Monday 12 January 2015

KUTOKA JAMIIFORUMS KUHUSU MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Quote By chabuso View Post
Ukitaka kijua historia ya John Okelo na historia ya mapinduzi ya Zanzibar soma hichi kitabu http://kwaheri.files.wordpress.com/2010/05/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf, katika kitabu hichi utapa ufafanuzi wapi John Okello katokea na wapi kafia na kwanini alijitanganzi kuwa yeye ndio jemedari wa mapinduzi ya zanzibar

Unajua watanzania tuna tabia ya kubwabwaja mambo bila ya kufanya utafiti, humu katika JF wana jamvi watatoa stori na hisia tafauti bila hata ya kufanya utafiti kuhusu hilo jambo..

Soma hicho kitabu utafaidika sana mkuu,just download hiyo PDF files,enjow the show wangu...
Chabuso,
Nakushukuru kwa kuwaomba wanaotaka kujua historia ya Zanzibar wasome
kitabu cha Dr. Harith Ghassany.
Hili ndilo tatizo kubwa la jamii yetu.
Uvivu wa kusoma na kupenda kulizungumza jambo mtu hana ujuzi nalo.

Sasa ikiwa Okello ndiyo kiongozi aliyepanga mapinduzi, Abdullah Kassim
Hanga 
nini ulikuwa mchango wake katika mapinduzi hayo?

Ali Mwinyi Tambwe nini ulikuwa mchango wake?

Oscar Kambona, Victor Mkello, Aboud Mmasai na wengine ambao hawatajwi
katika historia rasmi?

Nini mchango wa wale Wayahudi wawili?

Nini mchango wa wale vijana wa Ki-Dar es Salaam ambao hadi leo hawataki
kuhusishwa na mapinduzi kwa kujutia mauaji yaliyofanyika?

Katika hawa mmoja wao ndiyo aliyomhifadhi Karume nyumbani kwake
Dar es Salaam usiku wa mapinduzi na mwingine ndiye alikuwa ''rafiki''
wa wale Mayahudi.

Nini mchango wa Kambi za Kipumbwi na Sakura Tanga?
Nini mchango wa Kimche, Misha?

Au hajasikia majina haya katika historia ya mapinduzi?
Nini mchango wa Mohamed Omari Mkwawa?

Karume alimpa jina la kupanga, ''Tindo."
Kazi ya tindo ni kuvunja mawe.

Kwa kazi ipi hata Karume akampa jina hilo?
Soma kijana soma ndipo ufungue mdomo.

Au hajasikia jina hili pia?
Nini mchango wa Victor Mkello?

Au hawajui kwa kuwa mwaka jana zilipotoka medali za
mapinduzi hawa majina yao hayakuwapo?

Yes... let them enjoy the show...
Let the show begin...

 http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-historia/828-mchango-wa-john-okello-%5Bche-guevara-wa-east-africa%5D-umefutwaje-22.html#post11635949

Abeid Amani Karume na Wanamapinduzi
Edit / Delete




No comments: