Friday 8 August 2014

KUTOKA JF MSOMAJI AITA KUMBUKUMBU YA KLEIST SYKES YA VITA KUU YA KWANZA ''HEKAYA''


Quote By Pol Pot View Post
Shukraan al mudeer hi ni elimu kubwa sana

Pol Pot,
Wajib wetu kuhifadhi historia ya wazee wetu.

Kipande hiki cha Vita Vya Pili Vya Dunia nilikipata kwa njia ya ajabu kidogo.
Mimi nilikuwa nishakamilisha utafiti na kuandika.

Mswada ulikuwa unasubiri mchapaji (publisher).

Katika mahojiano yangu na marehemu Bwana Ally Sykes wakati wa utafiti 
kila mara alikuwa akitaja jalada la moja ambalo alikuwa akinambia kuwa lina 
taarifa muhimu.

Alikuwa akinambia kuwa jalada hili lilikuwa mikononi kwa marehemu kaka
yake Bwana Abdulwahid Sykes.

Siku moja nikakutana na Ally Sykes Msikiti wa Manyema katika maziko.
Ally Sykes akanambia, ''Mohamed njoo ofisini lile ''file'' la Bwana Abdu
nimelipata.

Katika jalada lile ndipo nilipokutana na mengi na mojawapo ni hizi ''War
Diaries,'' za Lance Corporal Kleist Sykes.

Nikarudi tena mezani kuongeza yale niliyokwishaandika.

Ndipo nilipojua kwa nini jalada lile lilimtaabisha sana Bwana Ally Sykes 
hadi alipoliona tena.

Nimesoma hapa jamvini kuna mtu kaghadhibishwa na kumbukumbu hii 
na kaandika mistari ya kukejeli hizi ''Shajara za Vita Kuu Vya Kwanza 
Vya Lance Corporal Kleist Sykes,'' ameziita ''hekaya.''


Mara nyingi kila nilipokuwa nikizungumza na Mzee Kitwana Kondo 
alikuwa na msemowake akipenda kuusema, ''It takes all sorts of people 
to make the world go round.''

Kwa hiyo mimi namtia Bwana ''Hekaya,'' katika kundi hilo.
Kama si Bwana, ''Hekaya,'' nisingepata hamu ya kuandika haya.

In Sha Allah nitaweka hapa jamvini maandishi ya mjukuu wa Kleist,
Bi. Daisy Aisha Sykes aliyoandika mwaka wa 1968 kuhusu maisha ya 
babu yake akiwa vitani kati ya mwaka wa 1914 na 1918.

Huenda Bwana ''Hekaya,'' akaamini kuwa hiyo ni historia ya kweli na 
wala si ''hekaya.''

No comments: