Sheikh Hamzah Rijal |
Risala
yangu kutoka Makka Na Ben Rijal
Asalam Alaykum kwa
wasomaji wanaofwatilia upenyu wangu katika gazeti la An-Nuur. Kwa wiki tano
sikuwa pamoja na nyie kwa kuwa nilikuwa kwenye Ibada ya Hijja huko Makka. Aya
katika Qur’an juu ya Hijja: 2:125, 2:158, 2:189, 2:196, 2:197, 2:198- 201,
2:203, 3:96-97, 5:1-2, 5:94-95, 5:96-97, 9:37, 22:26-27, 22:28-30, 22:33,
22:36, 22:37, 48:27. “Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe
pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani. Na alipo kuwa akisimama Ibrahim
pafanyeni pawe pa kusalia. Na tuliagana na Ibrahim na Ismail: Itakaseni Nyumba
yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu na wanao jitenga huko kwa ibada,
na wanao inama na kusujudu.” (2:125) Wengi wanaporudi Makka huwa na mengi ya
kuelezea juu ya safari yao kikamilifu lakini wengi wao huyaelezea yakesha na
wachache ambao huamua kuandika na maelezo yao yakabakia kuwa kumbukumbu, mfano
Malik Al-Shabaz kwa jina maarufu Malcolm X aliandika barua yake kutoka Makka na
hadi leo barua hio husomwa na wengi na kuvutiwa nayo.
Kuna maneno amayasema katika risala yake hio Al-Hajj Malik Al-Shabaz ambayo hadi hii leo yana uzito “America needs to understand Islam, because this is the one religion that erases from its society the race problem. Throughout my travels in the Muslim world, I have met, talked to, and even eaten with people who in America would have been considered 'white'--but the 'white' attitude was removed from their minds by the religion of Islam. I have never before seen sincere and true brotherhood practiced by all colors together, irrespective of their color.” Tafsiri ya juu juu “Nchi ya Marekani inahitajia kuuelewa Uislamu kwani ni dini ambayo imefuta kabisa ukabila. Nimetemebea kwingi katika nchi za Kiislamu, nimekutana, nimezungumza na hata nimekula na watu ambao kwa nchi ya Marekani wao wangejinasibu ni kama watu weupe, lakini hayo yamefutwa katika nyoyo zao kutokana na dini ya Kiislamu, sijapatapo kuona udugu wa kweli unawekwa na watu wa rangi zote kama hapo kwenye Hijja.” Maneno mazito na yanataka tafakuru, kwa yule mwenye chembe ya ubaguzi katika nafsi yake. Maneno haya kayazungumza miaka 51 iliopita na mpaka leo Marekani ubaguzi wa rangi unanuka. Safari ya Makka ni safari ambayo naweza kusema kuwa imekuwa katika fikra zangu tangu nikiwa na umri wa miaka 7 kwani nilipokuwa skuli tukisomeshwa juu ya nguzo 5 za Uislamu na ya 5 tukisoma “Nakwenda Ku-Hijji Makka kwa mwenye uwezo.”
Mwaka huo bibi yangu mzaa mama naye akenda Hijja na ikawa inanishughulisha kafikaje huko na alifanya nini huko Makka? Nilipofika umri wa miaka 28 ikawa fursa kwangu kwenda Hijja lakini wakati huo nchini Libya walikuwa hawachukui tena wageni kwenda Hijja katika zile meli zake maarufu, Traplus na Benghazi. Nikatafakari lini nitaweza kwenda kuitimiza nguzo hii ya Hijja na siku zinakwenda na zishakwenda hazirudi nyuma. Tunafahamishwa kuwa Hijja uwende kijana na usende ukiwa umri unakupa kisogo, maneno hayo yana nguvu na yana mantiki. Msongamano wakati wa Kutufu na Kussai, kusimama Arafa, kulala Muzadadifa, kupiga mawe Jamaraat hakika inahitajia uwe na nguvu zako usiwe dhaifu lakini vilevile kwenda katika umri wa miaka 50 na kwenda mbele unakuwa ndani ya ucha Mungu kwa zaidi kwani huwa hushughulishwi na chochote kile zaidi ya Ibada. Safari yangu yote ya Hijja ilinichukua siku 21 nikianzia Madina mji ambao Mtume (SAW) alihamia kutoka Makka baada ya kukimbia vitimbi vya makafiri. Mji huu una utulivu na watu wake wakarimu zaidi kuliko watu wa Makka. Nalioondoka nyumbani nakufanya kama tulivyotakiwa kwa kutia nia kuwa nakwenda kutimiza Hijja, kisha nikasali rakaa 2. Rakaa ya mwanzo nikasoma Suratul Kafiruna na rakaa ya pili nikasoma Al-Ikhlas. Baada ya kutoa salamu nikaomba kwa lugha yangu ya Kiswahili kutaka usalama kwa huko niendako. Kisha nikaagana na familia yangu akiwepo dada yangu na shemegi zangu na wahisani katika kuwaaga nikisoma “Astawdiu Llaha dinakum wa amanatakum wakhawatima aamalakum.”
Hapo tena safari ikaanza kwa kuelekea uwanja wa ndege. Nikiagana nawana familia Kuaga kwa safari hii muhimu katika maisha ya Muislamu miaka hii sio kama zamani ambapo waendao Hijja hawakuwa na hata taswira ndogo ya huko Makka kukoje wala hawakuwa na taarifa za undani, kwahio walikuwa wakitoa buriani na kuaga na kuwawacha wanaowawaga na vilio kwa kutokuwa na uhakika wa kurudi, kinyume cha miaka hii tulionayo katika miaka hii hayo hayapo, kwani anaondoka kuelekea Hijja huwa na sura kamili ya Makka na akifika huko huwa mara kwa mara anawasiliana na watu wake. Tulifika uwanja wa ndege saa 6 ya mchana na hapo tukasubiri uingie wakati wa sala na kutanguliza kwa kuzikusanya Sala ya Adhuhuri na Alasiri. Mie ndio nilikuwa Muadhini nikaadhini kisha nikakimu kusali sala ya Adhuri rakaa mbili bada ya salamu nikasimama tena kukimu na kusali sala ya Alasiri rakaa mbili. Ilikuwa muhimu sana viongozi kuwafahamisha Mahujaji watarajiwa kujua kusali sala ya safari na hata hivyo bado ilikuwa kikwazo kwa wengine. Tukaondoka uwanja wa Kisauni-Unguja katika milango ya saa kumi na kufika Madina ikiwa saa tatu za usiku, watu wa Uhamiaji hapo Madina walikuwa wapo tayari kutuhudumia na kutusalimu na huku kututakia Hijja ya amani, unapokutana na Ofisa huyo huchukui zaidi ya dakika tatu au tano. Tulipomaliza hayo tukawa tayari kuelekea Madina kwenye hoteli tuliopangiwa.
Tulifika hoteli saa 7 za usiku tukasali kwa kuchelewesha Magharibi rakaa 3 na Isha rakaa 2 kwenye Msikiti wa Mtume (SAW) na kuamua kukaa itikafu hadi kusali sala ya Alfajiri. Hapo unaukuta Msikiti tayari umeshaanza kujaza watu na unapojisikia unataka kula unakwenda kunywa maji ya Zamzam tena yapo baridi yanasambazwa Msikitini kote na hayakosekani na maji hayo huwa yanatokea Makka raha yangu ilikuwa ni kunywa maji ya Zamzam na mengine kujimwagia na kunawa uso. Msikiti wa Madina ni wenye kuvutia na umefanyiwa ukarabati katika nyakati tafauti kuna sehemu ya kale ambayo ndio ya Rasuli, kuna ile iliofanyiwa ukarabati na Waturuki na kuna sehemu iliofanyiwa ukarabati na Mfalme Fahad. Sehemu iliofanyiwa ukarabati na watawala wa Kituruki ina masafa ya mita ya mraba 16,500m2 (square meter) na kuchukua waumuni 167,000 kwa mara mmoja kisha kuna sehemu ya utanuzi iliofanywa na Mfalme Fahad ikiwa na masafa ya mita ya mraba 82,000m2 (square meter) ina uwezo wa kuchukua waumini 167,000 kwa mara mmoja. Kuna na sehemu ya chini yenye uwezo wa kuchukua waumini 90,000 ikiwa na mita za mraba 67,000 (67,000 meter square). Ina Minara 10 ikiwa 6 mipya na 4 ya kale, Msikiti huu wa Mtume (SAW) una milango 85 ikiwa na vipimo 3x6 meter mlango ambao nikiupita mara nyingi ni Fahd 22 kwani nikipita mlango huo huiona saa kwa nje na hufika hoteli niliofikia chini ya dakika 5. Nguvu za umeme hutokea kilomita 7 nje ya Msikiti na hilo jenereta kazi yake kutoa umeme kwa Msikiti huotu, likiwa linatoa Megawatt 2.5 na kuwa na vituo vidogo 4. Kuna kamera za kuchukua picha saa zote 543 na vipaza sauti vya nyongeza (amplifiers) 206 na kila kimoja kina uwezo wa kutoa 600 Watt na Maspika 3,500.
Hakika ni Msikiti wa kipekee ambao hauwezi kukosa Umeme wakati wowote ule wala kukosa maji kwa wakati wowote ule, haijatokea siku ukakatika umeme na kama hitilafu ikitokea dakika chache utakuwa umerejea. Unapokuwepo Madina kwa siku 8 utatakiwa usali sala 40 zote kwa jamaa katika Msikiti wa Mtume (SAW) nimebahatika kulitekeleza hilo na kila Sala mmoja unaoisali Msikiti huo unapata ujira wa 1,000. Msikiti huu wa Madina ndipo alipozikwa Mtume (SAW) na pembezoni mwake kazikwa Syd Abubakar bin Sidiq na Syd Umar bin Khattab, ilikuwa ada kwangu na wengi wa Mahujaji kuhakikisha kila bada ya Sala kufanya ziara katika kaburi la Mtume (SAW) na kwa wengine walijiekea walaakali yaani kwa uchache hakosi kwa siku kumzuru Mtume (SAW) kiongozi wa Umma walau mara mmoja. Msikiti wa Madina Unapokuwa katika ziara hii ambayo unaifanya ukiwa ndani ya Msikiti wa Mtume (SAW) unapata kila hisia, kwani wenzako ambao nao wanaingia katika sehemu hii ilio ndogo kabisa huku askari kutaka utoe salamu upite uwende zako, unapata msisimko wa kuona wengine wanalia, wengine wanamaliza kusoma dua zote wazijuazo ikiwa unapita mahali hapo huwezi kubakia hata dakika 3 unasoma huku unakwenda na wengine wanafwatia, kila ukiwa unazuru kaburi la Mtume (SAW) unajawa na hisia na kujua mbinu gani utumie upate kusoma dua zako kwa wingi.
Siku nikiwa katika ziara hii alikuwepo mzee kutoka Afrika ya Magharibi alipotoa salamu yake na huku analia hakika sote tulimfwata kwani ilikuwa analia na khushuu ndani yake hata askari aliokuwa akisema ya Hajj imsh alinyamaza kimya na huku tunakwenda na machozi kutulenga kwani unakuwa na hisia za namna yake ambazo sio rahisi kuzielezea kwa kutumia kalamu. Sitowacha aidha kukieleza kisa cha watu 2 mmoja akiwa mtu wa Misri nimemjua kwa lahaja yake na wa pili akiwa kijana kutoka Afrika ya Magharibi, tupo katika uzio tunasubiri tupishwe kwenda kwenye ziara kwani askari huchunga nidhamu ya kupisha watu kwa makundi kwenda kwenye ziara na kwa wakati mmoja hufikia watu 3,000 wanataka kufanya ziara. Huku ikiwa askari akiwa anataka watu wasimame waliopo kwenye uzio Mmisri kaka kitako na askari akimlazimisha kusimama, jawabu ya Hajj huyo ilikuwa “Sikiliza bwana mie nimekuja hapa kwa ibada kwa hio nipo tayari kwa lolote lile ili nitimize ibada.”
Askari aliona sasa haya makubwa akamrukia jamaa wa Afrika ya Magharibi ambaye amesimama lakini analazimisha uzio ufunguliwe, jamaa huyo anacho Kiarabu cha kutupa na kuchanganya lugha ya Kifaransa hataki kabisa kusikia kwanini tunachelewesha kuachiwa kwenda kufanya ziara. Alisema maisha yake yote ameyapanga Ku-Hijji na kumzuru Mtume (SAW) ilivyokua amefika basi ni lazima atimize lengo lake hapendi kuchelewesha. Askari na ubabe wake alifahamu hisia za watu walizokuwa nazo, sio muda akatuachia kuingia kwenye Msikiti ambapo kuna kaburi la Mtume (SAW). Aidha baina ya kaburi la Mtume (SAW) na Mimbari akiitumia kuna eneo linalojulikana kama Rawdha, kusali Rawdha ni sawa na kusali katika viunga vya Peponi. Mmoja alinifahamisha kuwa kuweza kuijuwa Raudha ni sehemu zote zina mazulia mekundu lakini hapa Rawdha mazulia yake ni ya kijani.

Unapotoka kufanya ziara
kwenye Msikiti wa Mtume (SAW) unatoka katika mlango unaoitwa Baqii ukenda moja
kwa moja kama mita 100 unafika katika makaburi ya Baqii ambapo amezikwa Bibi
Fatma mtoto wa Mtume (SAW) na ndugu zake, aidha hapo amezikwa sahaba maarufu
Syd Uthman bin Affan na Masahaba 10,000 aidha Imam Malik naye kazikwa hapo,
unapokuwa na ramani ndio itakusaidia kuelewa baadhi ya sehemu, lakini makaburi
yote hayana chochote kile kilichoandikwa na yote yapo sawa huwezi
kuyatafautisha. Sehemu ya Makaburi ya Baqii Aidha unapokuwa Madina unapata
fursa ya kuzuru maeneo muhimu ya Kihistoria kama Masjid Quba, Masjid Qiblatein,
Baqiii, Milima ya Uhud palipopiganwa vita vya Uhud. Nilibahatika kufika Msikiti
wa Quba Msikiti ambao ndipo alipofika Mtume (SAW) na kuujenga, Msikiti upo wa
kileo, nilifika hapo katika nyakati za Alasiri nikasali sala ya kuamkia
Msikiti, wakiwa waumini wa kike na kiume kila mmoja upande wake akisali hapo.
Msikiti wa Quba Aidha nilisali Masjid Qiblatein mahali ambapo Masahaba walisali
Rakaa 2 wakielekea Baitil Muqadas na rakaa mbili kuelekea Alqaba, unaposali
hapo na kwengineko unapata hisia na kuirejesha nafsi yako kuwakumbuka Masahaba
na kiongozi wao Mtume SAW. Masjid Qiblatein Nilifika Uhud pahali ambapo huko
nyuma niliandika makala juu ya vita vya Uhud. Nilipata msisimko hasa pale
nilipofika sehemu ya wapiga mishare 50 na kupanda mlima huo na kutafakar kwa kiasi.
Sehemu ya Mlima Uhud walipokuwa wapiga mishere walipowekwa Nilifanya ziara hizo
na bada ya kutimu siku 8 ikawa ni safari yakuelekea Makka na ilivyokuwa Hijja
yetu ni ya Tamatuu ilikuwa ni kuanza kwa kufanya Umra. Kabla ya kuondoka Madina
tulipata habari kuanguka kwa krini/Kachorora na kuua na kujeruhi baadhi ya
waumini, ilikuwa simu nenda simu rudi nalikuwa sipendi kutumia simu kwa
kuchelea kunifanya nishughulike, juu ya hayo nikawapigia simu nyumbani
kuwaeleza kuwa matokeo yaliotokea Makka sisi tupo Madina bado na tupo salama.
Hapo tena nyoyo zao zikatulia.
Kuelekea kufanya Umra Tulitoka hoteli yetu huko
Madina na kuelekea Makka na tulifika Miqaat sehemu ambayo ndio ya kutia nia,
wakati huo tumevaa shuka zetu mbili moja ya juu na ya pili ikiwa saruni (Ihram)
na bila ya kuvaa kitu chengine chochote kile. Tulipofika Mikaat tukasali rakaa
mbili na kutia nia kwa kusema “Lababaika Allahuma Bil Umra” na kuanza kutoa
tamko la Talbiya pasina kusita tukiwa kwenye magari ya mabasi tunaelekea Makka
‘Labbaika Allahumma Labbaika, Labbaika Laashariyka Laka Labbaika, Innalhamda Wa
Nni’mata Laka Walmulku, Laa Shariyka Laka.” Tuliendelea na kusoma Labbaika hadi
tukafika Makka na moja kwa moja tukaweka mizigo yetu nakuelekea kufanya Tawaf
na Sai. Viongozi wetu ni weledi wengine ni Hijja yao inakaribia ya 20 ikiwa
tangu wanasoma hapo Makka na hadi sasa wanaendelea kwenda Hijja na kutuongoza,
tulifika kwenye Alqaba na kuanza kutufu. Tumerahisishiwa kujua hasa wapi
pakuanza Tawaf kuanzia kwenye Jiwe jeusi-Hajjara alAswad, hapo kuna taa ya
kijani inawaka saa zote ukifika hapo ikiwa bega lako la kushoto ndio linaelekea
Alqaba na bega lako la kulia umeweka wazi, unaanza kwa kusema “Bismi Llahi
Allahu Akbar” na kuanza kuzunguka Alqaba mara saba, mara 3 za mwanzo unakwenda
mwendo wa mchupo unaitwa mwendo wa Matiti na upande wa kulia wa bega lako lipo
wazi, unapofika Rukul Yamani unasoma “Rabaana Aatina Fiduniya Hasanat
Awafil-Akhirat Hasanat Waqina Adhaba Naar.”
Kila ukifika Rukul Yamani unasoma
hivyo na Rukul Yamani ipo baina ya Maqam Ebrahim na kwenye jiwe jeusi.
Tulipomaliza mizunguko 7 tukasali rakaa 2 Maqam Ebrahim tukanywa maji ya Zamzam
ambayo yapo chekwa yanawasuburi Mahujaji tu, kisha tukaelekea Saayi baina ya
Swafaa na Marwa, unaanza jabali Swafaa unatoaa Takbir mara 3 na kwenda Safa
mara moja na ya pili kuwa Marwa na kumalizia Marwa. Unapoanzaunasoma:
“ ج
ا َّ
َ ْ
ح ن
َ َم
ف ِ
ِر اللّه
ِ آئ
َ ن
َشع ِ
َ م
ة َ
و ْ
ر َ
الْم َ
ا و
َ صف
ن ال
َّ َّ
إ أَن
ِ ِ
ه ْ
لَي َ
ع َ
اح َ
ن ُ
َالَ ج
ف َ
ر َ
َم ت
ْ ْ
َت أَِو
اع ي
َ لْب
ٌ يم
ِ ل
َ ع
ٌ ر
َ َشاكِ
ن اللّه
َّ ِ
إ َ
ا ف
ً ر
ْ ي
َ َ
خ وع
َطََّ ن
ت َ
م َ
ا و
َ م
َف ِبِِ
و َّ
َّ ط
َ )851:2( ي
Tulipomaliza kufanya Saayi tukapunguza nywele tukaelekea hoteli tulipofikia na
kuvua nguo za Ihram na kuvaa nguo za kawaida. Siku hii ya Umra kwangu ilikuwa
ni siku refu, kwani mwenzangu tulipoteana na matokeo hakufanya Saayi kwahio
alitakiwa airejee tartibu nzima ya Kutufu na kufanya Saayi, ikabidi nifwatane
naye na kumuonyesha mizunguko 7 ya Tawaf kisha na Kufanya Saayi, baada ya hapo
tukatoka saa 7 ya usiku kwenda yeye kuirejea Umra na mie kuzidi kuipa nafsi
yangu uneyenyekevu kwa kuwa naikabili Alqaba na kisha kuwa kwenye Swafaa na
Marwa. Nikisimama pembeni ya Alqaba Kabla ya Tarehe 8 Baada ya hapo kwa siku 6
mfululizo tukawa tunaelekea Msikiti wa Makka na kuwa tunajitahidi kusali
vipindi vyote kwa jamaa. Viongozi wa kikundi mara nyingi inapofika usiku huwa
wanatufanyia Semina, kuzidi kutuongoza kwenye ibada tusiwe tunafanya makosa.
Semina hizi walitufanyia tangu nyumbani ikiwa kama 10 mie nilikosa moja tu
kuhudhuria na Semina zote za Makka na Madina hakuna nilioikosa kwani hizi
Semina ndio zinaongoza na unapokuwa una mashaka unauliza katika jitahada za
kukuwezesha kuifanya Hijja yako iwe katika mstari. Ilipofika tarehe 8 Inapofika
tarehe 8 ndio Hijja inaanza kuanzia tarehe 8, 9, 10, 11, 12 hadi 13 ikiwa ni
siku 6.
Siku hizi zinakuwa zauneyenyekevu na kukupa taswira ya Qiyama, kukupa
taswira ya Masahaba walivyojitolea, inatoa taswira ya uneyenyekevu na
ustahamilivu. Tuliondoka hoteli milango ya asubuhi kuelekea Mina sehemu ambayo
kuna Mahema, hapo kuna Mahema yenye AC-Viyoyozi na kuna yasiokuwa nayo na hali
ya nyuzi joto ilikuwa baina ya 47-49 (47-49 0C) hali ni nzito hapo tukawa
tunasali sala ya Safari ambayo kwetu ilikuwa kila mtu ana kitabu juu ya sala ya
safari na viongozi kutueleza kuwa tunasalai Safar. Tulilala Mina hadi kusali
Alfajiri, kisha tukaelekea Arafa siku ya tarehe 9 na kuitumia siku nzima Arafa.
Tuliingia Arafa kwa kupitia Dhabb na tukarejea kwa kupitia Ma-zamiin kama
alivyofanya Mtume (SAW). Arafa kila kikundi kilikuwa na miongozo yao, lakini
ilikuwa ni kuomba na kuomba na kusoma Qur’an na kutoiwachia dakika ikutoe ndani
ya upuuzi, dua yangu ilikuwa lisinitokee lolote nikawa sipo Arafa, kwani “Hijja
ni Arafa” utapoikosa Arafa ndio itabidi urudie tena Hijja yako. Umma wa watu
milioni 2 na nusu wote ulikuwepo hapo, wapo waliokaa kwenye Mahema na kuna
ambao kwa siku nzima hawakuwepo kwenye mahema.
Arafa munapewa chakula cha bure
ikiwa hukuma ndio wanasimamia kupatiwa Mahujaji chakula pasina malipo.
Lilipozama jua tulielekea Muzdalifah hio ikiwa ni tarehe 10, tuakalala hapo
Muzdalifah ikiwa hakuna hema hakuna nyumba nyote mnalala hapo ikiwa nyote
mnalala kwenye mabusati, hapa unaona namna Uislamu unavyondosha umimi na ubwana
na kuwafanya wote ni wa moja kitu sawa, unaondoka Muzdalifah baada ya kusali
sala ya Alfajiri. Muzdalifah hapa ndipo unapookota vijiwe ambavyo hayatakiwi
majiwe kama wengine hutafuta mawe makubwa na kuvurumisha kwenye Jamraat na
kutoa maneno makali, vijiwe viwe kama punje ya nafaka, unaokota vijiwe viwe 7,
21 na 21 jumla 49 lakini ni vyema ukaokota zaidi ya hivyo hata ikifika 60 sio
mbaya kwani vinaweza vikakupotea. Niliokota vyangu na vya mzee ambaye tukikaa
pamoja hakuweza kwenda kupiga mawe ikawa nimchukulie, nijipigie na nimpigie.
Kuondoka Muzdalifah Ikiwa sasa kurudi Mina kunapokuchwa na kuelekea Jamraat.
Uongozi wa Saudi Arabia uliwaeleza mataifa yote kuwa watatakiwa wende kwa
wakati waliopangiwa. Kiongozi wetu akatuambia kuwa yeye akifika Mina hanywi chai hamsubiri mtu kuelekea kupiga mawe, asioweza abaki, anayetaka kunywa chai
anywe yeye hasubiri. Mie nikimuunga mkono pasi kujua kwanini naunga mkono amri
inayokaribia kuwa ya kijeshi.
Taib, saa mbili safari ya kuelekea Jamraat
ikaanza tukafika kiguzo cha mwisho kwani ni viguzo vyote ni 3 hapo tukapiga
mawe mara 7 kisha tuakaelekea kufanya Tawaf ya nguzo kama vile tulivyotufu
kwenye Umra, kisha tukanyoa, kuchinjiwa na kubadilisha nguo na kuvaa nguo za
kawaida baada ya zile shuka 2 na kubakia hoteli hadi usiku tukarudi Mina.
Tukarudi Mina katika Ayyam-e-Tashreeq (10, 11, 12, 13) tukenda siku iliofwata
tukapiga viguzo 3 kila kiguzo mawe 7 na siku iliofwata tukafanya hivyo hivyo
nakurudi Makka wengine wakipanda magari inayoweza kukuchukua muda wa saa 3
kufika Makka kutokana na msongamano wa magari na kina sisi wazee tunaojiweza
tuliamua kwenda kwa miguu muda wa saa nzima kufika Makka. Tulitakiwa tuwe
tunafanya mazowezi ya kutemebea na kwa kipindi cha miezi 2 mfululizo nilikuwa
natembea kwa muda wa Saa kila siku, kitu kilichokuja kunisaidia katika ibada
nzima ya Hijja. Kwahesabu tulioifanya nikuwa ule msongomano ulioleta msiba wa
kufa Mahujaji kwa kukanyagana tokeo lile lilipishana na kikundi chetu sio zaidi
baina ya dakika 5 na 10, kila kitu ni Maktoob yaani kinaandikwa.
Tukamalizia
nakufanya Tawaf-e-Wida na hiyo ndio kuikamilisha mzunguko mzima wa Hijja. Baada
ya kukaa Makka na Madina kwa wiki tatu tulirejea nyumbani salama na kupokewa na
ndugu na marafiki. Sahib yangu mmoja alinambia ikiwa Hijja ina misukosuko na
taabu na shida hapo ndipo unaipata hisia za Hijja, naam, tulikaa uwanja wa
ndege ikiwa ndege yetu inatakiwa itubebe Mahujaji 260 imekuja ndege ya kuchukua
watu 220 kwahio tukabaki uwanja wa ndege kwa masaa zaidi ya 24 kusubiri ndege
nyengine kutoka Ethiopia. Tukirudi nyumbani salama Risala hii ni safari yangu
na namna nilivyoitekeleza ibada sitotaka kuyatoa na kuyaeleza yalionakasoro ila
makala nyengine nitajaribu kuelezea namna ya kujipanga na nini vikundi vyetu
vya Tanzania vifanye kwa nionavyo. Nawaombea Waislamu wote Amani na utulivu
katika nyakati hizi na kumuomba Allah tulioenda Hijja ibada zetu azikubali na
walio na nia awafikishe kuweza kwenda kutimiza nguzo hii ya 5 katika Uislamu.
(Wasiliana na mie kupitia zuwarde@gmail.com au kwa simu 0777436949)
No comments:
Post a Comment