Monday, 30 November 2015

SHEIKH ISSA PONDA KATIKA PICHA: KUTOKA KIBLA CHA ALLAH HADI GEREZANI SEGEREA NA MOROGORO

''Allah ni Mjuzi Allah na ni Mbora wa kulipa. 
Sheikh Ponda utayakuta malipo yako kwa Allah yakiwa makubwa kwa subra na ustahamilivu kwa ajili ya dini yake. 
Hukuwa tayari kuuza uhuru wako kwa matakwa ya wenye kudhulumu. 
Muda wote ulitutia moyo mawakili wako kila tulipokutana na vitimbi. 
Mara nyingi sisi mawakili tulikuwa kama wateja na wewe ndiye wakili. 
Hakika wewe ni kiongozi. 
Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako. 
Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi. 
Allah anayo siri kubwa katika maisha yako Sheikh Ponda. 
Allah akuhifadhi kiongozi wetu.
Amin.''

Wakili Juma Nassoro



Sheikh Ponda akiwa katika pingu za mikono mahakamani



Sheikh Ponda akiwa huru baada ya kuonekana hana kosa na mahakama Morogoro
(Picha kwa hisani ya www.sehkideleblogspot.com)


Sheikh Ponda chini ya ulinzi
Sheikh Ponda katika hafla ya kusheherekea Eid El Fitr 2006 Viwanja Vya Mnazi Mmoja kushoto kwake ni Sheikh Ali Basaleh

Sheikh Ponda akizungunza na Waislam Msikiti wa Mtambani
Sheikh Ponda mbele ya Kibla cha Msikiti wa Mtambani
Sheikh Ponda kwenye hafla ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani 2013 Mwalimu Nyerere Conference Centre


Sheikh Ponda akielekea Kibla akiomba dua kabla ya kuongoza maandamano ya Waislam kupinga dhulma zilizokuwa zikifanywa na (NECTA) Baraza la Mitihani dhidi ya wanafunzi Waislam


Maandamano ya kuipinga NECTA yaliyoongozwa na Sheikh Ponda yakielekea Kidongo Chekundu




Wakili Juma Nassoro akiwa na Mzee Bilali Rehani Waikela kutokea Tabora aliyekuja kutoa ushahidi
Mahakamani Kisutu kesi ya Sheikh Ponda


Sheikh Ponda akizungumza na mawakili wake kushoto Salim Abubakar na Juma Nassoro

Sheikh Ponda mbele ya Kibla Msikiti wa Mtambani kulia ni Prof. Ibrahim Lipumba


Sheikh Ponda mahakamani Morogoro kulia kwake ni Wakili Juma Nassoro na Wakili Salim Abubakar



Kushoto Mzee Bilal Rehani Waikela, Mwandishi na Mahakamani Morogoro

Sheikh Ponda akizungumza na Wakili Nassoro na Wakili Salim Abubakar

Askari katika msafara wa Sheikh Ponda
Waislam wa Morogoro wakitoka kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda



Sheikh Ponda akiwa mahakamani na walinzi



No comments: