''Serikali
ya Tanzania mwaka wa 1993 ilitiliana sahihi mkataba na makanisa, mkataba
uliokuja kujulikana kama Memorandum of Understanding makubaliano ambayo
yalikuwa serikali kuidhinisha elimu, huduma za jamii na afya ziendeshwe na
Christian Council of Tanzania (CCT) and Tanzania Episcopal Conference (TEC) kwa
kushirikiana na serikali. Mkataba huu ulitayarishwa kwa siri na Dr. Costa Mahalu, wa Kitivo cha Sheria
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na ukatiwa sahihi na Waziri wa Nchi katika Ofisi
ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa. Mkataba huu ulitiwa sahihi bila ya
kuwashirikisha au kuwafahamisha Waislam.
Ili makubaliano haya yaweze kutekelezeka, serikali ilibidi ifanye
marekebisho kifungu 30 cha Education Act
No. 25, 1978.''
Hebu tufikiri hata kwa nusu sekunde kama haya yangelifanywa na Waislam, wamekaa kwa siri wakatengeneza mkataba baina yao na serikali na kutoa fedha kwenye hazina ya umma kwenda kwenye taasisi za Kiislam...hali ingelikuwaje...
No comments:
Post a Comment