Aliyenitumia
alitaka niihariri kwanza kisha kama naona inafaa niiweke hapa. Mimi sijaona
haja ya kuihariri. Naiweka kavukavu kasoro jina lake tu:
"A.alaykum.
Natamani ningeandika kama post yangu ila kwa usalama wangu napitia kwako ukiona
inafaa kuiweka au pia kuihariri kabla.
Mimi
ni mtumishi wa umma kupitia shirika la serikali.
Kushiriki
katika kura ya Jumapili, 20 March 2016 nikuisaliti nafsi yangu. Siwezi
kuisaliti nafsi yangu na nafsi za wanyonge walio wengi eti kwa kisingizo cha
kulinda ajira yangu. Ajira. Sikuajiriwa kwa sifa ya kupiga kura. Kura imo ndani
ya ridhaa ya nafsi yangu. Kura ni uhuru wangu.
Sitaki
kwa sababu uchaguzi uliopita sikuona hekaheka za kulazimishwa. Iweje uchaguzi
huu nilazimishwe. Uchaguzi uliopita sikuona bakora kuwatesa wanyonge. Uchaguzi
huu, wanyonge wanateswa eti kwa kuwa wameyaamua yale wasiyoyaridhia
wanga'ng'anizi wa madaraka.
Kama
tume haiingiliwi katika maamuzi, basi na tume ya moyo wangu haiingiliwi katika
maamuzi ya kwenda au kutokwenda kupiga kura. Kufukuzwa kazi kwa hili kutaacha
historia katika uhai wa maisha yangu. Natamani niwe shujaa katika jambo hili.
Siendi kupiga kura. Sipigi. Mnatosha na askari wanatosha kupiga kura. Wasipige
watu tu, wapige kura. Jumapili ni siku yangu nzuri ya kupumzika.
Mungu
ibariki Zanzibar.''
No comments:
Post a Comment