Wednesday, 21 September 2016

KUTOKA JF: BAADA YA UHURU KUPATIKANA 1961 KULIKUWAPO NA NJAMA?




Barafu,
Nimesoma kila kitabu, kila jalada katika majalada ya Nyaraka za Sykes
kutafuta labda kuna mahali ambapo palikuwa na mkuruzano sikuweza
kupata kitu.

Nimefanya mazungumzo mengi na Ally Sykes, Ahmed Rashad Ally,
Hamza Aziz, Zuberi Mtemvu,
na Ally Mwinyi Tambwe.

Sijapata kitu kuwa kulikuwa na uadui wowote baina ya wazalendo hawa.

Nimezungumza na wazee wengi wa Dar es Salaam kuhusu siasa baada
ya uhuru.

Sikupata kitu ila tatizo la kuvunjwa kwa Baraza la Wazee wa TANU 1963
na kukamatwa na kuwekwa kuzuizini masheikh kuanzia 1964 baada ya
maasi ya jeshi na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society na
Nyerere kuunda BAKWATA na kukamatwa kwa Mufti Sheikh Hassan
bin Amir
.

Haya ndiyo mambo yaliyotia dosari mapenzi ya Waislam kwa Nyerere.

Lakini haya niliyoeleza hapo juu mimi binafsi niliyajumuisha kuwa ni uoga
wa Nyerere kuwa Waislam katika Tanganyika kutaka kujenga Chuo Kikuu
na kwa hakika jiwe la msingi aliliweka yeye.

Hili la Waislam kupata elimu ya juu ilijaza hofu Kanisa.

Picha ilianza kujitokeza kwa kitabu cha Bergen mwaka wa 1981, ''Religion
and Development in Tanzania.''

Sasa mwaka wa 1992 Sivalon alipokuja kuandika kitabu, ''Kanisa Katoliki
na Siasa ya Tanzania Bara 1952 - 1985,'' (Ndanda 1992) kitendawili hiki
kikateguka.

Sijakuta popote kuwa palikuwa na njama za Waislam kumwendea Nyerere
kinyume.

[​IMG]

Hivi karibuni waandishi wa kitabu cha maisha ya Mwalimu Nyerere walinitafuta
niwapatie kitabu cha Bergen.

Inaelekea na wao wanataka kujua ukweli wa yale aliyoandika Bergen kuhusu
Nyerere kuwa aliahidi kulipa nguvu kanisa lake katika nchi ya kisekula na yeye
akiwa kiongozi mkuu.

Historia hii inataka utulivu wa akili.
Haitaki hamaki wala kuifunga akili ukawa unapenda kusikia kinachokufurahisha.

Barafu,
Nyerere hakutaka ''kufanywa,'' lolote na wazee wetu.
Wala hakuna jipya la kufunguliwa.

Abdul Mtemvu akiandika gazeti la ''Change,'' katika miaka ya 1990
alimfanyia mahojiano Dossa Aziz nyumbani kwake Mlandizi.

Alimuuliza Dossa, ''Baada ya haya yote kutokea baina yenu ikiwa leo
mtarudi Arnautoglo kufanya uchaguzi kati ya Abdul Sykes na Julius
Nyerere
, utamchagua nani?''

Jibu nakuachieni nyie mkisie nini alisema Dossa Aziz.

No comments: