Tuesday, 12 July 2016

KUTOKA JF: WANASEMA MAALIM SEIF ''KAKAANGWA,'' ''KATOLEWA JASHO,'' NDANI YA BBC NA SALIM KIKEKE


CUF kata ya Mzimuni Magomeni  Dar es Salaam wakisheherekea
ushindi serikali za mitaa uchaguzi wa 2015 Viwanja Vya Mtambani Magomeni
Mapipa







Stayfar,
Hakuna kiumbe mwenye akili timam awezae kumuabudu binadam mwenzake.
Hii ni kufru kubwa.

Hakuna anaemuabudu Maalim Seif ila wako wananchi wengi wanaomuunga
mkono kwa ajili ya siasa zake na uongozi wake.

Bahati mbaya sijakiona wala kukusikiliza kipindi lakini nitachangia.
Uchaguzi wa Zanzibar unaendeshwa ka sheria na kanuni.

Ikiwa ni hivyo basi ni lazima sheria ifuatwe vinginevyo ni vurugu kama hii ambayo
sasa imeikumba Zanzibar.

Uchaguzi ulifanywa na Dr. Shein akashindwa kama alivyoshindwa mwaka wa 2010.
Kakataa kushindwa kafuta uchaguzi kaitisha uchaguzi mwingine.

Tujaalie Maalim Seif angekubali kushiriki tena katika uchaguzi ule wa marudio.
Kitu gani kingemzuia Dr. Shein kufuta tena uchaguzi ikiwa angeshindwa?

Mtafiti yeyote anaefatilia siasa za Zanzibar anajua kuwa ni tabu sana kwa CCM kupata
ushindi dhidi ya CUF.

Sasa mambo haya hayataki ushabiki wa Maalima Seif yuko, ''kikaangoni,'' na Maalim Seif, ''jasho linamtoka.''

Hii si kweli.
''Mkaangaji,'' na ''mtoa watu jasho,'' ni Maalim Seif.

Rejea uchaguzi wa 1995.
Ali Ameir aliandika barua Tume kukataa matokeo ya kushindwa Salmin Amour.

Rejea uchaguzi wa 2010.

Maalim Seif asingetumia busara na hekima ya uongozi damu nyingi ingelimwagika siku ile pale Bwawani.

Mzee Hassan Nassoro Moyo shahidi wa hili pamoja na umma mkubwa wa Wazanzibari.

Ushabiki haujengi taifa.

Wazanzibari wanahitaji kutiwa moyo wakae kitako wajadili mstakbali wa nchi yao kwa faida ya vizazi vijavyo.

Wazanzibari wana mengi ya kujifunza katika historia yao kuanzia mapinduzi 1964 hadi leo.

Wazanzibari wa leo hawahitaji kuchonganishwa.

No comments: