Sunday, 24 July 2016

KUTOKA FB: MAGGID MJENGWA AIZUNGUMZA TANU




CCM Inabebwa Na Historia..
Ndugu zangu,
Ukisoma juzuu kama hiyo pichani kwenye maktaba yangu, basi, utakuwa na urahisi wa kupata tafsiri ya mengi yanayotokea leo kwenye nchi yetu.
Ni kwenye maandiko ya kitafiti ya mwaka 1981 ya wanazuoni wa aina ya Mwaga, Mrina na Lyimo unakutana na tafsiri ya mifumo ya vyama vya siasa Afrika inayokwenda mbele ya siasa na kuingia kwenye siasa ya vyama yenye kutokana na tamaduni, mila na desturi za kijamii.
Ukisoma historia ya TANU kwa umakini utaelewa kuwa kwenye Nchi kama ya kwetu hata vinavyoitwa vyama vya upinzani, mifumo yake bado ni ya Ki-TANU TANU na Ki-CCM CCM.
Haviwakilishi mbadala haswa wa kiitikadi, kifalsafa na kimfumo, bali manung'uniko ya kukosa fursa za urais, ubunge na uwaziri, au kwa tafsiri hiyo hiyo ya kutokuwa accomodated kwenye mifumo ya Ki- TANU TANU na Ki-CCM CCM.
Hatari iliyopo kwa vyama hivyo visivyokuwa na dola, ni pale chama kama CCM kitakapofanya mabadiliko makubwa na ya kishindo.
Vyama hivi vitadhohofika na vingine kufa kwa kukosa ajenda za kukamatia.
Hilo la mwisho ni jambo baya kutokea, kwa wote wenye kuamini umuhimu wa uwepo wa siasa za vyama vingi vyenye kuipa changamoto Serikali iliyopo madarakani.
Maggid,
Iringa.


Mohamed Said Salum Mwenyekiti niwie radhi sana. Hicho kitabu kinachodai kuwa ni historia ya TANU kwa kweli si historia ya TANU kama tuijuavyo wengi kwani wengine wazee wetu ndiyo waasisi wa hicho chama. Ukikisoma kitabu hakuna hata majina yao. Huwezi ukaandika kitabu cha TANU ukaacha kumtaja Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Amir kwa kuwataja wachache. Soma hapo chini kuhusu Hassan Upeka ikiwa unataka kujua zaidi kuhusu kitabu cha Historia ya TANU.

LikeReply25 hrsEdited

No comments: