Monday, 4 May 2015

KUTOKA JF: ATHMAN KASSANDA AMJIBU TARANGIRE KWA KUTUZAWADIA PICHA YA MAREHEMU MAMA YAKE








  1. Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
    Huu mzunguko hauchoki.. si utani.
    Mzee Mwanakijiji,
    Hakika huu mzunguko unachukua kasi kubwa kila kukicha.

    Watoto na wajukuu wa wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika sasa
    wanatafakhar na historia ya wazee wao.

    Jana hapa Majlis kuna mtu anaitwa Tarangire yeye aliwakebehi hawa wazalendo.

    Nilimuonya nikamwambia toka majuzi watu wengi wanaingia humu kumsoma
    Ali Msham na tawi la Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa 1954 na wengine ni watoto
    na wajukuu wa hawa wazalendo.

    Nikamtahadharisha kuwa watu hawa watafadhaika sana ikiwa watakusoma wewe
    unawatukania wazee wao bila kosa lolote.

    Ikiwa kosa lipo basi ni kwa wazee wao kuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa
    nchi yetu.

    Asubuhi hii nimeletewa picha hiyo hapo chini na rafiki yangu Athman Kassanda na
    kanisahihisha jina la marehemu mama yake kuwa siyo Khadija biti Said bali ni
    Khadija biti Jaffar:



    Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi la Magomeni
    Mapipa) na wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar (mama yake Athman Kassanda) wa
    tano Bi. Mtendwa biti Iddi Sudi, wa sita biti Feruzi wa saba Mama Tindwa

    waliokaa wa kwanza ni Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na wa tatu ni Bi. Titi
    Mohamed na pembeni ni mwanae.

    Nimeelezwa kuwa hao ndiyo walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU katika
    tawi hilo na hapa walimkaribisha Bi. Titi na Mzee Mwinjuma Mwinyikamb waje 
    tawini wafahamiane.

No comments: