SibonikeHujafikia makamu ya kufanya mnakasha na mimi. Toka mwanzo nilijua hutofika mbali.
Katika yote niliyokuwekea hapo mchango wako ndiyo huo? Basi nimekuwia radhi.
Ilitakiwa ujipime kwanza kabla.
Hiyo paper, "Tanzania a Country Without Heroes," niliitoa Nairobi
kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi za
Afrika ya Mashariki.
Watayarishaji walikuwa IFRA French Institute for Research in Africa /BIEA British Institute in East Africa.
Hawa jamaa ndiyo walionialika na kutoka Tanzania nilikuwa peke yangu.
Hili peke yake ingekujulisha moto wa maji unayotaka kuoga.
Pili paper yangu aliyepiga "critique," ni profesa. Sasa wewe hapa unaingiaje?
Hata ujanja huo huna?
Sibonike,Semina niliyotoa paper, "Tanzania: A Nation Without Heroes," ilihudhuriwa na hao hapo juu.
Je wewe unaweza kusogezewa kiti hapo ukakaa?
Unasema kuna shule zilitaifishwa ili Waislam wasome...
Msikilize
Mzee Kitwana Kondo aliyozungumza Bungeni mwaka 1999:
"Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu. Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga. Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha. Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini."
No comments:
Post a Comment