![]() |
| Sheikh Abdulkadir bin Sheikh Mohamed Ramiyya Sheikh wa BAKWATA wa Wilaya ya Bagamoyo na Khalifa wa Tariqa Kadiriyya |
Filamu ya Masheikh wa Bagamoyo ilikuwa ishafikia mwisho na wao kama jeshi lilikuwa lishateka nchi na sasa linaondoka likielekea kunakozama jua baada ya kuangamiza adui.
Hii ndiyo ilikuwa staili ya Hollywood kumaliza senema na baada ya mbabe kuelekea machweo ya jua ndipo inatokea ile "The End."
Enzi hizo mimi kijana mdogo niko Empire Cinema macho nimekodoa kwenye, "screen." Senema zetu zilikuwa za mchana siku ya Jumamosi na Jumapili.
Nakumbuka kwa masikitiko makubwa starehe niliyokuwa napata mwisho wa senema kumuona mbabe anondoka juu ya farasi wake kwa ushindi.
John Wayne au Clint Eastwood...

Hii senema ya Masheikh wa Bagamoyo ilikuwa kama vile wameshinda na ni wababe wanaondoka Dodoma kwa ushindi wanatokomea machweo ya jua la Maghrib, lile jua la rangi ya udhurungi.
Haikuwa.
Ghafla mlio wa risasi unasikika.
Kamanda aliyekuwa katangulia na jeshi lake linamfuata nyuma kuelekea machweo ya jua kapigwa risasi ya kichwa kaanguka.
Kinachofatia ni taharuki ya askari wake waliokuwa wanamfuata nyuma.
Risasi nyingine zinaanza kuvuma kila upande jeshi linashambuliwa na askari mmoja baada ya mwingine wanapigwa risasi mfululizo na kuanguka huku wakitoa vumbi kubwa.
Tahamaki jeshi zima limemalizwa.
Hapo ndipo senema inakwisha na ile "The End," inatokea...

Khalifa wa Qadiriyya Sheikh Abdulkadir Ramiyya anazungumza na waandishi wa habari na kuwapa taarifa ya BAKWATA kuwa hawatambui masheikh waliokwenda Dodoma kuonana na Lowassa...
Khalifa kapiga, "ambush."
Watazamaji senema wanapoondoka kuelekea majumbani wanalaumu wanasema, "Mbona hii senama imemalizika vibaya.
"Mimi sipendi mbabe anakufa," mmoja wa waliotazama senema analalamika.
Mimi najiuliza imekuwaje hii "script," imefanywa hivi?
Huyu Muongozaji Filamu anataka kutoa ujumbe gani?
Najisemea kirohoroho.
"Hapendi senema zenye kumalizika kwa furaha?" Jamaa mmoja anasema kwa mshangao.
"Huyu "director," mimi namjua senema zake zote yeye ni "tradegedies," tu. Hapendi kufurahisha watazamaji. Mara kazamisha meli, mara mchumba wake mbabe kanywa sumu, kagongwa na nyoka kafa ili muradi ni "director," mtata sana huyu..."
Kwani nani huyu - Oliver Stone au Spielberg?
Mtu mwingine anauliza.
Bla bla bla bla bla bla...

| Sheikh Abdulkadir Ramiyya Akiongea na Mtangazaji Octaviana wa Azam TV Leo 22 Machi 2015 Kuhusu Masheikh wa Bagamoyo Waliokwenda Dodoma kwa Lowassa |

.jpg)
No comments:
Post a Comment