Re: Sheikh wa Wilaya Bagamoyo amkana Lowassa
Emma na Wanamajlis,
Katika mashujaa wangu niliokuwa nikiwahusudu sana wakati mimi mdogo
ni Muhammad Ali wakati ule 1964 akijulikana kama Cassius Clay.
Baba yangu akifanya kazi posta na alikuwa akijua ni vipi nampenda Clay.
Yupo kazini mara tu alipopata habari kuwa Clay kampiga Liston akanipigia
simu kunifahamisha.
Leo nikiangalia nyuma zama zile huwa sisemi mengi hubakia kushukuru.
Kwa umri ule wa miaka 12 tayari nishakutana na "somo" yake Cassius Clay
Cassius katika "Julius Caesar," ya William Shakespeare.
Leo watoto ukiwauliza kuhusu kitabu hicho watakuuliza, "Kwani baba video
yake hakuna?"
Kusoma vitabu imekuwa adha kwa wanetu wepesi ni kuangalia DVD.
Tuyaache haya turudi kwa Muhammad Ali.
Katika vitabu vyangu nivipendavyo (nami ni mpenzi wa "biographies,") kimoja
ni "The Greatest My Own Story," alichoandika Ali kuhusu maisha yake.
Katika kitabu hiki kuna sura naipenda sana.
Ali anaeleza pigano lake na George Foreman mwaka 1974, Kinshasa, Zaire.
Ali anaeleza kuwa mchuaji wake (mtu wa massage) alikuwa mzee mmoja
kutoka Cuba.
Wakati wako kambini kwa matayarisho ya pigano lile yule mzee wa Kicuba akampa changamoto Ali akamwambia, "Ali usijisifu kwa kumpiga Sony Liston. Liston alipokutana na wewe umri wake ulikuwa ushapea mtu yoyote angempiga. Ikiwa wewe kweli unataka kuudhihirishia ulimwengu kweli wewe ni, "The Greatest," basi mpige Foreman. Huyu ni simba ana nyama ndani ya tundu lake. Ingia ndaniya tundu uichukue hiyo nyama."
Wakati ule Foreman ndiye alikuwa na mkanda wa dunia na kila mpinzani
alikuwa hakatizi mzunguko wa tatu tayari anakuwa keshawekwa chini yu
taabani janga lilomkuta Joe Frazier kutoka kwa Foreman dunia nzima ilishuhudia.
Ali aliingia katika tundu la simba na akatoka na nyama.
Alimpiga Foreman katika mzunguko wa saba na akawa bingwa wa dunia
kwa mara ya pili.
Hiki kisa nakileta kwa kuangalia hali ya mbio za urais katika CCM.
Picha inayojitokeza ni kwa wananchi kwenda kwa EL nyumbani kwake
Dodoma kumshawishi na kumuomba agombee urais na wao watampa kura
zao.
Katika "hope fulls," tuliokuwanao katika CCM hakuna ambae aliyeweza
kuonyesha kupendwa kama anavyopendwa EL.Natamani kuweka "inverted commas," lakini naogopa kuwaudhi wapenzi wa
LE naona nende hivi hivi juu - kwa juu.
(Katika raha mojawapo ya Majlis hii ni kuwa vijana wanakufunza msamiati
mpya wa kueleweka haraka - "juu kwa juu," maana yake haifati sheria yaani
"deviation from the norm").
Kwa hizi kampeni za wananchi kutoka kila pembe kwenda Dodoma nyumbani
kwake LE kumshawishi hakuna mpinzani wake hata mmoja aliyekanyaga
ardhi hiyo hata kwa pembeni yake.
LE kawaacha wenzake kwa mbali sana.
Hata hivyo kuna mengi yanayosemwa.
LE keshakuwa simba na ana nyama ndani ya tundu lake.
Shujaa gani katika CCM atakuwa na ujasiri wa kuingia katika tundu lile kuichukua
nyama ile?
Hakika ni wazi kuwa atakaeweza kupanda ulingoni na LE na kumshinda kwenye
ulingo njia kwake itakuwa nyeupe ndani ya CCM kupeperusha bendera ya kijani.
Lakini naogopa hata kuliwaza hili kwani naamini damu itakuwa nyingi sakafuni
hiyo siku ya pambano.
Sasa naona nimalize kwa kurejea tena kwa Cassius katika "Julius Caesar."
Caesar kamtazama sana Cassius kisha akasema maneno haya:
"Yond Cassius has a lean and hungry look.He thinks too much. Such men are dangerous."
Hapana sipigi, "alarm bell."
Ni wapi unaweza kumfananisha LE na Cassius na ni nani wakati utakapofika atasema:
"Et Tu Brute..."
Hiki ni kitendawili ambacho muda pekee ndiyo utaweza kukitegua.Last edited by Mohamed Said; Today at 17:54.
Tuesday, 24 March 2015
KUTOKA JF: EL, MUHAMMAD ALI NA ADHA YA UBINGWA
Re: Sheikh wa Wilaya Bagamoyo amkana Lowassa
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment