Jana baada ya Baraza Kuu kutoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba Iliyopendekezwa mara moja niliweka tamko lile hapa na nikaweka kwenye Jamiiforums. Watu walianza kuchangia katika JF lakini hata kabla ya saa 24 kupita mjadala ukafungwa na Moderator. Hapa chini ni baadhi ya yale niliyochangia JF kujaribu kuwaeleza wanaopinga Mahakama ya Kadhi nini hasa Mahakama ya Kadhi na historia yake:

By
kilapalio 
Mimi sina shida kama ntakatwaa kodi ikaenda kujenga zahanati na kununua madawa vijijini na kujenga barabara zitakazowasaidia watz wote bila kujali Dini,kabila rangi na jinsiaa naomba tuongee kwa Facts hizi mahakama za kadhi zinamsaidiaje mtz ambaye sio muislamuu na ambaye amwamin Mungu kwa mfano? Na la pili hizo Mou zinazotengezwa na serikali kupelekaa hela kwenye mashirika ya Dini naomba uzitaje as far as in know kuna PPP privat And Public partnership za Hospital za Mission zinazopokea grants kutoka serikalini kuwahudumia watz wote regardless of their faith nimejaribu kuuliza na nikaambiwa kuwa mahakama ya kadhi inaendeshwa kwa misingi ya shariah law na tunaona Nchi nyingi zilizopo Afrika zinazoendeshwa kwa misingi ya shariah law ndio zenye worst Record of human rights eg Sudan na northern Nigeria kwahiyo Said kama mtz mwenzangu Bado haujaniconvince You can have your mahakama ya kadhi but not with Tax Money sorry!!!!

By
Mohamed Said 
Chuakachara,
Jitulize na fanya mjadala wa maana kwa kuangalia ukwel wa
mambo.
Wapagani?
Ikiwa wapo na wana mahitaji yao serikali inawajibika kwao.
Lakini nakufahamisha kuwa Waislam katika Tanzania na katika
iliyokuwa Tanganyika wana historia ya kipekee na ukisoma hiyo
historia ndipo utawajua.
Anza na Vita Vya Maji Maji kisha njoo katika kupigania uhuru wa
Tanganyika.
Ndani ya historia hii kuna mengi ya kujifunza.
Ukitoka hapo njoo sasa katika historia ya Waislam baada ya uhuru
hadi sasa.
Ukisoma hayo yote utajua kuwa Waislam kama jamii walikuwa na
mahitaji yaomaalum na ndiyo yaliyowafanya kunyayua silaha dhidi
ya Wajerumani na ndiyo mahitaji hayo hayo yaliyowafanya wawe
mstari wa mbele kudai uhuru.
Turudi kwa Wapagani.
Ikiwa na wao kama jamii ya Watanganyika itafute historia yao dhidi
ya ukoloni ili ujue nini walichokuwa wanataka wakati ule na nini wa
nataka hivi sasa.
Usiwafananishe Wapagani (ikiwa wapo) na Waislam mfano huu
wako hauenei kwa kila hali.
Mahakama ya Kadhi ilikuwapo Wajerumani waliikuta na Waingereza
pia na waliziheshimu.
Mahaka ya Kariakoo nyuma ya Posta ya Kariakoo ilikuwa mahakama
ambayo Sheikh Said Chaurembo akihukumu ndoa, talaka na mirathi.
Mnazi Mmoja ilikuwapo mahakama pale na mmoja wa mahakimu
wake namkumbuka alikuwa Sheikh Kassim Juma.
Tabora Liwali Bilal Mshoro alikuwa akihukumu halikadhalika Songea
alikuwapo Sheikh Abdallah Simba.
Moshi alikuwapo Liwali Mussa Minjanga akihukumu pale Bomani.
Mahakama hizi zilikuwapo hadi mwaka 1963 na zikavunjwa kimya
kimya.
Mahakama hizi zilikuwa zikigharimiwa na serikali na zilikuwapo nchi
nzima popote walipokuwapo Waislam.
Ningependa kumaliza kwa kusema baadhi ya hao masheikh mahakimu
wakifahamiana vyema sana na babu yangu Salum Abdallah na mimi
nimewaona kwa macho yangu.
Hii ndiyo historia ya Waislam wa Tanganyika na Mahakama ya Kadhi.
Tuendelee na mjadala ikiwa utapenda In Sha Allah.
Historia hii haina maana, labda enzihizo, nafkiri ndio mana hiyo mahakama ya kadhi ilifutwa "kama kweli ilikuwepo" leo hii utamshawishi nani akubali kulipia gharama za ibada ya mtu mwingine. Kwanza ni aibu kulazimisha kuhudumiwa.

By
Mohamed Said 
Kilapalio,
Hutaelewa kwa kuwa ulichotanguliza ni ''choyo.''
Waislam na Uislam utanufaika.
Ungetanguliza mapenzi na udugu usingepata shida wala hofu.
Nadhani unajua kuwa Kanisa linapokea fedha kutoka serikalini
kuendesha mambo yake.
Je uko tayari kuona Waislam wanatengewa fedha na serikali
kwenda misikitini kuendesha miradi ya Kiislam?
Ukitaka zaidi katika haya Faiza Foxy tunae hapa yeye ni mtaalamu
wa MoU kati ya Serikali ya Tanzania na Makanisa.
Ni mabilioni ya shilingi...
Mambo haya yanataka akili iliyotulia si mambo ya ushabiki na kukimbilia
kusema.
Inataka tafakuri.
Inahitaji stahamala vinginevyo tutaiangamiza nchi.
Nchi iangamizwe mara ngapi
No comments:
Post a Comment