Thursday, 29 January 2015

KUTOKA JF: INAULIZWA BAKWATA INAMWAKILISHA NANI?


#301   Report Post    
Mohamed Said's Avatar
JF Senior Expert MemberArray
Join Date : 2nd November 2008
Posts : 5,979
Rep Power : 339909




Likes Received
4769




Likes Given
248

Default Re: Muswada wa Mahakama ya Kadhi kutikisa Bunge

Quote By mogi View Post
Bakwata ni chombo cha nani na kinawaongoza kina nani
Mogi,
Historia ya BAKWATA inaanza mara tu uhuru ulipopatikana.

Mwaka wa 1962 Waislam wa Tanganyika walifanya Muslim Congress
chini ya uongozi wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir kwa mwamvuli
wa iliyokuwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS).

Mkutano ule uliazimia kuwa kwa kuwa uhuru ushapatikana vikwazo
vya ukoloni dhidi ya Waislam na Uislam havipo kwa hiyo sasa wakati
umefika kwa Waislam kuweka mikakati ya maendeleo na msukumo
uwe ni katika elimu.

Waislam walianza kujenga shule na wakaja na mpango wa kujenga
Chuo Kikuu.

Kanisa lilipata hofu na mwamko huu.

Kanisa liliona nguvu ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kanisa likaingia hofu.

Njama zikapangwa za kuhujumu EAMWS.
(Njama hizi Padri John Sivalon pia kazieleza katika kitabu chake
"Kanisa Katoliki...'')

Njama hizi zikafanikiwa na serikali ikapiga marufuku EAMWS na
ikawaundia Waislam BAKWATA mwaka 1968.

Waislam wameikataa BAKWATA toka ilipoasisiwa hadi hii leo.

Ndiyo maana unasikia Waislam tunasema, ''Sheikh wa BAKWATA,''
''Mufti wa BAKWATA,'' nk. nk...

Hii ni kutofautisha kati ya Waislam na BAKWATA.
Ikiwa unapenda kujua historia nzima ya mkasa huu soma kitabu
changu:

"Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) Historia
Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa
Waingereza Katika Tanganyika,'' Phoenix Publishers, Nairobi 2002.

Ukipenda ingia hapa: 

BAKWATA KIBARAKA KIPINDI MAALUM KILICHORUSHWA NA RADIO KHERI, RADIO QUIBLATAIN NA RADIO IMAAN 1 OKTOBA 2012 - Mohamed Said

Sikiliza kipindi hiki nikieleza historia ya BAKWATA na kama unavyooma
kilirushwa na stesheni tatu za Kiislam na kilikuwa mubashara yaani live.
Last edited by Mohamed Said; Today at 14:22.

No comments: