Sunday, 19 June 2016

KUTOKA JF: BRENDON GRIMSHAW MHARIRI WA TANGANYIKA STANDARD 1968




Nguruvi3,
Umezungumza mengi ambayo hayana maana kwa hiyo sitajibu ila
hili la kumdhalilisha Abdul Sykes.

Mimi ndiye niliyemfufua Abdul Sykes kwa kuandika maisha yake na
ndiyo leo uko hapa unatokwa na povu na jasho.

Kitabu kimechapwa miaka 18 iliyopita lakini hadi leo kinavuma kila mtu
anakisoma tunakwenda sasa toleo la 4 katika miaka 18.

Kushoto ni Brendon Grimshaw
Unakijua kisa cha Brendon Grimshaw aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti,
Tanganyika Standard?

Unaijua taazia aliyomwandika Abdul Sykes baada ya kuona kuwa magazeti
ya TANU Nationalist, na Uhuru, yamemdhalilisha kwa kukataa kuandika
ukweli wa mchango wake kwa Nyerere na TANU yenyewe?

Mimi nimdhalilishe Abdul Sykes?
Nitaanzia wapi?

Huna moja ulijualo katika historia hii.

Wanamajlis,
Ikiwa mnataka kujua Grimshaw alisema nini kuhusu Abdul Sykes mwaka 
wa 1968 katika Tanganyika Standard semeni nitoe darsa In Shaallah.

Grimshaw akijuana na Abdul toka 1950s.

No comments: