Thursday 23 October 2014

SAFARI YA HIJJA 1435/2014

Nilikuwa katika kundi la Waislam waliopata mwaliko kutoka kwa Mfalme wa Saudi Arabia, Mfalme Abdulla kufanya hijja mwaka huu. Mwaliko huu ulitumwa kwa wengi Afrika nzima na tulikujafahamiana pale tulipokutana wote Addis Ababa tarehe 29 Oktoba na tukaletewa  ndege maalum ya Saudi Arabia Airlines kuja kutuchukua kutupeleka Jeddah kisha kuchukuliwa na mabasi kwenda Makka siku hiyo hiyo usiku. 

Waalikwa walikuwa katika makundi tofauti kutokana na wanayofanya katika kuutumikia Uislam. Kundi letu lilikuwa na watu wanne kutoka radio za Kiislam Tanzania - Sheikh Shamsi Elmi wa Radio Quiblatein (Iringa), Nadir Mahafoudh wa Radio Nur (Zanzibar), Sheikh Mohamed wa Radio Istiqama (Pemba) na Mwandishi akiwakilisha Radio Kheri (Dar es Salaam), Sheikh Arif Nahdi wa Radio Imaan (Morogoro) alipata mwaliko lakini hakujaaliwa kuhudhuria. 

Jumla yetu tulikuwa watu 28 kutoka Tanzania Kama nilivyosema mwaliko huu ulitumwa kwa wengi Afrika nzima na tulikujafahamiana pale tulipokutana wote Addis Ababa tukisubiri ndege maalum ya Saudi Arabia Airlines kuja kutuchukua kutupeleka Jeddah. Hapo Uwanja wa ndege wa Addis Ababa ndipo tulipokuta wenzetu kutoka nchi nyingine za Afrika. Kulikuwa na waalikwa kutoka Lesotho, Afrika Kusini, Namibia, Nigeria, Benin, Mali, Chad na kwengineko. 

Tuliswali Salat Fajr na Dhuhr katika Uwanja wa Bole Addis Ababa. Tulihirimia Uwaja wa Ndege Addis Ababa na kuvaa Ihram zetu. Kutoka Addis Ababa tukachukuliwa na ndege ya Saudi Arabia Airlines kuelekea Jeddah. Tuliswali L' Asr na Maghrib katika Uwanja wa Mfalme Abdulaziz, Jeddah. Kutoka Jeddah tukachukuliwa na mabasi kwenda Makka siku hiyo hiyo usiku. 

Waalikwa kutoka Tanzania walikuwa masheikh kama Sheikh Muhammad Iddi Mkurugenzi wa Al Risala International, waalimu wa madrasa na viongozi wake kama Ali Kondela kutoka Tabora, walimu wa shule, waandishi kama Mzee Khalid Mtwangi mwandishi mashuhuri wa makala za Kiislam, Sheikh Khatib Girigiza Mhadhiri kutoka Chuo Cha Diplomasia, Kurasini Dar es Salaam, Muhajir Kachwamba mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mkuu wa Chuo Cha Kiislam Morogoro (MUM) Prof. Hamza Njozi,  nk. 

Tafadhali angalia picha...



Mahujaji Watarajiwa Katika Semina ya Jinsi ya Kutekeleza Ibada ya Hijja

Hafla ya Kuwaaga Mahujaji Iliyotayarishwa na Tanzania Haj Trust Mgeni Rasmi Akiwa Rais Mstaafu Sheikh Ali Hassan Mwinyi Mwandishi Akimkabidhi Mgeni Rasmi Nakala ya Kiingereza na ya Kiswahili ya Kitabu Cha Abdulwahid Sykes

Mahujaji Wakiagana na Ndugu na Jamaa Kabla ya Kupanda Ndege Kuelekea Saudi Arabia
Sheikh Katungunya wa Msikiti wa Manyema Muda Mfupi Kabla Hajapanda Ndege Kwenda Saudi Arabia

 


Dufu Kuwaaga Mahujaji

Viongozi wa Haj Trust  Wakiongozwa na Mohamed  Ghalib Wakiwahudumia Mahujaji Uwanja wa Ndege
Mahujaji wa Zanzibar na Bara Walipokutana Uwanja wa Ndege Siku ya Safari

Add caption
Kushoto Kwenda Kulia: Sheikh Salim, Sheikh Mohamed Iddi na Sheikh Mbwana Urari Mratibu wa Safari ya Mahujaji Waalikwa Siku ya Safari Uwanja wa Ndege















Makka
Kushoto Kwenda Kulia: Mwandishi, Sheikh Nadir Mahfoudh, Sheikh Mohamed na Sheikh Shamsi Elmi



Sheikh Khatib Girigiza Akitoa Maelekezo kwa Mahujaji wa Tanzani Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa
Sheikh Nadir Mahfoudh Akiwa Ndani ya Ihram Uwanja wa Ndege Addis Ababa
Sheikh Nadir na Sheikh Muhammad Iddi Uwanja wa Ndege Addis Ababa
Displaying 20140929_121139.jpg
Mzee Khalid Mtwangi 

Wasafiri Katika Basi la Uwanja wa Ndege
Makka

Masjid Nabbawy Madina

Sheikh Nadir na Mwandishi Wakipumzika Baada ya Tawafu na Sai


Mzee Khalid Mtwangi na Mwandishi

Mwandishi Kushoto na Sheikh Nadir Mahfoudh Wakikaribishwa Hotelini  kwa Kupewa Maji ya Zam Zam
Kushoto Kwenda Kulia: Sheikh Nadir Mahfoudh, Mwandishi, Sheikh Mohamed, Sheikh Shamsi Elmi
Sheikh Abubakar mwanafuzi wa Afrika University Sudan na  mfanyakazi wa TV Afrika Khartoum  Akiwa Makarim Ummul Qura Hotel Makka 
Babu Ali Mbele ya Kaaba
Mahujaj Wakielekea Jamarah Kupiga Mawe
Mahujaji Wakiwa Muzdaliffa
Kushoto Kwenda Kulia: Sheikh Nur Mohamed (Mbeya), Sheikh Shamsi Elmi (Iringa) na Sheikh Mohamed (Pemba)
Displaying 20141001_191500.jpg
Sheikh Nadir Mahfoudh Akizungumza na Waendesha Rado Kutoka Afrika ya Kusini

Mzee Khalid Mtwangi Uwanja wa Ndege Addis Ababa
Sheikh Kassim Haidar Al Farsy wa TV Africa Zanzibar Uwanja wa Ndege Addis Ababa
Mahujaji Wakiwa Uwanja wa Ndege Addis Ababa

Makka


Sheikh Shamsi Elmi Katika Moja ya Semina za Radio Makka
Watu Mashuhur Waliokuja uongea na Mahujaj Katika Hotteli Waliyofikia
Masjid Nabawy Picha Kutoka Dirisha la Hotel 

Sheikh Shamsi Elmi Akiwa Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa Akifanya Kazi Wakati Akisubiri Safari ya Jeddah

No comments: