Yule aliyeshika kijinga cha moto kuchoma historia au mwandishi wa
hiyo historia inayounguzwa?
Nani mwenye chuki mie au wewe unaetukana?
Mwenye chuki na hasad noyoni ni nani?
Mie niliyeandika niliyeshika kalamu kuandika yale ambayo nahisi kuwa
wanahistoria yamewapita kuandika kwa makusudi au kwa kutokujua
au yule anaetia moto historia asiyoipenda?
Nikuulize tena Mohd Sewer N Waste,
Mimi na hao waliotia kibiriti toleo lile la Africa Events nani alikuwa
kwa siri anapaka matope historia?
Hutokaa ukajua na kwa kweli mimi nimeacha mengi kuandika ambayo
Ally Sykes alinieleza.
Nilimsihi hayo tuyaache kwa sasa na msimamo wangu ulikuwa mengine
na tuwaachie watafiti wengine waje kuandika.
Mohd Sewer N Waste,
Ungependa nikueleze yale ambayo nilimkatalia Ally Sykes kuyaweka
katika kitabu?
Laiti ungeliyajua...
Usingekuja na huo mchezo wako wa kitoto.

Last edited by
Mohamed Said; Today at 06:08.
No comments:
Post a Comment