Sunday, 10 August 2014

KUTOKA JF HAMAKI NA GHADHABU KUHUSU KITABU ''KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU''

Quote By Ndjabu Da Dude View Post
Sijaona hata sehemu moja ametaja kapitia madrassah Fulani kwenye CV au resume yake ya Wikipedia huyu "Mwana Msomi wa Allah"?Minafiki iliyotukuta inayojifanya "maislamu" kama Sheikh Mohamed Said, Ritz, et al inaishia kumsifu kwa "usomi" wake wa vyuo kama Harvard, hadi kudiriki kunena eti haiwezakani kupingana naye kwenye jambo lolote yote sababu kasoma Harvard. Halafu hapo hapo utaona vimbuzi mtu kama hao wamefanya kulaani "mfumo kristo" bila kuelewa kuwa elimu ya vyuo vikuu vya dunia ya leo isingekuwapo bila ya mchango pekee na mkubwa wa kanisa Katoliki. Matter of fact, watu kama Mohamed Said wasingefika hapo walipo bila ya kwenda shule za misheni kama St Joseph's enzi hizo. Daadeki, kitabu kimoja kaandika "mwana wa Allah", msomi wa Harvard kinawafanya "maislamu" ya dizaini ya Mohamed Said WAMSUJUDU mtu kama huyu mwandishi, sambamba na yule super hero mwingine wa watu hawa, Kighoma Malima, aliyesoma Princeton University. Halafu bila aibu, achilia mbali ushahidi wowote Mohammed Said anakujana kaulia eti somebody Sykes, yule super hero mwingine wa hii clique, eti naye alikubaliwa na Princeton University aanze masomo pale?

Ndjabu Da Dude,
Umenitaja.

Kisha lugha yako naona umeghadhibika.
Umetumia maneno, ''minafiki,'' ''maislamu,'' nk.

Waungwana hawatukani.
Muungwana hajibu matusi wala lugha mbaya.

Muungwana hukaa kimya au atanasii.

Kwa kawaida na kwa hakika hili lipo katika akida yangu mie mtu akinitaja 
huwa simwachi lazima In Sha Allah nitampa jibu.

Lakini maalim wangu Sheikh Haruna alikuwa akitufunza katika madras 
anasema mtu yoyote aliyeghadhibika hafai kufanyanae mnakasha.

Alikuwa akiendelea kusema kuwa hafai kufanyanae mnakasha hadi hapo yeye
atakapotulia.

Akisema kuwa itakuwa bora ikiwa utaweza kumpa maneno mazuri, mnasihi 
ili hasira zake zipoe.

Maalim Haruna akisema mtu mwenye ghadhabu hawezi kufikiri sawasawa 
kwani anakuwa kama nusu, ''Pesambili Potea.''

Huyu Pesambili Potea alikuwa mwendawazimu wa Kihindi na ndiyo tulipokuwa
watoto alikuwa kichaa maarufu Dar es Salaam ya 1950/60s.

Pesambili Potea akicharuka alikuwa akitukana ovyo na kupopoa watu mawe.

Kwa mafunzo haya ya Maalim Haruna mimi nakusihi ndugu yangu punguza 
hamaki.

Hapa jamvini tunajadiliana tu si mahali pa kutukanana.

Hapa ni mahali pa kubadilishana fikra.
Punguza ghadhabu.

In Sha Allah utapokuwa umetulia nifahamishe nami nitarejea hapa jamvini
na tutafanya mjadala wa heshima.

Watazamaji In Sha Allah watastarehe kama kawaida utakapotulia na mimi
nikakupa majibu yangu.

Nitakueleza kwa nini katika CV zetu hatuweki vyuo tulivyosoma utotoni
tukiwa na miaka 6 na kuendelea.

Chembelecho Faiza Fox sisi tunaingia chuoni watoto wadogo nyie wenzetu
mnaingia chuoni watu wazima.

No comments: