http://www.mohammedsaid.com/2015/01/skh-ali-muhsin-barwan.html
Kipindi Maalum Cha Mapinduzi ya Zanzibar
Radio Kheri
Kumbukumbu ya Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Sheikh Ali Muhsin Al – Barwani 1919 – 2006
Msomi , Mwanasiasa, Mshairi, Mhariri wa Gazeti, Mwandishi wa
Vitabu, Mwalimu na Mfasiri wa Qur’an Tukufu
Sheikh Ali Muhsin Barwani |
Sheikh Ali Muhsin
Barwani wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar alikuwa kiongozi wa Zanzibar
Nationalist Party (ZNP) vilevile chama hiki kikijulikana kama Hizbu. Kwa
mapenzi makubwa wanachama wa Hizbu walikuwa wanamwita, “Zaim,” yaani ''Kiongozi.'' Sheikh Ali
Muhsin alipigania uhuru wa Zanzibar mpaka ukapatikana tarehe 10 December 1963.
Sheikh Ali Muhsin alishiriki katika mkutano wa katiba Lancaster House. Baada ya
mapinduzi yaliyotokea Zanzibar tarehe 12 Januari 1964 Sheikh Ali Muhsin
alikamatwa na kusafirishwa Tanganyika ambako alifungwa Ukonga na jela nyingine
kwa kipindi cha miaka 10 na miezi michache. Katika kipindi alichokuwa kifungoni
Sheikh Ali Muhsin aliandika miswada kadhaa ambayo alikuja kuichapa kama vitabu.Kabla
hajafa mwaka 2006 Sheikh Ali Muhsin aliandika kitabu cha maisha yake ambayo ni
kumbukumbu ya yote yaliyopitika Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi. Baada ya kuachiwa kutoka kifungoni mwaka 1974 Sheikh Ali Muhsin baada ya kuona kuwa hatoweza kuondoka nchini kwa kuwa alinyimwa pasi ya kusafiria, Sheikh Ali Muhsin alitoroka nchini na kukimbilia Kenya ambako kwa msaada wa UNHCR aliweza kusafiri kwenda Cairo.
Hassan Abdallah Khamis Akiendesha Kipindi Cha Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Akimhoji Mwandishi |
Mwandishi na Sheikh Ali Muhsin Barwani, Mascut Oman 1999 |
Mwanamapinduzi Akimvuta Ndevu, "Muarabu." |
Mwanamapinduzi Katika Kofia ya Chuma na Mkononi Ameshika Panga |
Mwandishi Akifanya Kipindi Cha Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Akisoma Kutoka Kitabu Alichoandika Sheikh Ali Muhsin Barwani ''Kujenga na Kubomolewa Zanzibar'' Bonyeza Hapo Chini Kukisikiliza Kipindi |
1 comment:
ASALAM ALAYKUM!
Mwenye kutaka kujua ukweli upo wapi ni kuangalia na kuyasikiliza yanasomewa na pande mbili tafauti, kisha nikuyapima yale ambayo ameyasikia na kuyasoma na kuja na uamuzi bila ya kufwata mkumbo.
Katika wanaoyapima ya pande mbili mie ni mmoja wapo kwahio nasubiri, hio Audio niendelee kujifunza.
Post a Comment