Monday, 23 March 2015

JF PANAFUKA MOSHI KISA KIMEFANYIKA KISOMO IKULU

Re: Kisomo Ikulu Dar es salaam

Quote By Bulesi View Post
Huyo mpangaji wa Ikulu mbona matambiko yake yote anafanyia Bagamoyo sasa kwanini anajisi IKULU yetu kwa hicho kisomo na harusi za nduguze? Hiyo ni dalili tosha ya kiongozi asiyejari maadili ya kazi yake sawa na yule marehemu aliyegeuza ofisi za hazina kuwa msikiti wake akidhani angekuwa pale milele!!
Wanamajils,
Laiti historia ya uasisi wa African Association 1929 uasisi wa TANU
1954 na kupigania uhuru wa Tanganyika ingeliandikwa kwa usahihi
wake unaostahili leo asingelitokea mtu akakejeli "visomo."

Kwani "kisomo," ni nini?
Kisomo ni dua.

Dua nayo ni kitu gani?
Dua ni maombi kwa Allah.

Kisomo au dua katika historia ya uhuru wa Tanganyika ina nafasi ya
pekee katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mikutano yote ya TANU pale Mnazi Mmoja ilikuwa ikianza kwa dua.

Vikao vyote vya TANU pale New Street katika miaka ya mwanzo ya TANU
ilikuwa inaanza kwa dua.

Katika mikutano ya Mnazi Mmoja wakati wa kudai uhuru kabla Nyerere
hajapanda jukwaani alikuwa anatanguliwa na Sheikh Suleiman Takadir
na alisoma "Surat, Fatha," yote huku wananchi wamesimama wima na
mikono yao wamenyanyua na mwisho kwa umoja wataitikia, "Amin."

Nyerere alikuwa akienda madrasa ya Mufti Sheikh Hassan bin AmirMtaa wa Amani akiongozana na Abdulwahid Sykes na Dossa Aziz
kwa ajili ya hili au lile katika harakati za kupambana na Waingereza.

Hawataondoka pale ila Sheikh Hassan bin Amir atanyanyua mikono na
kuomba dua.

Hii ndiyo historia ya Tanganyika ambayo leo haitakiwi na inakejeliwa.
Kejeli na kebehi hii inakuja kwa kuwa historia hii imezikwa na viongozi
wetu hawaitaki.

Wametengeneza historia yao iliyofuta haya yote.
Yapo mengi naweza kueleza lakini na tuishie hapa.

Ingia hapa upate habari kamili:  http://www.jamiiforums.com/jamii-photos/770825-kisomo-ikulu-dar-es-salaam.html
Last edited by Mohamed Said; Today at 06:42.

No comments: