Click hapo chini kwenye mshare mwekundu kusikiliza:
Mkutano wa kwanza wa wa TANU pale Ukumbi wa Arnautouglo ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.
Kulia: Idd Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere na Haruna Taratibu |
Mtangazaji wa Azam TV Faraja Kiongole na Mwandishi katika Kipindi
Maalum cha Mashujaa
Maalum cha Mashujaa
Video itawekwa hivi karibuni In Shaallah...
Katika kipindi hiki nilijaribu kueleza historia ya baadhi ya mashujaa ambao wanahistoria wamewaacha kuwatafiti na kuwaandika kwa makusudi au kwa kutojua michango yao. Katika maelezo yangu picha za mashujaa hawa ziliwekwa kwenye screen ya TV.
Naziweka baadhi ya picha hizi hapo chini:
Waasisi wa TANU jumla yao ni 17 lakini historia zao hazijulikani. Kati ya hawa 17 ni Abdul Sykes (The Life and Times of Abdulwahid Sykes The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika) na Julius Nyerere na Japhet Kirilo (Earle Seaton and Japhet Kirilo, ''The Meru Land Case''). peke yao ambao maisha ya yao ya siasa yamefanyiwa utafiti na kuandikwa kitabu. Ally Sykes akishirikiana na mwandishi ameandika kuhusu maisha yake ingawa kitabu bado ni mswada hakijachapwa (Ally Sykes and Mohamed Said, ''Under The Shadow of British Colonialism''). Lameck Bugohe ambae ni mmoja wa waasisi wa TANU amelalamika kuhusu hali hii ya kutoandikwa historia ya kweli ya TANU.
Soma historia ya Lameck Bugohe hapo chini:
Picha hii inaeleza historia ya Rashid Ali Meli mzalendo aliyefungua ''safe,'' ya kazini kwake Dar es Salaam Municipal Council alipokuwa akifanyakazi kama mwekafedha akatoa fedha zote na kuzipeleka kwa Iddi Faizi Mafongo zitiwe katika safari ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955. Rashid Ali Meli alifanya haya baada ya kuona kuwa juu ya michango iliyopita lakini fedha za safari zilikuwa hazijakamilika. Ilikuwa TANU warejeshe hizi fedha kwa haraka. Bahati mbaya sana siku ya pili tu wakaguzi wakafika kumkagua ilhali fedha haijarejeshwa. Huu kwa macho ya sheria ilikuwa ni wizi. Katika kipindi nimeeleza nini kilitokea.
Historia ya Iddi Faizi Mafongo na Haruna Taratibu zinapatikana hapo chini:
Hilo hao juu ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Sheikh Suleiman Takadir. Baraza hili lilikuwa ni baraza ambalo wajumbe wake wote walikuwa Waislam. Hili ndilo baraza lililompeleka Nyerere UNO mwaka wa 1955. Nyerere aliamua kulivunja hili baraza mwaka wa 1963 kwa kuwashutumu kuwa wazee hawa walikuwa wakichanganya dini na siasa.
Ali Msham alikuwa mwenyeji wa Kilwa na alihamia Dar es Salaam katika miaka ya 1950 kuja kutafuta maisha. Alifungua ''workshop,'' yake Kariakoo akitengeneza samani. Harakati za uhuru zilipoanza yeye alifungua tawi la TANU nyumbani kwake Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu. Siku moja alimtembelea Mwalimu Nyerere ofisini kwake New Street akasikitishwa na ile samani aliyoikuta katika ofisi ya Nyerere. Msham akaamua kumtengenezea Mwalimu Nyerere samani inayokwenda na hadhi ya rais wa TANU. Ilipokamilika alimualika Mwalimu Nyerere kwenye tawi lake la TANU ili amkabidhi zile samani ambazo ndiyo hizo hapo kwenye picha.
Katika kipindi hiki nilijaribu kueleza historia ya baadhi ya mashujaa ambao wanahistoria wamewaacha kuwatafiti na kuwaandika kwa makusudi au kwa kutojua michango yao. Katika maelezo yangu picha za mashujaa hawa ziliwekwa kwenye screen ya TV.
Naziweka baadhi ya picha hizi hapo chini:
Walioasisi TANU tarehe 7 Julai 1954 |
Soma historia ya Lameck Bugohe hapo chini:
Kushoto: Iddi Faizi Mafongo Mweka Hazina wa TANU Makao Makuu, Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Mwalimu Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro mmoja wa waasisi wa TANU 1954, Haruna Taratibu Muasisi wa TANU Dodoma. Picha hii ilipigwa Dodoma mwaka wa 1956 |
Picha hii inaeleza historia ya Rashid Ali Meli mzalendo aliyefungua ''safe,'' ya kazini kwake Dar es Salaam Municipal Council alipokuwa akifanyakazi kama mwekafedha akatoa fedha zote na kuzipeleka kwa Iddi Faizi Mafongo zitiwe katika safari ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955. Rashid Ali Meli alifanya haya baada ya kuona kuwa juu ya michango iliyopita lakini fedha za safari zilikuwa hazijakamilika. Ilikuwa TANU warejeshe hizi fedha kwa haraka. Bahati mbaya sana siku ya pili tu wakaguzi wakafika kumkagua ilhali fedha haijarejeshwa. Huu kwa macho ya sheria ilikuwa ni wizi. Katika kipindi nimeeleza nini kilitokea.
Nyerere akiwa UNO 1955 |
Historia ya Iddi Faizi Mafongo na Haruna Taratibu zinapatikana hapo chini:
Baraza la Wazee wa TANU 1955 |
Kulia: Ali Msham na aliyekaa katika meza ni Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere siku Ali Msham alipomkaribisha kwenye tawi la TANU Magomeni
alilofungua nyumbani kwake mwaka wa 1955
Historia ya Ali Mshama iko hapo chini:
http://www.mohammedsaid.com/2016/02/ali-msham-tawi-la-tanu-na-duka-la.html
http://www.mohammedsaid.com/2016/01/kutoka-facebook-ali-msham-na-julius.html
http://www.mohammedsaid.com/2016/01/kutoka-facebook-ali-msham-na-julius.html
http://www.mohammedsaid.com/2016/01/kutoka-fb-mjadala-wa-ali-msham-na.html
Earle aliisaidia sana TAA wakati uongozi ulipochukuliwa na vijana mwaka 1950 akifanya kazi kwa karibu sana na TAA Political Subcommittee hasa katika mambo ya sheria inayohusu makoloni yaliyokuwa chini ya udhamini kama Tanganyika ilivyokuwa chini ya udhamini wa Uingereza. Seaton alikuwa raia wa Bermuda na mwanasheria akifanya shughuli zake Moshi.
Habari za Earle Seaton hapo chini:
Historia ya Zuberi Mtemvu hiyo hapo chini:
Earle Seaton na Julius Nyerere |
Habari za Earle Seaton hapo chini:
http://www.mohammedsaid.com/2016/06/earle-seaton-bermuda-na-dome-budohi.html
Katika pilikapilika za kupambana na ukoloni wa Waingereza wako wazalendo walifungwa jela, Mwaka wa 1953 Ali Migeyo alipigwa mabomu Kamachumu wakati akihutubia mkutano wa hadhara. Alipelekwa mahakamani na akahukumiwa kifungo. Robert Makange na Rashid Kheri Baghdelleh walihukumiwa kifungu cha miezi sita kwa kosa la kuandika makala katika gazeti la Mwafrika makala ambayo Waingereza waliiona ni ya ''uchochezi.'' TANU kwa kuchukia kuona wanachama wake wanaitwa wafungwa waliwapa jina la, ''Prison Graduates,'' yaani, ''Wahitimu wa Jela.''
Soma historia ya Ali Migeyo hao chini:
http://www.mohammedsaid.com/2014/02/ali-migeyo-ushapata-kumsikia-shujaa.html
Katika mashujaa wanaostahili kukumbukwa ni Bantu Group ambalo lilikuwa kundi la vijana waliojitolea kuhamasisha umma kuingia TANU na wao ndiyo walikuwa walinzi wa Mwalimu Nyerere na viongozi wengine.
''Prison Graduate'' Robert Makange |
Soma historia ya Ali Migeyo hao chini:
http://www.mohammedsaid.com/2014/02/ali-migeyo-ushapata-kumsikia-shujaa.html
Katika mashujaa wanaostahili kukumbukwa ni Bantu Group ambalo lilikuwa kundi la vijana waliojitolea kuhamasisha umma kuingia TANU na wao ndiyo walikuwa walinzi wa Mwalimu Nyerere na viongozi wengine.
Waliosimama nyuma na silaha za jadi ni Bantu Group na waliokaa kulia ni Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia. |
Bi Titi Mohamed |
Rajab Matimbwa katoka Chole, Uzaramo kaja Dar es Salaam kijana mdogo kutafuta maisha. Rajab Matimbwa, Bi. Titi ni shangazi yake na akikaa nyumbani kwake Shauri Moyo. Harakati za kudai uhuru zilipoanza Dar es es Salaam Rajab akajikuta ana kibarua cha kuuza maji kwenye bomba moja lililokuwa linatazamana na ofisi ya TANU New Street (sasa Lumumba Avenue). Kabla ya kufanya kazi ya kuuza maji tayari Rajab alishapewa kibarua na John Rupia cha kuuza mgahawa pembeni ya Pugu Road na ikatokea akaelewana vizuri sana na Mzee Rupia na familia yake yote akawa mtoto wa nyumbani. Rajab anawakumbuka watoto wa Mzee Rupia, Paul na dada yake Kipanya, Mpuya (Stephen) na kaka yao mkubwa Albano. Mzee Rupia alikuwa na lori lake limeandikwa, ''Msichoke'' likibeba mijengo. Mikutano ya hadhara ya TANU ilipoanza Rajab aliwakusanya vijana wenzake wanne wakaanzisha kwaya ya kwanza ya TANU Rajab akiwa kiongozi na mtunzi mkuu wa nyimbo za kuhamasisha watu kujiunga na TANU na nyimbo za kuwasema Waingereza. Wanakwaya wenzake walikuwa Said, Abdallah, Juma, Binoga na Katumbwele. Said akatunga nyimbo ya kwanza iliyokuwa ikisema, '' Watanganyika njooni tuchanganyike tukisifie chama chetu cha TANU Mola akipenda tupate uhuru.'' Rajab akatunga, ''Sikia wana kuteseka nchi ni shida tupu yatukalia. Sisi Watanganyika tunateseka kutawaliwa ni fedheha.'' Hizi nyimbo zilipokuwa zikiimbwa pale Mnazi Mmoja kabla Nyerere hajapanda jukwaani zilikuwa zikiwajaza hamasa wananchi. Kwaya hii ilitunga nyimbo nyingi sana ambazo nyingine hadi leo bado zinaimbwa kama ile nyimbo maarufu, ''Tazama Ramani.''
Rajab Matimbwa |
No comments:
Post a Comment