Mzee Chihota alikuwa Meneja wa Arnatouglo Hall nadhani alipotoka yeye
ndiye akaja Denis Phombeah, Mnyasa.
Mzee Chihota alikwenda masomoni Uingereza na huko mauti yakamfika na
alizikwa huko huko.
Hii ilikuwa miaka ya mwanzoni 1950s.
Kuna Mtaa Temeke umepewa jina, ''Chihota,'' kwa heshima yake.
yake.
Hawa walitoka Rhodesia.
Gershom Chihota nilisomanae St. Joseph's School na tukicheza mpira sote
na kupiga muziki yeye akipiga bass guitar.
Baada ya uhuru kupatikana walirudi kwao na huko Raymond alifariki.
Huyu alisoma Urusi na alioa Mrusi.
Raymond alipomaliza shule Aga Khan alifanyakazi TBC kama mtangazaji na
allikuwa na kipindi, ''Teenagers Time,'' akipiga pop music akina Cliff Richard,
Helen Shapiro, Elvis Presly, Beatles, Rolling Stones etc.
Ray kama alivyokuwa akijulikana alikuwa mmoja wa ''Chipukizi,'' na akina Henin
Seif, Abdul Nanji, Badrin, Salum Hirizi (Sammy Davis), Yusuf Ramia, Hussein Shebe, Cuthbert Sabuni,
Sauda Mohamed, Maryam Zialor na vijana wengi wa Dar es Salaam.
Salum Hirizi (Sammy Davis) 2016 |
Kushoto ni Abdul Nanji kama alivyo hivi sasa n na John Mtembezi |
msaada wa David Wakati wakaanzisha kipindi RTD, ''Chipukizi Club.''
Kipindi hiki kilipendwa sana na vijana hadi pale kilipokuja kupigwa marufuku na
Regiional Commissioner wa Dar es Salaam, Mustafa Songambele kwa sabau ati
kinatukuza utamaduni wa kigeni.
Mustafa Songambele 2015 |
walizokuwa wakipiga.
Chipukizi walikuwa wakipiga pamoja na vijana wa Kigoa wakijiita, ''The Blue Diamonds.''
Walikuwa na wapiga magitaa hodari sana.
Hii ilikuwa 1963/64.
Ray na Yusuf Baruti wakaenda kusoma Urusi na ''members,'' wengi wa Chipukizi wakaondoka kwenda
nje.
Hussein Shebe akaenda Nairobi kujiunga na Ashantis kama muimbaji na kwa kweli
aliipaisha ile bendi na hawakukaa sana Nairobi wakenda Addis Ababa wakawa
wanapiga Wabe Shebelle Hotel, hotel kubwa sana wakati ule.
Sal Davis ndiye aliyemchukua Hussein kumpeleka Nairobi.
Sal alikuja Dar es Salaam na alifanya show moja na Chipukizi Radio Tanzania na hapo
ndipo alipomsikia Hussein akiimba.
Sal Davis na Meneja wa Philips Uwanja wa Ndege Nairobi aliporudi na nyimbo ya kumsifia Jomo Kenyatta wakati wa uhuru 1963 |
Badrin na Nanji wao walikwenda America.
Salum Hiirizi anasema nyimbo ambayo Badrin akipenda kuimba ilikuwa, ''Fame
and Fortune,'' ya Elvis Presley.
Sabuni na bendi yake, ''The Flaming Stars,'' akiwa na Peter Kondowe (Peco) na
George Mzinga wao wakaenda Mombasa.
Miaka mingi baadae nilifika Addis Ababa na nilikaa Wabe Shebelle lakini hoteli ilikuwa
taaban, imechoka.
Nakumbuka nililetewa Coke lakini sikuweza kuitambua chupa jinsi ilivyokuwa imesagika.
Hii ilikuwa 1989 enzi ya Mengitsu Haile Mariam na Hussein Shebe na Ashanti
wamekimbia wanapiga muziki wao Italy.
Nakumbuka Ray aliporudi alikaribishwa Radio Tanzania English Service kwa mahojiano
katika kipindi cha muziki.
katika nyimbo alizochagua apigiwe moja naikumbuka kwa kuwa nami nikiipenda,
''Let The Good Times Roll,'' ya Ray Charles.
Mwaka wa 1993 nilikwenda Harare na nilimtafuta Gershom na Norman na bahati
nzuri nilikutananao.
Nina picha nikizipata nitaziweka hapa In Shaallah.
Baada ya miaka mingi sana nilikutana na Hussein Shebe kwenye boat tunakuja Dar es
Salaam kutoka Zanzibar nilikuwa na rafiki yangu Tamim Faraj.
Tulikumbushana mengi na akanipa cassette yake na Ashanti.
Hivi sasa Hussein amepumzika muziki na akiwa na nafasi hupita nyumbani kwangu
kunijulia hali kila anapokuja kutoka Zurich anakoishi na mkewe Mswiss na wanae na kila
siku ananikaribisha Switzerland.
Ingia You Tube ustaladhi na muziki wa Hussein Shebe.
Katika mahojiano nliyofanya na Hussein ananambia kuwa siku alipomwambia Meneja wake
kuwa yeye muziki basi alishtuka na akambembeleza sana.
Hussein hajatazama nyuma.
Mke wake anasema, ''Huyu Hussein toka amerudi kwenye Uislam wake...''
Siku moja nafanya mahojiano na Hussein.
Ghafla ananyanyuka ananambia, ''Mohamed Maghrib sasa tuswali kwanza...''
Machozi yalinilengalenga...
Tulikuwa nyumbani kwa rafiki yake toka udogo wao - Henin Seif.
Kakutana na mke wangu msikitini anamwambia, ''Mohamed si rafiki yangu ni ndugu yangu...''
No comments:
Post a Comment