Skukuu Ninayoikumbuka
Hamza
Z. Rijal
Jambo
kubwa la mtu kushukuru kwa muumba wake hakuna kama kupata umri mrefu ambao
unakuwa umo kwenye siha nzuri pamoja na akili timamu. Katika maisha, wengi wetu
kutokana na kukosa zile taaluma za kuweka kumbukumbu kwenye maandishi matokeo
yake hushindwa kuandika yaliotutokea na matokeo yake hukurupuka pale
linapotokea jambo kisha ukaliunganisha na siku zilizopita kwa kulisimulia na
kuishia hivyo.
Nimekula chumvi na nimekamilisha zaidi ya miongo 6 ya maisha namshukuru Mungu. Maisha yangu katika umri wangu nimeona mengi kama Waswahili wasemavyo kuishi kwingi kuona mengi na nitaongezea neno nalo sio kuona mengi tu na hata kupatwa na mengi.
Hii leo nitayaelezea kati ya hayo yakuona mengi yaliomo kwenye siku za skukuu namna tulivokuwa tukiipokea na jazanda ya skukuu katika miaka ya 50 na 60 tulivokua tukisheherekea.
Skukuu ya mfungo mosi na skukuu ya mfungo tatu hizi ni skukuu ambazo sio skukuu katika Uislamu tu bali zimekua ni sehemu ya mila yetu ya watu wa visiwani hata tukaja na msemo usemao Mkaidi hafaidi ila siku ya Eid, huku ni kusema kua Eid imeingia ndani ya maisha na utamaduni wa Mzanzibari.
Mara nyingi hasa skukuu ya mfungo mosi wazee hujitaarisha kuhakikisha kua mwanawe anapata nguo mpya na atajipiga mtu kwa kadri ya uwezo wake ahakikishe mwanawe anapata nguo mpya katika kipindi hicho, chembelecho sahib yangu aliofika kunambia kua katika maisha yake ya utotoni alikua akivaa nguo mpya mara mbili kwa mwaka, pale skuli inapofunguliwa hutakiwa avae sare mpya na katika siku za skukuu. Wazee wakijitahidi katika siku nne za kusheherekea skukuu kuhakikisha kila siku ya Mungu mwana atapata nguo mpya iwe ya mkono shilling au mavazi ya kina John White na Teralini, Lasi au hata Van Husen shati la bei ghali ukilivaa unaonekan ni kantika enhe.
Kuishehrekea skukuu ilikuwa ni mmoja kwa nchi nzima, mwezi unapoandama ikiwa wengi wetu tulikua hujikusanya pale Forodhani na mmoja kati yetu akauwona na huku askari mpiga mzinga akiwa na darubini yake akauwona, tena hapo unahakikishwa na kupelekwa salamu kwa mfalme na kutolewa amri mizinga ishirini na moja kupigwa. Kila mzinga ukipigwa huwa ni furaha hasa watoto utawasikia eeeh na huko ng’ambo majumbani utasikia vigeregere vimeshamiri na watu kutoka nje kukumbatiana na kuanza kupeyana salamu za Eid, Laidina wengine huja na kejeli sina jina wala sina pesa. Laidina wengine watakuja na jawabu Minal faizina, Awam bada awam, sininaa baada sinina.
Bada hapo tena akina mama huanza kupindua masufuria kwa maandalizi, visheti, mkate wa mayai, maandazi, mkate wakusukuma ingawa jina linapotea siku hizi ni chapatti, keki, mchuzi wa asubuhi alkhasir maandalizi kutoka magharibi hadi usiku wa manane.
Ifikapo asubuhi huelekea kusali sala ya Eid ambayo nyakati hizo idadi ya watu wa visiwa hivi ilikuwa haizidi watu laki tatu kwa hio misikiti iliokuwa ikisaliwa Eid ni michache kabisa, bada ya kusali Eid hapo tena watu wakipeyana mikono. Bada ya hapo wengi wa watu wakipendelea kwenda kuwakumbuka waliotangulia kwenye haki na kuwaombea kisha huwenda nyumba kwa nyumba kwa jamaa waliomhusu kisha humalizia kwa marafiki na inapofika milango ya saa nne au tano ndio mtu hufika nyumbani kwake nasisi ilikua kufika makwetu. Hapo tena huwa pameandaliwa kikweli na huliwa mlo wa furaha, hata wasiokunywa chai ya maziwa siku hio chai ya mkandaa au istighan huwekwa pembeni.
Bada ya chai kina sisi watoto hukaa na mzee akawa anatoa hikaya za siku zao, mara utasikia hodi, utampokea mmoja wa rafiki wa mzee mtamkaribisha na kuandaliwa iwe vileja, kisheti, keki na kahawa na mazungumzo yenye kufurahisha yasiokua ya siasa wala maisha magumu. Anapoondoka aliokuja kukupeni mkono wa Eid husomwa dua na kupakana mafuta mazuri na kuagana, yanaendelea hayo ingia toka hadi inapofika sala ya adhuhuri, baada ya sala tena utakuta mzee akiwa mama kwako mke kwa babako ameandaa maakulati itakua pilau na sharbati wala sio juice. Sharbati ni rangi la podari ya Portelo au machungwa inaongezewa na sukari au shira na arki na kuwekwa na barafu kila mtu atapewa gilasi moja na hakuna nyongeza hata wazee walikua na vipimo ambavyo nyumba zilikuwa na nidhamu yake ikiwa leo hayo hayapo.
Bada yamlo watu hupumzika hadi Alasiri kisha hapo husali na vijana kuelekea Mnazi Mmoja, raha, raha iliyoje Mnazi Mmoja unaingia na shilling moja yako na kama umekua na shilling 5 basi unaiona dunia yote ipo mikononi mwako. Watoto siku hizo wakipendana na wakionyesha mapenzi makubwa ambayo yakiwachukua hadi wanavyokuwa watu wazima, mie binafsi darasani mwetu tulikua watu 6 tukifwatana pamoja kwenda Mnazi Mmoja na saa nyengine ukakuta na wenzenu wengine mkaungana nao.
Mnazi Mmoja kwenye uwanja wa furaha na burdani ukiwa na Shillingi mmoja tu utafurahi, Karagosi psa nne, Zarina Psa nne, kisha kwenye beni psa nne, umepanda pembea psa nne umebakiwa na nusu shillingi, chauro, baajia na maji ya sharbati umebakiwa na psa nane hapo unaangalia nini ufanye unaweza kuzibakisha kwa siku ya pili au ukaimalizia kwa kula pamba na genderi hapo shilling ndio itakua imekhitimika, unarudi nyumbani na chauro na bajia na genderi na kuwageia wenzako, almuradi skukuu nzima umestarehe na kuiona ya furaha kabisa.

Mnazi
Mmoja kulikua na michezo ya kila aina ya kufurahisha, uliokua ukinivutia ni
Karagosi anaitwa katika njia za katuni, anaitwa “karagosi?” anaitika “eeenh”
hujambo atajibu “sijambo” kisha karagosi na mkewe vituko moto mmoja na mke wa
karagosi mwisho atapigwa rungu nasi sote tufurahi eeeeeh, na kwa utamu wa
karagosi unaweza kuingia mara ya pili ule utamu na akili yako kuhangaishwa yule
karagosi anavyochezeshwa, kwenye Zarina sina la kusema. Juu ya starehe zote
hizo watoto mwisho wao kuweko viwanja vya Mnazi Mmoja ni iliapo honi ikilia
yaani saa kumi na mbili na nusu, watu wazima nao hufika Mnazi Mmoja kuanzia
bada ya sala ya Magharibi na wao kujiburudisha. Skukuu ikiwa ni furaha tupu
kuanzia kwa wazee hadi watoto.
Jee leo? Hayasemeki wala hayana mshiko kwani Mswahili kapoteza ule utamaduni
aliokuwa nao aliuunganisha na Uislamu, nimetaja Mswahili kwa kuwa muasisi wa
Elimu Zanzibar L.W. Hollingsworth, alimueleza Mswahili ni yule aishiye katika
mwambao na anazungumza Kiswahili kama ni lugha yake ya mwanzo, kwa hio Mswahili
utampata Unguja, Pemba, Kilwa, Bagamoyo, Tanga, Lamu. Mombasa n.k. Waswahili
uendapo katika miji yao utawakuta minendo yao ni ya aina moja, haya nikutokana
kuwa Mswahili kajiunganisha maisha yake yote tangu anazaliwa mpaka anakufa na
Uislamu.
Hamzah Z Rijal |
No comments:
Post a Comment