Mwinyi Baraka |
Kushoto: Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Julius Nyerere, Sheikh Abdallah Chaurembo, Rashid Kawawa na Tewa Said |
Mwinyi Baraka na Nyerere |
Watatu kulia ni Mwinyi Baraka Sheikh Said Omar Abdallah
Kutoka
kulia kwenda kushoto: Waliokaa: wa kwanza ni Sayyid Ahmad Hamid Mansab Ibn
Shaykh Abi Bakr bin Salim (alikuwa akisomesha Nahw, na Sarf); wa pili kutoka
kulia ni Al-ällama alkabir Sheikh Sulaiman bin Muahammad Al-Alawi - huyu bwana
ni mwalimu wa karibu maulamaa wote wa Zanzibar na nchi jirani za Afrika ya
Mashariki- alilkuwa bahari isiyo na fukwe kwenye elimu mbali mbali.
Yeye
alisomesha Fiqh; Arudhi (elimu ya fani ya kutunga mashairi ya Kiarabu); Balagha
na kadhalika. Ni shida, kama si muhali, kumpata mwana chuoni ye yote katika
Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini, asiwe mwanafunzi wa Maulana huyu: Allah
yarhamhu.
Maisha
yake yote yalikuwa katika kusomesha dini tu, tokea anaamka hadi anakwenda
kulala.
Msikiti
Gofu ulikuwa ndio mahali anaposomesha kuanzia baada ya sala ya Alfajiri, hadi
baadaye kwenda Muslim Academy, na akirudi baada ya sala ya Adhuhuri hadi baada
ya sala ya Isha. Allah yarhamhu wa yuskinuhu al-Janna.
Wa
tatu kutoka kulia na Sayyid Umar bin Abdallah Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim
(Mwinyi Baraka). Yeye alikuwa Mwalimu Mkuu wa Muslim Academy. Wa nne kutoka
kulia ni Sayyid Abdurrahman bin Hamid Al-Sirry - Huyu Bwana alikuwa bahari
katika elimu za Lugha, Mashairi na fani nyengine. Yeye alisomesha Arabic
Literature (al-Adab al-Arabiyy).
Wa
tano kutoka kulia ni Sayyid Ali Badawi Jamalullayl- huyu Bwana alikuwa alim
mkubwa sana. Alisomesha Jiographia ya Nyota, Sayari na Ardhi. Vile vile
alisomesha Elimu ya Maani na Balaghah
|
No comments:
Post a Comment