Maalim Seif akizungumza na Mwandishi (haonekani kwenye picha) nyumbani kwake Dar es Salaam |
Mwandishi akimkabidhi Maalim Seif kitabu cha Kumbukumbu za Ali Muhsin Barwani ''Conflict and Harmony in Zanzibar.'' |
Kumtembelea Maalim Seif
nyumbani kwake ni mfano Waingereza wangesema ‘’a walk in the park,’’
Kiswahili chake labda mtu ungesema unatoka chumbani kw.ako unakuja sebuleni
yaani ni wepesi usiomithilika. Maalim nimefahamiananae kwa mara ya kwanza 1992
nilionananae Starlight Hotel Titi Street, Dar es Salaam. Hizi zilikuwa siku za mwanzo za
siasa za vyama vingi. Miaka mingi imepita na hapa katikati tukionana kwa mbali
sana na kwa muda mfupi mfupi ile ya kupeana salaam, Waswahili wanausemi, ‘’salaam
ya Mungu,’’ ikiwa na maana mnasalimiana kisha mnapitana kila mtu na hamsini
zake. Lakini namini Maalim akinisoma na wakati mwingine akinisikia katika
vyombo vya habari, pia wakati mwingine akipata salaam zangu kupitia jamaa na marafiki. Lakini
mimi Maalim nimenfuatilia kwa karibu na nimempiga picha nyingi sana kwa
kiasi ya miaka ishirini na zaidi.
Leo nimepata bahati ya kumfikia nyumbani
kwake Sharif Shamba nje na mbali na matarumbeta na shamrashamra za mikutano na mengineyo.
Ilikuwa starehe tukinywa kahawa na kucheka mfano tuko barzani tunapumzika. Lakini tabu kukutana na mtu kama Maalim Seif ukaacha kumdodosa lau kwa mbali kwa namna ya maskhara. Najua kitabu cha Ali Muhsin kakisoma kilipochapwa tu mwaka wa 1997 lakini niliona nimepelekee kuchokoza upya fikra zake. Mimi binafsi katik kitabu cha Ali Muhsin moja ya sehemu iliyokamata fikra zangu ni pale anapohadithia yale aliyokutananayo katika jela mbalimbali za Tanganyika wakati alipofungwa baada ya mapinduzi. Nikamrushia Maalim swali, ''Maalim tupate basi kitabu makhsusi ulipokuwa kifungoni.'' Kacheka kidogo. Nilikuwa nimemkumbusha mbali. Jibu lake lilikuwa, ''In Shaallah.'' Sikumuacha karibu nikaongeza na ''Memoirs...'' yaani kumbukumbu za maisha yake. Mara ya mwisho kuwa jirani sana na Maalim ilikuwa mwaka wa 2012 Bwawani Hotel nikiwa na TV Imaan tulikokwenda kumsikiliza Maalim akizungumza kuhusu hali ya Zanzibar na mategemeo ya wananchi.
Maalim alikuwa sasa yuko serikalini. Nakumbuka shida niliyowapa walinzi pale nilipoingia katika chuma cha faragha alipokuwa Maalim Seif, Mzee Hassan Nasoro Moyo na viongozi wengine. Mimi nilikuwa nje na wala sikuwa na nia ya kuingia ndani ya chumba kile kwani mtangazaji na mtu wa kamera tayari walikuwa ndani ya chuma kile wakishughulika. hawa vijana wote wana vitambulisho shingoni vinaning'inia na watu wa usalama weshawaruhusu. Mimi sina chochote lakini Ismail Jussa ndiye kanishika mkono tunazunguma basi hadi mle chumbani nikawa sasa uso kwa uso na Maalim. Ikawa sasa tunazungumza hili na lile, ''easy.'' Sasa nimefungua ''tablet,'' yangu nampiga picha Maalim na wakati mwingine kumwelekeza ''pose,'' niitakayo. Kumbe jamaa wa Usalama kidogo weshafanya wasiwasi wa kutaka kunijua mie nani. Mara niko kwa Mzee Moyo tunazunguza na kucheka. Lakini jamaa wa Usalama bado hawajanijua mie nani. Mara nimerukia Eddy Riyami basi ikawa kwao wao ni tafrani kidogo. Nilipotoka nje tu wakanifikia kwa maswali...
Jicho halisahau kile ambacho jicho la kamera liliona. Naomba kamera yangu ikuchukue katika barabara ya kumbukumbu turudi nyuma zaidi ya miaka ishirini iliyopita pale nilipoanza kufuatilia nyayo za Maalim na wale aliokuwa pamoja na yeye...

Fatilia ukurasa huu...In Shaallah tunautengeneza....
Mwandishi akiwa Viwanja Vya Jangwani akifuatilia mkutano wa CUF na kupiga picha mwaka wa 2000 |
Kalenda ya Maalim Seif kuingia Ikulu Zanzibar 1995 ilikuwa imewekwa kwenye maskani maarufu CUF ''Jaws,'' Stone Town |
Mwaka wa 2012 baada ya miaka 17 kupita na hali ya siasa za Zanzibar kubadilika, Maalim na CUF wakipata nguvu kila kukicha nilifanya mahojiano ya televisheni na Baraka Shamte, kada mkubwa wa CCM na mwana ASP. Wakati huu Maalim alikuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar. Nimepata kumjadili Baraka Shamte mara kadhaa katika mitandao ya kijamii. baraka Shamte ni mtu mwenye histroia kubwa katika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964. Baraka Shamte ametunukiwa nishani ya miaka 50 ya mapinduzi.
Mwandishi Akifanya Mahojiano na Baraka Shamte Kada Maarufu wa CCM Nyumbani
Kwake Mkunazini Zanzibar Kuhusu Historia ya Mapinduzi. Baraka Shamte ni Mtoto wa Mohamed Shamte Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Zanzibar Aliyepinduliwa Katika Mapinduzi ya 1964 |
Uchaguzi wa Mkuu Zanzibar 1995 Mwandishi akiwa nje ya kituo cha kupiga kura Darajani siku ili mvua kubwa ilipiga |
Shaaban Mloo na Kabourou kampeni za uchaguzi wa 2000 |
Kushoto: Prof. Ibrahim Lipumba, Shekue, Mama Ummie na Ummie biti yake.
Nilipokutana na Maalim kwa mara ya kwanza aliniuliza uwezekano wa CUF kupata wanachama Bara. Fikira ya Maalim ilikuwa ni kuwapata wazee wetu wa Dar es Salaam kuunga mkono chama. Mimi nikamwambia kuwa wazee wetu tuwaache kwa sasa tulenge vijana. Nakumbuka nilirudi tena kwa Maalim na baadhi ya vijana wachache viongozi na tukabadilishana mawazo.
Vijana hawa walikuwa wametokea chama cha National Reconstruction Alliance ambako mwenyekiti alikuwa Prof. Malima na alipokufa ikawa vijana wamepwelewa. Sasa Alipopatikana Prof. Lipumba moto ukawaka upya na matumaini mapya yakaibuka. Mwandishi ndiye ailiyemtambulisha Prof. Lipumba katika mkutano mkuu wa CUF. Tulikuwa tunaingia katika uchaguzi mkuu wa 1995. Mwandishi ndiye ailiyemtambulisha Prof. Lipumba katika mkutano mkuu wa CUF. Tulikuwa tunaingia katika uchaguzi mkuu wa 1995. Kwa kuwa mwandishi hakuwa mjumbe katika mkutano ule alisubiri nje ya ukumbi pale Star Light hadi usiku wa manane ndipo alipoingizwa mkutanoni kwa kazi hiyo tu kisha akatoka nje kupisha mkutano uendelee. Siku zile kwa shida ya fedha CUF wakifanya mikutano yao usiku na asubuhi wajumbe wanapanda mabasi kurejea makwao. Naamini Maalim hakujuta kwa kuletewa vijana badala ya wazee wetu kwani kila alipopita mikoani na vijijini alipokelewa na vijana hawa. Baadae zilitufikia taarifa kuwa wapinzani wetu walishangazwa ni lini tulijenga mtandao ule wa nchi nzima na bila shaka swali hili pia lilikuwa kichwani kwa Maalim. Iko siku In Shaallah tutaelezana ni vipi hawa vijana walipatikana na tulikuwa na hadi anuani zao pamoja na nyumba na mtaa...ni hadithi ya kusisimua sana...
Vijana wanachama wa NEMA mstari wa mwisho wapili kutoka kushoto waliosimama
ni Shaaban Mzuzuri, mwandishi, Salehe Yongo (marehemu) na Adam Juma.
Tulikuwa sisi ndiyo waasisi wa ''mtandao.''
Mtandao wa Kikwete, Lowassa, Rostam wa 2005 uliomtia madarakani Jakawa Kikwete ulikuja miaka kumi baada yetu ila tofauti ilikuwa moja tu. Sisi ni watu masikini ya Mungu hatukuwa na fedha kilichokuwa kikitusukuma ni mapenzi ya nchi yetu na ari ya kupigania usawa na haki kwa kila mwananchi bila ya ubaguzi.
|
Mwandishi akiwa IDM Mzumbe akikitangaza kitabu cha Abdul Sykes 1999
Uchaguzi. wa mwaka wa 1995 ulitufunza mengi na kilipotoka kitabu changu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924- 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' kitabu kilifungua mlango mwingine wa kuwafikia vijana wa Kiislam wasomi. Kitabu kilifungua historia mpya haijapatapo kuandikwa popote na kubwa zaidi ya yote mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika..Vijana walipatwa na butwaa kusoma kuwa TANU haikuasisiwa kama walivyokuwa wakifundishwa katika historia na Nyerere bali na marehemu Abdulwahid Sykes. Historia waliokuwa vijana wakisomeshwa toka shule ya msingi hadi chuo kikuu ikaporomoka kwa kasi ya ajabu. Harakati hizi mpya za chama kingine nje ya CCM ikapata wafuasi wapya.
Sasa likazuka tabaka lau kama ni dogo la wasomi vijana wa Kiislam ambao kwa yale waliyoyasoma katika kitabu kile wakahisi wao na wazee wao ni jamii iliyodhulumiwa kwani haiwezekani Waislam wapiganie uhuru kwa kiasi kile kisha mwishowe uhuru wenyewe usiwanufaishe kitu. Hapa ndipo nilipogundua kosa nililafanya la kuandika kitabu kwa Kiingereza badala ya Kiswahili na hivyo kukosa wasomaji wengi.
Kwa upande wa vijana wa Kizanzibari nao walishangazwa kusikia kuwa Sheikh Hassan bin Amir Mzanzibari alipigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Julius Nyerere na akina Abdul Sykes. Mwandishi akaalikwa Chuo Kikuu Cha Zanzibar akatoe mada kuhusu Sheikh Hassan bin Amir. CUF haikuwa na tabu kwa vijana wasomi Zanzibar. Lile lilikuwa jimbo lao salama. Shida ilikuwa katika vyuo vikuu Bara. Katika uchaguzi wa 1995 tulimsindikiza Prof. Lipumba aliyekuwa mgombea urais wa Bara kwa tiketi ya CUF. Hivi vyuo vikuu Bara ni ngome ya Ukristo kwani Waislam hawajaweza kufikia hata asilimia kumi. Wanafunzi waliokuja kumsikiliza Prof. Lipumba walikuja zaidi katika kumkejeli kuliko kumsikiliza kama mgombea urais na mchumi bingwa. Lakini uchaguzi wa mwaka wa 2000 umma uliojitokeza katika mikutano ya Prof. Lipumba ulitisha CCM. Hasa mapokezi ambayo hayajapata kuonekana siku alipotoka Mwanza kuja Dar es Salaam wakati wa uchaguzi.
Sheikh Hassan bim Amir akipeana mkono na Julius Nyerere katika sherehe ya kuweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu Cha Waislam 1968 |
Kwa upande wa vijana wa Kizanzibari nao walishangazwa kusikia kuwa Sheikh Hassan bin Amir Mzanzibari alipigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Julius Nyerere na akina Abdul Sykes. Mwandishi akaalikwa Chuo Kikuu Cha Zanzibar akatoe mada kuhusu Sheikh Hassan bin Amir. CUF haikuwa na tabu kwa vijana wasomi Zanzibar. Lile lilikuwa jimbo lao salama. Shida ilikuwa katika vyuo vikuu Bara. Katika uchaguzi wa 1995 tulimsindikiza Prof. Lipumba aliyekuwa mgombea urais wa Bara kwa tiketi ya CUF. Hivi vyuo vikuu Bara ni ngome ya Ukristo kwani Waislam hawajaweza kufikia hata asilimia kumi. Wanafunzi waliokuja kumsikiliza Prof. Lipumba walikuja zaidi katika kumkejeli kuliko kumsikiliza kama mgombea urais na mchumi bingwa. Lakini uchaguzi wa mwaka wa 2000 umma uliojitokeza katika mikutano ya Prof. Lipumba ulitisha CCM. Hasa mapokezi ambayo hayajapata kuonekana siku alipotoka Mwanza kuja Dar es Salaam wakati wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment