Thursday, 7 May 2015

KUTOKA JF: "UDINI" KATIKA KITABU CHA MOHAMED SAID "THE LIFE AND TIMES OF ABDULWAHID SYKES (1924 - 1968) THE UNTOLD STORY OF THE MUSLIM STRUGGLE AGAINST BRITISH COLONIALISM IN TANGANYIKA




  1. Mohammed Said,
    Mimi nakukubali sana katika maelezo yako wala sii kwamba hakuna ukweli wowote isipokuwa Historia ya Nchi huandikwa WATU walohusika na kwa minajiri gani. Kama ni UHURU wa Tanganyika kina AbdulWahid hawakuutaka UHURU wa Waislaam wa Tanganyika isipokuwa UHURU wa WATU wote wa Tanganyika haikubagua dini wala Kabila. Kwa hiyo unapoandika kuhusu wazazi wako ungewataja tu majina yao na michango yao, basi kitabu chako kingepata sifa kubwa sana nchini pengine hata kusomwa mashuleni.

    Kosa ullifanya ni kupeleka Udini zaidi ya kuonyesha michango yao isipokuwa mchango wa Uislaam katika Uhuru wa Tanganyika kiasi kwamba ukawaweka hata watu walopingana na TANU juu ya Uhuru wa Tanganyika kina Takadir na AMNUT kuwa katika mashujaa walosahaulika. Kama kweli kweli waislaam walitaka Uhuru wao basi wangekiunga chama hiki cha AMNUT mkono badala ya TANU kilichochanganyikana na watu wa makabila mbali mbali.

    Kwa nini unapenda sana kumshusha Nyerere pamoja ya yote alotutumikia? kwa sababu Mkristu au kwa sababu wazee wako hawakupewa nafasi. Mzee Ali Sykes hadi anatutoka alikataa siasa kabisa yeye mwenyewe na historia inatuonyesha wazee wengi waliacha siasa baada ya kutimiza wajibu wao wakafanya biashara zao.

    Wewe ni mwandishi mzuri sana na unajua kuzitafuta habari lakini unakumbwa na hili jinamizi la Udini ambalo kama nilivyokwambia wazungu wanapenda sana kuwasoma watu kama wewe kwa sababu wanajua upeo wa fikra zako na utaweza kuwa hatari kiasi gani. Na katika hali kama ya leo ya Ugaidi unaweza kuwepo katika list ya watu wanaotazamwa sana kwa sababu wanaamini watu kama wewe ni hatari na je umeweza vipi kuwalaghai wengine kuwajaza chuki dhidi ya wakristu au watu wengine.

    Haya yalifanyika sana Uingereza wakiwaachia masheikh wakizungumza wazi Trafalgar Square, kumbe wakiwachunguzana kuchukua picha za watu wanaohushulia mara kwa mara mihadhara ile, Ilipoanza tu habari za Ugaidi wakakusanywa hata wasokuwemo na kwa sababu kama hizi usidhani unafanya la maana sana ikiwa ncjhi yako yenyewe kitabu chako kimepigwa marufuku. Think big mkuu wangu nakuasa tu.

  2. Pedagogic at Heart
  3. #233   Report Post    
    Mohamed Said's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 2nd November 2008
    Posts : 6,677
    Rep Power : 340063








    Likes Received
    5754








    Likes Given
    275

    Default Re: Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

     
    Mkandara,
    Niwie radhi.
    Hilo "kosa" ni hukumu ya nani?

    Wanahistoria gani waliochambua itabu changu na kukuta kuna makosa?

    Nani kakuambia kuwa kitabu changu hakina "sifa kubwa?"
    Nani kakuambia kuwa niliandika ili kitabu kisomwe shule?

    Hivi unajua kuwa nina kitabu "The Torch on Kilimanjaro" (2007)kimechapwa
    na Oxford Unnversity Press (OUP), Nairobi kwa ajili ya shule za Tanzania.

    Hivi unajua nini kimetokea kuhusu kitabu hiki?
    Kimepigwa "conspiracy of silence."

    Usinambie kuwa OUP wanachapa kitabu ndani kina udini.
    Hakisomeshwi shle za Tanzania lakini kinasomeshwa Kenya na Uganda.



    Nani kakuambia kama kitabu cha Abdul Sykes kina udini?
    Unaweza kuonyesha huo udini ulipo?

    Unataka niamini kuwa walopotosha historia ya TANU walikuwa
    wanaongozwa na udini wao?

    Wapi nimemshusha Nyerere.
    Nionyeshe kwenye kitabu changu mahali nilipomshusha.

    Nami nakuahidi In Sha Allah nitarejea hapa Majlis kukupa jibu.

    Nani alikwambia wazee wangu walitoa mali na nguvu zao katika
    TANU ili wapewe nafasi?

    Unajua utajiri alokuwanao Dossa Aziz?
    Mdini nani?

    Umemsoma Bergen (1981) na Sivalon (1992)?
    Unajua kwa nini kitabu cha Njozi (2002) kilipigwa marufuku?

    Hawa ndiyo waloeleza nani mdini.
    Panapofanyika mazungumzo si Trafalgar Square bali ni Hyde Park.

    Mimi sina taarifa kuwa kitabu changu kimepigwa marufuku.
    Nenda Tanzania Publishing House (TPH) kipo pale kinauzwa.

    Unaniasa mimi.
    Unaniasa kwa lipi?

    Hivi unajua Taifa lilipoamua kutoa medali kwa Abdul Sykes na mdogo
    wake Ally baada ya kuwapuuza kwa miaka 50 unajua "text" iliyosomwa
    viwanja vya Ikulu kwenye sherehe ilitoka wapi?

    Acha kujitisha na kuwatisha wengine.
    Nilichoandika ndiyo ukweli wenyewe.

    Kama kuna msomi yeyote anaona mimi nimesema uongo na aandike
    kitabu chake aeleze ukweli.

    Mimi nimeandika baada ya kusoma historia ya TANU iliyoandikwa na
    Chuo Cha Kivukini.

    Historia ile imepotoshwa pakubwa na kukosewa mwisho wa kukosewa ndipo
    nikaandika hii historia kama nilivyokuwa nikiwasikia wazee wakihadithia.
    Last edited by Mohamed Said; Today at 17:19.

  1. Mkandara,
    Niwie radhi.
    Hilo "kosa" ni hukumu ya nani?

    Wanahistoria gani waliochambua kitabu changu na kukuta kuna makosa?

    Nani kakuambia kuwa kitabu changu hakina "sifa kubwa?"
    Nani kakuambia kuwa niliandika ili kitabu kisomwe shule?

    Hivi unajua kuwa nina kitabu "The Torch on Kilimanjaro" (2007) kimechapwa
    na Oxford Unnversity Press (OUP), Nairobi kwa ajili ya shule za Tanzania.

    Hivi unajua nini kimetokea kuhusu kitabu hiki?
    Kimepigwa "conspiracy of silence."

    Usinambie kuwa OUP wanachapa kitabu ndani kina udini.
    Hakisomeshwi shule za Tanzania lakini kinasomeshwa Kenya na Uganda.



    Nani kakuambia kama kitabu cha Abdul Sykes kina udini?
    Unaweza kuonyesha huo udini ulipo?

    Unataka niamini kuwa walopotosha historia ya TANU walikuwa
    wanaongozwa na udini wao?

    Wapi nimemshusha Nyerere.
    Nionyeshe kwenye kitabu changu mahali nilipomshusha.

    Nami nakuahidi In Sha Allah nitarejea hapa Majlis kukupa jibu.

    Nani alikwambia wazee wangu walitoa mali na nguvu zao katika
    TANU ili wapewe nafasi?

    Unajua utajiri alokuwanao Dossa Aziz?
    Mdini nani?

    Umemsoma Bergen (1981) na Sivalon (1992)?
    Unajua kwa nini kitabu cha Njozi (2002) kilipigwa marufuku?

    Hawa ndiyo waloeleza nani mdini.
    Panapofanyika mazungumzo si Trafalgar Square bali ni Hyde Park.

    Mimi sina taarifa kuwa kitabu changu kimepigwa marufuku.
    Nenda Tanzania Publishing House (TPH) kipo pale kinauzwa.

    Unaniasa mimi.
    Unaniasa kwa lipi?

    Hivi unajua Taifa lilipoamua kutoa medali kwa Abdul Sykes na mdogo
    wake Ally baada ya kuwapuuza kwa miaka 50 unajua "text" iliyosomwa
    viwanja vya Ikulu kwenye sherehe ilitoka wapi?

    Acha kujitisha na kuwatisha wengine.
    Nilichoandika ndiyo ukweli wenyewe.

    Kama kuna msomi yeyote anaona mimi nimesema uongo na aandike
    kitabu chake aeleze ukweli.

    Mimi nimeandika baada ya kusoma historia ya TANU iliyoandikwa na
    Chuo Cha Kivukini.

    Historia ile imepotoshwa pakubwa na kukosewa mwisho wa kukosewa ndipo
    nikaandika hii historia kama nilivyokuwa nikiwasikia wazee wakihadithia.

    ''The Torch on Kilimanjaro''


    ''The Torch on Kilimanjaro'' Kitabu Kilichofitiniwa Kisiingizwe Katika Mtaala wa Shule za Msingi za Tanzania


    Aliyesimama juu ya boneti ya Land Rover akihutubia wananchi ni Mwalimu Nyerere
    na picha ya pembeni ni Nyerere na Kenyatta.




    Mwandishi akitoa maelezo kuhusu kitabu
    The Torch on Kilimanjaro


    Mohamed Seif Khatib katika Uzinduzi wa Kitabu, ''The Torch on Kilimanjaro''
    Kilimanjaro Kempinski Hotel kulia kwake ni Sheikh Abdillah Nassir 



    Mwalimu akikiangalia kitabu










    ''The Torch on Kilimanjaro,'' ni kitabu kilichochapwa na Oxford University Press (OUP) Nairobi.

    Kitabu hiki kilikuwa katika mradi wa kuchapa vitabu kwa ajili ya shule za msingi madhumuni yakiwa ni kumsomesha mwanafunzi lugha ya Kiingereza na wakati huo huo ajifunze na historia ya nchi yake ili kujenga uzalendo.

    Waandishi kutoka Afrika ya Mashariki waliandika vitabu kiasi ya 15 isipokuwa Tanzania.

    OUP walimfuata mwandishi na kumuomba aandike kitabu kimoja ili angalu Tanzania na wao wawemo katika orodha ya nchi zilizoshiriki katika mradi ule wa kusomesha lugha ya Kiingereza Afrika ya Mashariki.

    Mwandishi akapeleka mswada Nairobi.
    Baada ya muda alikwenda Nairobi kuonana na mhariri ili kurekebisha mswada.

    Mhariri akasafiri hadi Dar es Salaam baada ya kupata marekebisho na kazi ikakamilika.
    Kitabu kikachapwa.

    OUP wakafanya dhifa kubwa sana ya kukizindua kitabu  Kilimanjaro Kempinski Hotel ambako wakuu wa Wizara ya Elimu walikaribishwa pamoja na vyombo vya habari.

    Mgeni wa heshima alikuwa Mohamed Seif Khatib.

    Waalikwa wote walipewa nakala moja ya kitabu na mwandishi alikieleza kitabu mbele ya hadhira ile.


    Kwa upande wao OUP walikisifia kitabu kile kuwa kitachangia katika watoto wa shule za msingi kujifunza Kiingereza na historia ya nchi yao hususan historia ya Mwalimu Nyerere alipoanza kudai uhuru wa Tanganyika mwaka 1954 hadi uhuru ulipopatikana mwaka 1961.

    Aliposhuka tu kutoka kwenye jukwaa watu wa televisheni na magazeti wakamzunguka kumhoji kuhusu kitabu kile.

    Tanzania kitu chochote kinachomuhusu Nyerere kinauzika.

    Mwandishi na mchapaji OUP walitegemea makubwa kutoka kitabu kile.
    Haikuwa hivyo.

    Kitabu hiki kimepigwa chenga kuanzia mwaka 2007 licha ya juhudi nyingi za OUP kuwaandikia Wizara ya Elimu kuwaomba wakiingize katika mtaala wa kusomesha lugha ya Kiingereza.

    OUP walimweleza mwandishi kuwa wao hawajui kwa nini kitabu hiki chenye historia ya Mwalimu Nyerere hakitakiwi wakati kule Kenya kitabu cha Jomo Kenyatta 
    ''The Kapenguria Six''    kilicho katika mradi huu kipo katika mtaala wa shule za msingi na kinasomeshwa.




    The Kapenguria Six

    Muswada mpya 'The School Trip'' ambao mwandishi aliwapa OUP na wakaupokea kwa ajili ya uchapaji baada ya kuona uzuri wa kitabu kile cha kwanza, OUP wameghairi kukichapa kitabu na maelezo ni kuwa mwandishi hauziki nchini kwake lau kama ana kipaji cha uandishi wa hadithi za watoto.

    Hata hivyo OUP walimshirikisha mwandishi katika mradi mwingine kwa ajili ya vitabu Afrika ''The Mermaid of Msambweni and Other Stories'' (2007) kitabu cha mkusanyiko wa waandishi kutoka nchi tofauti za Afrika Tanzania ikiwakilishwa na mwandishi huyu.

    OUP wala hawakushughulika kukitangaza kitabu hiki hapa Tanzania.
    Ndiyo maana husikika minong'ono kuwa kuna kitu katika uendeshaji wa serikali kinaitwa ''Mfumokristo.'' 

    Huu mfumo inasemekana una watu wake unaowapenda na kuwatumikia.
    Je, Wizara ya Elimu ni moja ya taasisi zinazoongozwa na ''Mfumokristo?''




No comments: