PNC 1JF-Expert Member
New
Asante wazanzibar Mungu asaidie Maalim apewe ushindi wake
Ntaluke.N.JF-Expert Member
New
Dr.Shain kasema ni rais halali wa Zanzibar..pamoja na kuwa na historia mbaya pale Uchaguzi unaporudiwa kwa bara la Afrika bado CCM wanajiandaa na uchaguzi Unatakaofanyka Februari kwa mujibu wa gazeti la RAIA MWEMA.
MlaleoJF-Expert Member
New
Kwanini Watu Wanaabudu Mungu? maana vituko wanavyofanya ni vya ajabu.... Dhurma haitakiwi nadhani wamelisahahu kuwa Dini zinakataza... Huyo Jecha atafutwe na aweke wazi moyo wake kama ni Mcha Mungu otherways Ajiunge na Freemason tu tuelewe ni Mjenzi huru Wachina hawamjui Mungu lakini hawafanyi Mambo ya ujinga uonevu na mabaya kama wacha Mungu waliopo Duniani
SIGNATURE
- New
simplemindJF-Expert Member
New
MysteryJF Gold Member
New
Mmenena vyema Maimamu wa Zanzibar.
Hakuna suluhu nyingine yoyote huko Zanzibar, zaidi ya kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais, aliyeshinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25/10/2015.
Hoja hiyo inakuwa na nguvu zaidi tukitilia maanani kuwa waangalizi wote wa ndani ya nchi na wa jumuiya ya kimataifa walitoa taarifa zao kuwa uchaguzi huo wa Zanzibar uliendeshwa kwa mazingira ya uhuru na haki, na kuthibitisha hilo ni kuwa fomu zote za matokeo kwa majimbo yote 54 ya huko Unguja na Pemba ziliwekwa saini na mawakala wote wa vyama wakiwemo wa vyama vikuu vya siasa vya huko Zanzibar vya CCM na CUF.
Kulithibitisha hilo ni kuwa hata wawakilishi waliochaguliwa kwenye majimbo yote hayo 54 walikabidhiwa vyeti vyao vya ushindi na wasimamizi wa uchaguzi huo kwenye majimbo husika.
Kutokana pia na tangazo hilo la kuufuta uchaguzi alilolifanya Mwenyekiti wa ZEC Jecha kuwa halina uhalali wowote kisheria.
Kwa mazingira hayo uamuzi wowote utakaofanywa na watawala kinyume cha kumtangaza mshindi aliyeshinda kwenye uchaguzi wa tarehe 25/10/2015 watawala hao watakuwa wameamua kwa makusudi kuitumbukiza nchi yetu kwenye machafuko makubwa.
- New
simplemindJF-Expert Member
New
Dire need for zomea
MlaleoJF-Expert Member
New
Why Zanzibar ifutwe nayo ibakie Mikoa tu Raisi asiwepo Magufuli Aingie na kutumbua Majipu hadi nchi nzima ikae Sawa... maana kuna Harufu ya Ubaguzi tu Hawataki Mpemba atawale Visiwa...
Kuna issue nilisikia wanaogopa atawarejeshea nchi kwa waliopinduliwa maana ni Yao mgogolo huu ushakuwa kama wa Israel na Palestina
SIGNATURE
kagombeJF-Expert Member
New
MysteryJF Gold Member
New
Hiki ni kipindi kigumu sana ambacho Taifa letu linapitia kutokana na mkwamo wa kisiasa wa huko Zanzibar ambako watawala wlioko madarakani wameamua kuutengeneza mgogoro wa kisiasa kwa ajili tu ya masilahi ya chama chao tawala kutokana tu na kugundua kuwa mgombea wao wa CCM Dr Shein alikuwa amebwagwa na mgombea wa CUF Maalim Seif.
Ni jambo la muhimu sana kwa wakati huu viongozi wa CCM wakaweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kukubali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015.
Hasa tukizingatia kuwa 'kiburi' cha watawala wetu kimeanza kulitafuna Taifa letu baada ya serikali ya Marekani kuzuia msaada wa nchi yao kupitia mfuko wa MCC kwa nchi yetu wa zaidi ya dola za marekani milioni 472.
Tutambue pia kuwa Marekani ndiyo kiranja wa dunia hii, kitendo chao cha kuanza kuikatia misaada Tanzania ni lazima kitaungwa mkono na mataifa mengine makubwa hususani mataifa ya Ulaya.
Kwa hiyo watanzania wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunapaswa kulaani kwa nguvu zetu zote hila za watawala wetu wa CCM kule Zamzibar ya kutaka kuendelea kung'ang'ania madarakani kama vile Mwenyezi Mungu amewapa wao hati miliki ya kuitawala nchi yetu hadi mwisho wa dunia!
Ntaluke.N.JF-Expert Member
New
- New
nash2010JF-Expert Member
New
Nilijua ushaleta "vitu" vyako
SIGNATURE
evansGREATDealSenior Member
New
SIGNATURE
Andrew NyerereJF-Expert Member
New
Wangemwandikia pia balozi wa Urusi.
JFK wabongoJF-Expert Member
New
Mapinduziiiiii, Daimaaaaa!
JFK wabongoJF-Expert Member
New
JFK wabongoJF-Expert Member
New
Wednesday, 6 January 2016
KUTOKA JF KUHUSU TAMKO LA JUMUIYA YA MAIMAM ZANZIBAR (JUMAZA) KUHUSU UCHAGUZI ULIOFUTWA
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment