Katika moja ya vitu nikimuhusudu Bwana Ally Sykes ni jinsi alivyokuwa hodari
wa kutunza nyaraka na kumbukumbu.
Alikuwa na tabia ya kuweka katika jalada chochote atakachokuandikia au wewe
utakachompelekea katika maandishi.
Nyaraka zote za TAA na TANU alikuwa akiziweka kwenye ''safe,'' na zile za kawaida
akizihifadhi katika ''filling cabinet'' na akijua majalada yake kwa majina.
Utasikia akimwambia secretary wake Bi. Zainab, ''Hebu nipe ''file,'' la fulani.''
Nina hisi hata mimi amenifungulia jalada ingawa sikupata kuliona kwani iko siku
alinitolea ''notes'' niilizochukua katika mazungumzo tuliyofanya miaka 20 iliyopita.
Nilipigwa na butwaa.
Bwana Ally alikuwa na picha nyingi sana za wakati wa kupigania uhuru na
akizitunza kama nembo ya jicho.
Katika moja ya vitu nikizozana na Bwana Ally Sykes ni nyaraka zenye taarifa
za taifa hili yeye kukataa kuzikabidhisha kwa Tanzania National Archive (TNA).
Bwana Ally alikuwa na kisa na sababu za kuamua kukaanazo mwenyewe
nyaraka zake.
Alipata kunieleza mkasa uliomfika katika siku za mwanzo za uhuru kuhusu hizo
nyaraka hiyo kwake likawa funzo.
![Click this image to show the full-size version. [IMG]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXNGf0Mi92rXq7Yj0FSJ-0BB1ramlQ0NAksxWAmL99F9WzdZgSjqS0dHRqqO-VKDQI5ShN9cF3jAJvKmiW6hehFMshpo7cj1TXySBr1ujkwT0f4BwZLVZ6aDyR1nwLWwV6dV2PKd2FYQY/s400/IMG-20160306-WA0082.jpg)
Hii picha nilipiga na Bwana Ally Muthaiga Country Club Nairobi tarehe 21 May
1989.
Muthaiga Club ni ''exclusive club,'' ya ''millionaires'' na ni Waafrika wachache sana utawaona katika club hii.
Bwana Ally alikuwa mwanachama toka mwaka wa 1967.
Nilikuwa kila nikenda Nairobi Peter Colmore akinialika hapo club na
tukizungumza mengi katika historia ya Afrika Mashariki katika miaka ya
1950 hadi 1960.
Jina lake hasa ni Peter Dashwood Murray Colmore.
Ilikuwa kupitia Peter Colmore nikaweza kuandika historia za wanamuziki
mashuhuri kama Frank Humplink, Mwenda Jean Bosco na Eduardo
Masengo.
| Peter Colmore akiwa nyumbani kwake Muthaiga |
Hapo Nairobi ndipo Ally Sykes alipoanza siasa mwaka wa 1947 alipotoka
Burma Vita Pili ya Dunia na ndipo alipojuana na wanasiasa wa wakati ule
hapo mjini kama Jomo Kenyatta, WW Awori, Tom Mboya na wengineo.
Wakati huu alikuwa kijana mdogo sana wa miaka 20 na alikuwa akihudhuria
mikutano ya siri ya Mau Mau.
Kwa hakika nimesoma mengi kutoka kwa Bwana Ally Sykes na siku zote
akinijulisha kwa watu kama mtoto wake.
Watu wote alionijulisha kwao niliweka kumbukumbu zao katika mazungumzo
yetu.
Alipokufa Peter Colmore February 2004 taazia zilizoandikwa na magazeti ya
Kenya zilikuwa za kurashiarashia.
Taazia niliyoandika mimi kutoka Dar es Salaam ilichapwa na The East African
na walistaajabu imekuwaje mimi nimemjua mtu huyu kwa kiasi kile.
Mimi niliwajibu kuwa Peter Colmore alikuwa baba yangu.
Lakini hata kabla sijakutana na Peter Colmore nikiwa mtu mzima mwaka 1995
Nikimjua toka utoto wangu.
Ofisi yake ilikuwa ilikuwa karibu na nyumba tuliyokuwa tukiishi Mtaa wa Lindi
mwisho karibu na Arab Street (sasa Nkrumah).
Peter Colmore: The Man With the Midas Touch - News
Bwana Ally alinijulisha kwa Jim Bailey.
Jim Bailey ndiye alikuwa ''owner'' wa gazeti la Drum Magazine likichapwa
Johannesburg.
Afrika Kusini wametengeneza Filamu ya maisha ya Jim Bailey inaitwa ''Drum.''
Nilimsaidia Jim Bailey kupitia mgongo wa Bwana Ally Sykes kuhariri na
kuchapa kitabu cha Nyerere cha picha: ''Nyerere of Tanzania.''
Nilimshangaza Mzungu kwenye ndege tukielekea Johannesburg ambako yeye
ndiko kwao nilipomwambia kuwa mimi ni rafiki ya Jim Bailey.
Ikasadifu kuwa wao walikuwa majirani.
Nikamwambia kuwa nataka nimtafute sahib yangu nikifika Johannesburg.
Alinipa pole.
Akanambia Bailey tumemzika mwezi uliopita.
Bailey ameacha Bailey African History Archive, Johannesburg na ameifanyia
historia ya Afrika hisani kubwa sana.
historia ya Afrika hisani kubwa sana.
Huu ni mkusanyo wa picha na makala kuhusu harakati za kudai uhuru wa Afrika
pamoja na mengi katika ukoloni.
pamoja na mengi katika ukoloni.
No comments:
Post a Comment