Naweza kuamini kabisa haya uyasemayo pasipo shaka kabisa.
Sasa hivi nimeanza kufuatilia mihadhara yako mbalimbali kuanzia ile ya TV Stations, Radio Stations na hata Misikitini. Mimi always naangalia arguments za mtu irrespective anazungumzia wapi.
Mzee wangu Mohamed nilikuwa naangalia Clip yako moja ukagusia Habari ya bibi Titi Mohammed alivyofanyiwa, kwa lugha ya sisi vijana tunaita "Figisu-Figisu". Kwa kweli ilinisikitisha sana.
Mwanamama muhimu kama Bibi Titi, Leo hii humsikii kabisa katika historia ya nchi yetu. Yaana kwa ujumla, watu wachache waliibaka historia yetu.
Na kinachoniuma zaidi ni kufundishwa uchafu, uhongo, ujinga na upuuzi katika masomo yangu ya historia tokea niko Primary mpaka Secondary School.
Sasa hivi nipo naangalia video ya mahojiano yako kuhusu historia ya mzee Abdul Sykes
Lakini niseme jambo moja tu, Serikali imefanya makosa mkubwa sana, iwe kwa makusudi au kwa Bahati mbaya kuachia hizi nyumba ambazo wazee wetu walikuwa wanakutana kwa ajili ya harakati zao za kisiasa zibomolewe na pasiwepo alama yoyote ya kumbukumbu.
Hizi nyumba zilitakiwa kuwa makumbusho mahususi sana. Hili ni kosa kubwa kubwa sana kuwahi kufanyika katika nchi yetu. National Museum wangezichukua na kuzifanya sehemu ya utalii na kujifunza.
Yaani nipo hapa naangalia wazee wetu walikotokea, hizi nyumba zingetunzwa pamoja na hizo picha mbalimbali za wakati huo, hakika ingekuwa jambo zuri sana.
Kusema kweli imeniuma sana sana kwa serikali kushindwa kutunza hizi kumbukumbu.
No comments:
Post a Comment