Mara kwa mara hupenda kuainisha baadhi ya matokeo ya nchi yetu na fikra za waandishi waliaondika vitabu maarufu duniani. Moja ya post yangu kuhusu kupigwa kwa raia Zanzibar katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa marudio nilimkumbuka James Baldiwin na kitabu chake mashuhuri, ''The Fire Next Time.'' Leo asubuhi nilipokuwa natalii mitandao ya kijamii na kuona jinsi watu wasivyoonekana katika mistari mirefu ya wapiga kura kama ilivyo kawaida ya chaguzi za Zanzibar palepale kikanijia kitabu cha Lewis Caroll, ''Alice in Wonderland,'' kitabu ambacho kinaeleza mikasa katika nchi ya ajabu. Zanzibar hii leo inaandika historia mpya ya kuwa kisiwa cha ajabu na mikasa. Kuna wakati nikisoma habari za Mazombie nikawa naifananisha Zanzibar na Haiti ya Papa Doc na kwa hakika ikawa inarandana kabisa. Nawaona Ton Ton Macoute wa Haiti ndani ya Mazombie. Lakini kubwa ni pale serikali ilipotoa kauli kuwa hawajui kama kuna watu wanaranda mitaani na silaha za jadi na silaha za moto wakipiga wananchi na wakiingia katika studio za radio na kuvunja mitambo na kuwapiga watangazaji. Nikawa najiuliza Zanzibar kisiwa kilichojulikana kwa usomi wa dini ya Kiislam na ustaarabu wa miaka mingi imefikaje hapa...
Wasimamizi wa wapiga kura Zanzibar |
Kituo cha kupiga kura |
Kituo cha kupiga kura
Kituo cha kupiga kura |
Hamad Rashid akitoka kupiga kura
Ghost Town |
Zanzibar imeshuhudia kitu ambacho kitaelezwa kwa miaka mingi ijayo vizazi kwa vizazi. Siku mji kwa ghafla ulipopotea, watu wakawa hawaonekani barabarani na mitaani na maduka yote kufungwa. Watu wamejificha ndani ya majumba yao kuepusha shari. Mji na mitaa iliyojaa shughuli, fumba na kufumbua umekuwa kile kinachojulikana kama, ''Ghost Town,'' yaani mji usiokuwa na watu. Huenda si watu wengi wanajua nini maana yake. Kwa ufupi, ''Ghost Town,'' ni mji uliohamwa na mara nyingi huwa baada ya kutokea vita au nakama nyingine yoyote ile kama tetemeko la ardhi. Hali ikiwa hivi watu huhama mji kwenda kutafuta hifadhi kwengineko. Binafsi nimeshuhudia, ''Ghost Town,'' Uingereza mwaka wa 1992 kwenye mji ujulikanao kama Tilbury nje kidogo ya London. Siku za nyuma Tibury ilikuwa bandari na watu wa mji ule wengi walikuwa wafanyakazi bandarini. Katika miaka ya 1980 wakati wa utawala wa Margret Thatcher mji ulikumbwa na matatizo ya uchumi ikawa hakuna meli zinazoingia bandarini kuleta au kuchukua bidhaa. Ikabidi bandari ianze kufifia kidogo kidogo na watu wakaanza kuhama mji. Maduka, mahoteli na nyumba zilizokuwa zimapangishwa ghafla zikawa hazina wateja. Nilifika Tilbury kwa treni mchana na nilipata mshtuko mkubwa. Natembea njia nzima kama unavyoona hapo juu Michenzani ilivyo, niko peke yangu kiasi nasikia hadi mlio wa sauti ya kiatu changu kinapogonga barabara. Hakuna paka, mbwa wala nzi...wala husikii sauti ya kitu chochote. Kwa mukhatasari Zanzibar ndivyo hivi ilivyo kwa sasa.
Kura iliyoharibiwa |
Kura iliyoharibiwa |
Idadi ndogo wajitokeza uchaguzi wa marudio Z’bar
Jecha |
Kura inaharibiwa kwa kukusdia |
Nipashe, Jumatatu 21 Machi 2016 |
Mwananchi Jumatatu 21 Machi 2016 |
Nipashe, Jumatatu 21 Machi 2016
Mtu wakala, lakini akiulizwa wa chama gani hajui.
Wakiona Camera, wanainama chini kama vile wamefumaniwa na wake zao.
Inafika wakati mpaka ripota kicheko kinamjia kwa nguvu kwa jinsi gani Wazanzibari tunavyofanya manyago ya kila aina.
Kila kitu: wamekwenda kusali, wewe msimamizi huna dini?
Kutoka Facebook
Mheshimiwa Jecha alitowa matokea ya uraisi wa Zanzibar chapchap ndani ya masaa 16 tu. Utaratibu wa mara hii alioutumia ni tafauti na wa chaguzi zote. Kwanza matokeo hutolewa ya jimbo moja moja, ndio baadaye ndio yanatolewa majumuisho.
TUNACHOKISUBIRI mpaka sasa na matokeo ya uraisi kwa kila jimbo ili tuone hizi kura alizopata Mh. Ali Shein na kufikia hizo 299,982. Hapa ni sawa na kusema kura 299,982 gawa kwa majimbo 54 ni sawa sawa na wastani wa kura 5,555.22 kwa jimbo. tuone hapo. Vile vile tuwaone wapiga kura waliojitokeza siku hiyo ambao ni 341,965 gawa kwa majimbo 54 wastani waliojitokeza ni 6,330.83 kwa jimbo licha ya ukimnya uliotawala siku ile mpaka makarani kuchapa usingizi.
RAIS DR SHEIN anaingia kwenye record za Dunia?
Dr. Ali Mohamed Shein anaingia kwenye rekodi ya dunia kama mojawapo ya viongozi waliowahi kuchaguliwa kwa asilimia kubwa ya kura baada ya kupata 91.4% ya kura zote zilizopigwa huko Zanzibar hapo jana.
Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya viongozi wengine maarufu waliowahi kuchaguliwa kwa kura nyingi:-
1. Dictator Sadam Husein yeye aliwahi kupata asilimia 100%
Saddam Hussein - Wikipedia, the free encyclopedia
2. Dictator Gnassingbe Eyadema aliwahi kupata 99.9%
Togolese presidential referendum, 1972 - Wikipedia, the free encyclopedia
3. Dictator Nursultan Nazarbayevalipata 95.5%
Elections in Kazakhstan - Wikipedia, the free encyclopedia
4. DictatorHeydar Aliyevalipata 98.8%
Azerbaijani presidential election, 1993 - Wikipedia, the free encyclopedia
5. DictatorAyaz Mutalibovalipata 98.5%
Azerbaijani presidential election, 1991 - Wikipedia, the free encyclopedia..
6. DictatorOmar Bongoalipata 100%
Gabonese general election, 1973 - Wikipedia, the free encyclopedia..
7. Rais Dr Ali Mohamed Shein alipata 91.4%
[Update] Ruling party candidate wins Zanzibar re-run election by 91.4%..
8.Dictator Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga alipata 99.16%
Zairean presidential election, 1984 - Wikipedia, the free encyclopedia..
9. Dictator Robert Mugabe alipata 92.76%
Zimbabwean presidential election, 1996 - Wikipedia, the free encyclopedia..
10. DictatorTeodoro Obiang Nguema Mbasogoalipata 95.36%
Equatorial Guinean presidential election, 2009 - Wikipedia, the free encyclopedia
Mwenye macho ya kuona na aone.
|
Ali Karume |
Mashallah tuteme mate chini... Muapishwa katika jimbo letu la Malindi pale Oktoba 25 alipata kura 2,234....ila katika "demokrasia ya marejeo" ya Machi 20 amepata kura 5,875....kwa hivyo kupata kura 3,539 za ziada... mashallah mashallah
Ati Pemba waliojitokeza na kumpa kura Bwana mkubwa ni watu 60,000. Yaani kachukua wale wake 17000 aliopata, na wale 30,000 waliowanyima vitambulisho wakashindwa kupiga kura october tarehe 25 ilhali wamo katika daftari, akaona bado akachukua na 13,000 katika kura laki moja zetu ili tu afikie asilimia 40 ya wapiga kura wote walioandikishwa katika daftari Pemba.
Anataka tuamini kwamba pemba kulijitokeza watu takriban 400 kwa saa katika kila jimbo ili kukidhi haja ya hizo kura 60,000 za kwake tu alizoshinda wakati watendaji wa tume wakinsinzia kwa kukosa watu. Kuota mchana, kwani wangalijiibia hizo kura 20,000 za kawaida wangelipungukiwa na ushindi wakati wapo peke yao? Uwatukane wapemba halafu na kura uwaibie.. Baniani mbaya ..
No comments:
Post a Comment