Thursday, 16 June 2016

KUTOKA JF:KATIBA YA TANGANYIKA 1950





Nguruvi3,
Kuhusu kusherehekea mapinduzi Wazanzibar wenyewe wananasihana
kuwa kuna mauaji yalifanyika katika mapinduzi haifai kusherehekea
kwani ni kinyume na mafunzo ya Uislam.

Nasaha zangu kwao ni hizo kuwa wamuogope Allah kwani yaliyopitika
ni ya kujutia.

Hakika nasimama katika kauli yangu kuwa sijamdharau na kumdhalilisha
Mwalimu Nyerere.

Ningeweza kuishia hapo lakini nitaongeza maneno ili nifahamike.

Nilichotofautiana na wanahistoria wengi na huu ndiyo ulikuwa msimamo
wa CCM katika historia ya TANU ni kuwa Mwalimu Nyerere ndiye aliyeunda
TANU 1954 (Angalia: Historia ya TANU, Chuo Cha Kivukoni, 1981).

Hapa ndipo tulipokhitilafiana mimi nikenda nyuma ya Nyerere nikaanza na
mwamko wa Waafrika kuanzia miaka ya 1929 na kw akutumia Nyaraka za
Sykes nikaeleza vipi siasa zilianza hadi kufikia 1950 walipoingia vijana kutoka
Chuo Kikuu Cha Makerere khasa waliokuwa Dar es Salaam wakishirikiana na
Sykes brothers Abdul na Ally Sykes walivyoleta mabadiliko ndani ya TAA.

Historia hii sasa inafahamika sina haja ya kuirudia kwa kirefu.

Hili la umuhimu wa Nyerere nilisema hivyo kwa muktadha wa mimi kuendelea
kutafiti katika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru.

Umuhimu wa Mwalimu Nyerere kwangu mimi katika historia ya TANU na ya
kudai uhuru...

Maana yangu ni kuwa kwangu mimi nimeshasahihisha kile kilichokosewa kwa
wanahistoria kudhani kuwa kabla ya Nyerere hapakuwa na kitu.

Inawezekana wengine waliandika hivyo kwa kutokujua na wengine labda kwa
kuelekezwa na wengine kwa kujipendekeza (Angalia: HAK Mwenegoha (1976),
John IlliffeEdward Barongo, Saadan Abdu KandoroKirilo na Seaton 
na Chuo Cha Kivukoni).

Mtafiti yoyote yule akiwasoma waandishi hawa walioandika historia ya TANU
watapata mshtuko mkubwa sana watakapokuja kusoma kitabu cha Abdul
Sykes
.

Baada ya kuandika historia ya TANU kama nilivyoelezwa na wazee wangu na
kuona nyaraka za wakati ule kuyakinisha niliyoelezwa kile kitendawili cha kuwa
kaja Nyerere Dar es Salaam 1952 kawa na ofisi, kawa na fedha za kuendesha
chama, kama na watu wa kumuunga mkono yote akiyafanya peke yake, kikawa
nimekitegua.

Sasa umuhimu wa mimi kuendelea na utafiti wa Mwalimu Nyerere na historia
ya TANU ndiyo sasa haupo tena.

Kama vile isivyowezekana kuandika historia ya TANU bila ya kumtaja Abdul
Sykes 
kwa kutaja jina moja tu kwani yako mengi ndivyo hivyo hivyo
isivyowezekana kuandika histora ya TANU bila ya kumtaja Mwalimu Nyerere.

Nina yakini nimeeleweka.

Katiba ya kwanza ikiwa unakusudia ile aliyopendekeza Gavana Edward Francis
Twining, 
waliyoiandika ni TAA Political Subcommittee na wajumbe wake ni hawa:
Mufti Sheikh Hassan bin AmirAbdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu,
Dr.Vedasto Kyaruzi, Said Chaurembo 
na John Rupia.

Hii ilikuwa mwaka wa 1950.

Swali la mwisho sina la kusema kwa kuwa nitakuwa nawasemea watafiti wengine.

Umuhimu wa Mwalimu Nyerere katika historia ya TANU umekoma kwangu kwa
sababu nimekamilisha nililokusudia.

Watafiti wengine wanaendelea (Angalia: Morton 2014).

Mwisho ningependa kusema kuwa umenipa sharti kuwa ''nisichanganye mambo''
kwenye kapu moja na ''nisitumie vitabu.''

Sijui vipi unaweza kufanya mjadala wa kisomi nje ya vitabu.

Ikiwa utaona nimeweka rejea za vitabu niwie radhi hali kadhalika ikiwa utaona
pia nimeweka yote katika kapu moja.

No comments: