Sunday, 29 November 2015

KUTOKA JAMIIFORUMS: MATATIZO YA UCHAGUZI WA ZANZIBAR





  1.  Re: Kiini cha matatizo ya Zanzibar, Mapinduzi ya mwaka yaliyomwondoa Sultani

    Quote By ngozimbili View Post
    divide and conquer,ndio sera iliyofeli zanzibar,hakuna kabila la wapemba wala waunguja,pemba na unguja ni visiwa vyenye watu wa makabila yote ya zanzibar,lakini mkoloni ni mkoloni tu hawezi kushindwa kuwagawa watu,ndio maana watu wa bara wanachanginyikiwa vp mwanamapinduzi kindakindaki nasoro moyo yupo na maalim seif,mansour himidi mtoto wa brigedia yusuf himidi comrade wa nasoro moyo,yupo na maalim seif,amani karume,fatma karume,eddy riyami,ismail jusa babu duni mtoto wa dadake komandoo salmin amour naweza kuandika kitabu HUO UBAGUZI HIYO HISTORIA IKO WAPI YA KUHALALISHA KUFUTA MAMLAKA YA WANANCHI KUCHAGUA MUSTAKBALI WAO?
    Ngozimbili,
    Napenda kukuunga mkono kuhusu historia ya Zanzibar.

    Wengi hawaijui vyema historia ya Zanzibar pamoja na Mapinduzi ya Zanzibar.

    Kutoijua historia ya Zanzibar kunakwenda hata kwa viongozi wetu wa juu na
    ndiyo maana utasikia wanasema maneno ambayo huwashangaza Wazanzibari
    wenyewe na kujiuliza kama kweli hawa viongozi wanaizungumza Zanzibar au
    nchi nyingine.

    Naweka hapa chini barua aliyoniletea rafiki yangu mmoja Mzanzibari akieleza
    hali ya Zanzibar ilivyo:

    ''Hawa wenye siasa kali za kigozi (kibaguzi) za kuwaangalia watu kwa rangi
    zao na asili zao hapana shaka hawawajui Wazanzibari walivyo.

    Sielewi mtu anazungumza nini anapotaja "Black Africans" yaani "Waafrika
    Weusi" kukhusiana na Zanzibar!

    Bora nitoe mifano michache asaa wakatuelewa Wazanzibari tulivyo.

    Nadhani kwa hawa magozi, mtu kama hayati Mhishimiwa Abedi Amani
    Karume 
    ni mfano mzuri kwao wa "Black African" kwani alitoka bara na kuja
    Zanzibar.

    Lakini, ikisha baada ya hapo alifanya nini ili watoto wake wabakie kuwa
    "Waafrika Weusi?"

    Jawabu ni kuwa: alimwoa mwanamke wa Kizanzibari ambaye kwa aliye gozi
    hatamkubali Bi. Fatma kuwa ni "Mwafrika Mweusi" mwenziwe, kwani rangi
    yake Bi. Fatma si ya "Mwafrika Mweusi" kwa mujibu wa fikra za aliye gozi.

    Tusisite hapo; tuje kwa wanawe Wahishimiwa Amani na Ali Karume.
    Wote wawili wamewaoa Wazanzibari wenzao lakini wenye asili za Kiarabu.

    Tusisite hapo, tuje sasa kwa wajukuu wa hayati Mhishimiwa Abedi Karume,
    utakuta mpaka Mzungu ameolewa nao.

    Tusisite hapo, sasa angalia wake wa wahishimiwa wengi pia.

    Mfano mzurini wa hayati Brigadier Yusuf Himid ambaye alimwoa Bi. Fatma
    Jinja
     ambaye ni Mwarabu aliyechanganya nasaba; huyu ni mama yake mzazi
    Mhishimiwa Mansour Yussuf Himid.

    Aliwaoa pia na wanawake wengine wenye asili za Kiarabu.

    Tusisite hapo; tuje sasa kwa aila ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha
    Afro-Shirazi, hayati Mhishimiwa Thabit Kombo Jecha.

    Naye alimwoa pia Mzanzibari mwenye asili ya Kihindi na kumzaa Mhishimiwa
    Mahmoud Thabit Kombo. 


    Mhishimiwa Mtoro Rehani Kingo, mwenye asili ya bara, ambaye alikuwa
    Mhariri wa gazeti liitwalo Afrika Kwetu (gazeti ambalo lilikuwa sauti ya Chama
    cha Waafrika kukhusu siasa za Zanzibar tokea miaka ya 1950), baadaye alikuwa
    pia Mkuu wa Chama cha Afro-Shirazi, na bada ya hapo akawa Memba wa Braza
    la Mapinduzi (MBM), naye huyu pia alimwoa bibi wa Kiarabu aitwaye Fatma
    Mbarak
    .

    Mhishimiwa Said wa Shoto naye pia alikuwa Memba wa Baraza la Mapinduzi la
    mwanzo, ni Myamwezi kutoka Tanganyika; alikuwa akitisha sana kwa vitendo
    alivyowafanzia Wazanzibari, naye alimwoa mwanamke wa Kiarabu aitwaye
    Saada "Mgeni" Mbarak Al-Alawy. 

    Mhishimiwa Said Ali Bavuai alikuwa pia Memba wa Baraza la Mapinduzi,
    naye pia alimwoa msichana wa Kiarabu aitwaye Fawziya Al-Bahri na kuzaa
    naye.

    Mhishimiwa Ibrahim Makungu aliyekuwa katika jopo la siri la Watu Kumi
    na Nne ("Commeettee of 14") ambalo likiamua uuwawe, basi roho yako haikuwa
    na salama Zanzibar, naye pia alimwoa msichana wa Kihindi aitwaye Katu Lalji
    Punja
     na pia alimwoa Nahida Sarhan, msichana wa Kiarabu.

    Mwingine mwanajopo hili ni Ramadhan Haji ambaye alimwoa msichana wa
    Kiarabu aitwaye Badriya Muhammad Seif.

    Mhishimiwa Ali Muhsin naye pia aliwaoa wasichana wawili wa Kiarabu.

    Dr. Salmin Amour, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, alimwoa Bibi wa Kibaharani
    anayeitwa Rukiya Khalil Mirza Al-Bahrani.

    Kuna na wengine wengi tu waliokuwa wakijinata na Uafrika wao ambao wao
    wenyewe waliwataka wasichana wa Kiarabu, wa Kibaharani na wa Kihindi na
    kwa nguvu za Serikaliya Zanzibar walifungishwa ndoa za haramu na Serikali,
    kwani wengi katika wasichana hao hawakuwa radhi kuolewa kwa mirututu ya
    bunduki na nguvu za Serikali na wazee kufungwa jela na kuadhibiwa wakikataa
    kutoa idhini ya kuwaozesha watoto wao wa kike.

    Lakini pia, ni muhimu kusema kuwa kuna na wengi wengineo waliooana kwa
    khiyari zao na kwa ridhaa za wazazi wao bila ya kulazimishwa na Serikali,
    na haya ndiyo yaliyokuwa ya kidasturi tangu zama za zama.

    Mifano ya waliokuwa wakijinata kwa "Uafrika" wao -- na kumfanya Mwarabu
    ndiye adui wao mkubwa kabisa -- na wakati huohuo kuwaoa wasichana wa
    Kiarabu ni mingi sana.

    Jinsi Mhishimiwa Rais Abedi Amani Karume alivyotafakharia uamuzi wake
    wa kulazimisha ndoa za aina hii, siku moja katika mwezi wa Januari 1968
    aliwaamuru Wahishimiwa wote na wengineo waliofungishwa "ndoa" na
    wasichana wa Kiarabu, Kifursi na Kihindi kufika katikaKarume House ili kupiga
    picha pamoja.

    Kwa hivyo yoyote asiyeijua Zanzibar na watu wake inataka aelewe vizuri nini
    anasema anapozungumzia "Waafrika Weusi" kukhusiana na Zanzibar, kwani
    hata watoto na wajukuu wa Mhishimiwa hayati Abedi Karume atawakuta
    kuwasi "Waafrika Weusi" tena kwa walivyochanganya nasaba.

    Wale leo wanaojinata kwa asili zao za "Uafrika Weusi" au za "Kibantu" au
    zozote nyinginezo na kusema Waarabu na warudi kwao, watuelezee vipi
    tuwakatekate vipande, kwanza, watoto na wajukuu wa hawa wahishimiwa
    ilisehemu za miili yao zilizokuwa za Kiarabu tuzirejeshe Arabuni na sehemu
    zilizokuwa za "Kibantu" tuzipeleke kuzizika Kamerun kwenye chimbuko la
    Wabantu!

    Kuna pia wale wanaojisemea ovyo kuwa "Wafrika Weusi" ndio walio wengi
    Zanzibar.

    Ukweli ni kuwa hakuna msomi anayezijua takwimu za watu wa Zanzibar
    asiyejua kuwa ni Washirazi ambao ndio wenye idadi kubwa kabisa Zanzibar,
    na kama walivyoandika katika barua yao wanachama wa African Association
    tarehe 9 Julai, 1946 kumpelekea Balozi wa Kiingereza, kuwa Washirazi si
    Waafrika ni Waasia.

    Sasa, juu ya idadi ya Washirazi ongeza idadi ya wenye asili za Kiarabu na
    za Kihindi, "Waafrika Weusi" vipi wanakuwa ndio wengi Zanzibar?

    Tafadhalini, tukizungumzia jambo hadharani, kama katika mitandao, tuwe
    tunapaelewa vizuri pahala tunapopazungumzia na tunaelewa vizuri asili za
    watu wake zilivyo.

    Vinginevyo itakuwa tunazungumzia tusiyoyaelewa vyema, tunapasuana vichwa
    na kupotezeana wakati.''

    Wanamajlis,
    Hii ndiyo historia ya Zanzibar na hao ndiyo Wazanzibari ambao ndiyo leo hawa
    wamekuwa kila wakipiga kura kuanzia mwaka 1995 wamekuwa wakiichagua
    CUF lakini kundi dogo la wahafidhina ambao wanadai wao ndiyo wenye haki ya
    kutawala wamekuwa wakitumia nguvu kupora ushindi huo.

    Hivi sasa tuko katika mvutano wa uchaguzi wa 2015.
    CCM Zanzibar wamekataliwa kwa mara nyingine na Wazanzibari.

    CCM imeamua safari hii kufuta uchaguzi na wanataka uchaguzi urudiwe.
    1. Re: Kiini cha matatizo ya Zanzibar, Mapinduzi ya mwaka yaliyomwondoa Sultani

      Quote By masopakyindi View Post
      Mkuu hadithi yako ingeekeweka kama ungeongekea vile vile , yaani wewe na mtu wako huyo aliyekuandikia barua jinsi watu wasio waafrika walivyoingia kisiwa cha waafrika.
      Kusema kuwa waafrika walitoka huko bara na wakahamia Zanzibar, ni kujidanganya na kutoukubali ukweli wa waadrika waliokuwepo hapo kwa karne na karne.

      Siyo siri, ni kasumba inayowamaliza waafrika wa huko unguja na Pemba , kupenda kuoa wale wasio asili yao.
      Wengine hufanya hivyo ili kuonekana kuwa kastaarabika au amekuwa mwungwana.
      Offspings za hao watu ndo wako mbele kuukana uafrika wao na kufanya allegience na asili za mama zao.

      Hili nimeliona, its a weakness and strenrh at the same time!

      Kwa mtu wa matamanio, angeweza kusema pengine baada ya karne Zanzibar itakuwa a mixed race country na hivyo kuondoa chokochoko zote za kisiasa, lakini hata leo si hivyo.
      Masopyakindi,
      Tufanye mjadala wa kistaarabu sote tufaidike mie na wewe na watazamaji.
      Lugha za ''hadithi,'' mnakasha utaharibika kwani kejeli hazijengi.

      Mimi si mpiga hadith.

      Inawezekana kwa hakika kulikuwa na Waafrika katika visiwa hivyo wenyeji
      na pia wakaja wahamiaji Waafrika na Waarabu kwa karne nyingi.

      Historia hii kwa hivi sasa kwa kweli nionavyo mimi haina maana yoyote.
      Zanzibar ya karne ya 18 si Zanzibar ya leo ya karne ya 21.

      Mengi yamebadilika na ndiyo maana rafiki yangu akaniandikia barua hiyo
      niliyoiweka hapo.

      Ndiyo maana leo unaona mahasimu wakubwa wa miaka ya 1950 na kabla ya
      mapinduzi leo wanaoleana bila kinyongo.

      Wala wajukuu hawaelezwi uhasama uliopita kati ya babu zao hadi kufikia
      kuuana.

      Sitaki kutaja majina kwani kufukua makaburi hakujengi.

      Tatizo kubwa linalowakuta watu wa Bara katika muungano ni kudhani kuwa
      wenye haki Zanzibar ni hawa mahafidhina licha ya ukweli kuwa kila wakiingia
      katika uchaguzi Wazanzibari wanawakataa sasa miaka 20.

      Kitu cha kujiuliza hapa ni hii inasabishwa na nini?

      Iweje hao wanaojigamba kuwa ni ''wanamapinduzi,'' leo wanakataliwa na
      Wazanzibari?

No comments: