Bi. Titi Mohamed na Julius Nyerere Viwanja Vya Jangwani Wakati wa Kupigania Uhuru wa Tangnayika Miaka ya 1950 Mwanzoni |
Hakika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ni kisa khasa.
Bi. Titi Mohamed anaghadithia anasema wako Tabora 1958 wakati
wa Kura Tatu.
Hali ilikuwa tete kupelekea TANU kumeguka pande mbili.
Baadhi ya wanachama wamekataa kata kata kuingia katika uchaguzi
ule wenye masharti ya kibaguzi.
Mwalimu Nyerere ameingiwa na hofu ana wasiwasi chama kitavunjika.
Wapinzani wa Kura tatu ni watu wenye nguvu katika chama wakiongozwa
na watu kama Jumanne Abdallah, Bhoke Munanka, Sheikh Suleiman
Takadir na wengineo.
Kushoto: Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir, Clement Mtamila na Bi. Titi Mohamed Nyuma Maria Nyerere, Rajab Diwani na John Rupia |
Mwalimu Nyerere akawa hana hata hamu ya kula chakula anashindia maziwa.
Bi. Titi akimmudu sana Mwalimu Nyerere na watu wengi hawajui hili jina la
Mwalimu Nyerere alipewa na Bi. Titi.
Bi. Titi kamfuata Nyerere anamwabia,'' Nini wewe nasikia hutaki kula. Unaogopa
kufungwa? Mwenzako Kenyatta yuko jela nini wewe unaogopa kufungwa?''
''Sikiliza Titi si lazima nende jela...''
Mwalimu alijibu kwa unyonge kabisa.
Bi. Titi Mohamed na Julius Nyerere Siku ya Uhuru wa Tanganyika 9 December 1961 |
Ukipenda kukijua kisa cha Kura Tatu ingia hapo chini:
Mohamed Said: UCHAGUZI WA KWANZA TANGANYIKA ''UCHAGUZI WA KURA TATU'' 1958 KUTOKA KUMBUKUMBU ZAKE SHEIKH SEMBE
Kitabu kilichoandika mengi katika historia ya uhuru wa Tanganyika |
No comments:
Post a Comment