Sijaileta stori hii kama kejeli.
Historia ya TANU na nyakati zile ina mengi ambayo nilikutananayo
katika utafiti.
Hebu sikiliza kisa hiki.
Baada ya uhuru pakatokea waandishi wakawa wanamkejeli marehemu
Abdul Sykes kuhusu TAA wakikiita chama cha ''starehe,'' na majina
mengi ya dharau na kejeli.
Hawakuishia hapo wakawa hata kuwa Abdul kaunda TANU wakaifuta na
kumvisha Nyerere taji lile.
Haikupita muda ikawa Abdul Sykes hatajwi kabisa katika kundi la wazalendo
walioasisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ajabu ni kuwa hili hata siku ile alipofariki magazeti hayakuandika chochote
kuhusu mchango wake katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Kilichondikwa ilikuwa kutoa taarifa kuwa Nyerere kahudhuria maziko ya
Abdul Sykes.
Hiki ndicho kipindi Shariff Attas alipokutana na Nyerere pale TANU Office.
Kwa bahati mbaya sana ikawa Nyerere hakumkumbuka Shariff.
Bahati mbaya zaidi Shariff Attas yeye akaamua iwe hawakupatapo kujuana.
Sikuleta kejeli kwani hakuna tija katika hilo.
Nia yangu ilikuwa kuonyesha TANU ilikuwa imetoka wapi na vipi kwa kuacha
kuandika historia ile nchi imepoteza hadhi za mashujaa wake.
Palitokea watu waliokuwa wanakerwa na kejeli zile mmojawapo akiwa Ahmed
Rashad na walimfuata Abdul kumtaka aeleze historia ya TANU lakini yeye
alikataa kusema lolote.
Laiti nisingeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes wengi hapa JF mngebaki
kizani kuhusu historia ya TANU.
Abdul Sykes na Julius Nyerere marafiki wakubwa wakati wa kuunda TANU
leo wote ni marehemu.
Tunataja majina yao katika historia ya Tanganyika kwa ajili ya kuhifadhi heshima
na kumbukumbu zao.
Mimi nasikitika mkasa wa Shariff Attas umekuchoma kiasi umefika kutukana.
Hii ni bahati mbaya.
Miaka 30 iliyopita wakati naanza utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes siikufikiria
hata kwa mbali kuwa kitabu hiki kitaleta msisimko katika historia ya Tanganyika.
Kushoto: Hussein Shebe, Abdallah Awadh, Abbas Sykes, Kleist Sykes Aliyechutama Bwana Shomari Msikiti wa Kipata 2014. |
No comments:
Post a Comment