Toleo la Pili (2015)
Kitabu hiki kilikuwa katika mradi wa kuchapa vitabu kwa ajili ya shule za msingi madhumuni yakiwa ni kumsomesha mwanafunzi lugha ya Kiingereza na wakati huo huo ajifunze na historia ya nchi yake ili kujenga uzalendo. Waandishi kutoka Afrika ya Mashariki waliandika vitabu kiasi ya 15 isipokuwa Tanzania. Oxford University Press (OUP) walimfuata mwandishi na kumuomba aandike kitabu kimoja ili angalu Tanzania na wao wawemo katika orodha ya nchi zilizoshiriki katika mradi ule wa kusomesha lugha ya Kiingereza Afrika ya Mashariki. Kitabu hiki kwa bahati mbaya hakijakubaliwa kutiwa kwenye mtaala wa Tanzania ingawa kinasomeshwa katika shule za Kenya na Uganda.
|
No comments:
Post a Comment