Tuesday, 21 June 2016

KUTOKA JF: UNAJINASIBISHA NA CCM VIPI UNAWACHUKIA WAASISI WA TANU?






Mag3,
Mimi nisingekujibu kama usingenitaja.
Umeweka CCM kama utambulisho wako.

Mimi nitaanza na hapo.
CCM inatokana na TANU na TANU inatokana na TAA.

TAA ilikuwa African Association hadi 1948 ilipobadilisha jina na kuwa TAA.
Kleist Sykes ni muasisi wa AA na alikuwa si tu kiongozi akiwa katibu bali
alikuwa mfadhili mkubwa.

Mwanae Kleist, Abdulwahid alikuja na yeye kama baba yake kuwa kiongozi
wa TAA akiwa katibu (1950), katibu na kaimu raisi 1951 - 1952 kisha akawa
kaimu rais 1953 Nyerere akiwa rais.

Kama baba yake, Abdul alikuwa kiongozi na mfadhili wa TAA na TANU.
Lakini kubwa Abdul akaja kuwa mmoja katika wazalendo 17 walioasisi
TANU 1954.

[​IMG]
Abdulwahid Sykes ni huyo wa nne kulia aiyevaa miwani ya jua

Si haya tu hata hiyo nyumba ambayo leo ndipo yalipo makao ya CCM Dar es
Salaam alijenga Kleist Sykes na Abdul akifuatana na baba yake siku za
Jumapili wakati huo mtoto mdogo wa miaka mitano alishuhudia ujenzi wa
nyumba hiyo.

Nyumba yenyewe ndiyo hiyo hapo chini katika sherehe ya kufungua ofisi
ya AA mwaka wa 1933:

[​IMG]

Huu si uongo si hadithi wala si ngano.

Huu ni ukweli ambao kwa bahati mbaya unawachoma roho wengi kwa kuona
mbona haikuwa sisi tuliofanya haya?

Ikiwa wewe au yeyote yule wa mfano wako ana taarifa nje ya hiyo hapo juu
na aje barzani tujadili.

Sioni kosa gani Maalim Faiza kafanya kwa kukutag kwani sote tukijadiliana
hapa kuhusu historia ya nchi yetu kimezidi nini leo hata wewe kuhamaki?

Hakika mila yenu moja.
Unajinasibisha na CCM unawachukia waliounda TANU?!

Photo

[​IMG]
Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Avenue

Ajabu ya Rahman.
Shonde huishia tahayuri.

No comments: