Kipindi Maalum Radio Kheri '' Sheikh Ali Muhsin Barwani (1919 - 2006)
Msomi, Mwanasiasa, Mshairi, Mhariri wa Gazeti, Mwandishi wa Vitabu, Mwalimu na Mfasiri wa Qur’an Tukufu
Kumbukumbu yaMiaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar''
Chini Kwenye Ngazi ya Ndege Ali Muhsin Barwani, Mohamed Shamte, Hasnu Makame na Abeid Amani Karume |
Sheikh Ali Muhsin
Barwani wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar alikuwa kiongozi wa Zanzibar
Nationalist Party (ZNP) vilevile chama hiki kikijulikana kama Hizbu. Kwa
mapenzi makubwa wanachama wa Zanzibar walikuwa wanamwita, “Zaim” yaani
Kiongozi. Ilikuwa nia ya Sheikh Ali Muhsin Zanzibar ipiganie uhuru wake chini ya
chama kimoja cha kizalendo chenye nguvu chama cha kitaifa badala ya vyama vilivyojijenga
katika misingi ya rangi. Ilikuwa pigo kubwa sana kwake Abeid Amani Karume alipoasisi
Afro Shirazi Party, chama kilichosimama kwa maslahi ya Waafrika na Washirazi. Sheikh
Ali Muhsin alipigania uhuru wa Zanzibar mpaka ukapatikana tarehe 10 December
1963. Sheikh Ali Muhsin alishiriki katika mkutano wa katiba Lancaster House.
Baada ya mapinduzi yaliyotokea Zanzibar tarehe 12 Januari 1964 Sheikh Ali
Muhsin alikamatwa na kusafirishwa Tanganyika ambako alifungwa Ukonga na jela
nyingine kwa kipindi cha miaka 10 na miezi michache. Katika kipindi alichokuwa
kifungoni Sheikh Ali Muhsin aliandika miswada kadhaa ambayo alikuja kuichapa
kama vitabu baada ya kutoka kifungoni. Kabla hajafa mwaka 2006 Sheikh Ali Muhsin aliandika kitabu cha
maisha yake, ‘’Conflict and Harmony in Zanzibar,’’ ambacho kilikuja kufasiriwa kama ‘’Kujenga na Kubomolewa Zanzibar.‘’
Katika kitabu hiki cha maisha yake Sheikh Ali Muhsin anaeleza yaliyopitika
Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi. Baada ya kushindwa kupata pasi ya
kusafiria, Sheikh Ali Muhsin alitoroka nchini mwaka 1974. Hadi anafariki siku zote Sheikh Ali Muhsin alikuwa akisema yale hayakuwa mapinduzi bali mavamizi.
Mwandishi Akisoma Kutoka Kumbukumbu za Sheikh Ali Muhsin Barwani |
Studio za Radio Kheri Kipindi Maalum Cha Mapinduzi ya Zanzibar |
Studio za Azam TV Kipindi Maalum Cha Mapinduzi ya Zanzibar |