Saturday, 10 September 2016

KUTOKA JF: ''UJANJA,'' WA NYERERE


Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Sulieman Takadir, Julius Nyerere
Nyuma kulia John Rupia, Rajab Diwani na Mama Maria Nyerere wakati wa kupigania
uhuru wa Tanganyika
Mwandishi akifanya mahojiano ya televisheni na Abbas Sykes 2012




Barafu,
Kwanza ningependa kukufahamisha kuwa Dossa hakuwa anamuendesha
Nyerere.

Kumwendesha mtu ni kuwa dereva kaajiriwa.

Dossa hakuwa dereva wa Nyerere bali Dossa alikuwa na gari ya kutembelea
na gari hiyo ndiyo aliyokuwa akipanda Nyerere.

Kuhusu uhusiano wa Chief Kidaha Makwaia na Abdul Sykes huu uhusiano
ulikuwapo hata Abdul hajamjua Nyerere.

Uhusiano huu ulikuwa wakati Chief Kidaha ni mjumbe wa Legico na Abdul ni
Rais wa TAA.

Hiki ndicho kipindi alichomtaka Chief Kidaha ajiunge na harakati za kuunda TANU.
Si kama habari hizi zilikuja kusemwa baadae na watu kuelezwa baada ya ''ujanja,''
wa Nyerere.

Historia hii haikupatapo kujulikana hadi mimi nilipoiandika baada ya kuelezwa na mke wa Abdul Sykes, Mama Daisy.

Kuhusu ''ujanja,'' msome Abdul Sykes utafahamu uwezo wake si wa kufadhili chama tu bali hata ''intellect,'' yake.

Angalia ni watu gani Abdul alikuwa anasubihiananao wakati ule kuanzia akina 
 Chief Kidaha, Chief Marealle, Chief Fundikira, Earle Seaton nk.

Huyu ni kijana aliyepata ''admission,'' ya Makerere 1942 na Princeton University 1953.

Huyu ni kijana ambae aliweza kuunda TANU ndani ya ubongo wake kuanzia 1945 akiwa vitani Burma na kukamilisha ndoto yake 1954.

Huyu ni kijana aliyekuwa ana uwezo wa kuandika shajara (diary) zake aidha kwa ''long hand,'' au kwa ''hati mkato,'' (short hand).

Huyu ni kijana aliyeweza kuwaunganisha vijana wenzake dhidi ya ukoloni katika chama alichoasisi baba yake 1929.

Abdul ndiye aliyempokea Nyerere Dar es Salaam na kumtia katika, ''circle.''

Kuhusu hayo unayosema katenda Nyerere ''ujanja,'' dhidi ya historia hii mimi sina haja ya kuyarejea hapa.

Kuna wakati Abdul Sykes hakuwa ananasibishwa na TANU wala na historia ya
uhuru wa Tanganyika wala na Nyerere.

Hili jambo sasa haliwezekani tena.
Kwangu mimi kazi ya kuandika historia ya wazee wangu imekamilika.

Mwaka wa 2011 Abdul na Ally Sykes katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru
wa Tanganyika, ndugu hawa wawili walitunukiwa medali kutambua mchango
wao katika uhuru wa Tanganyika.

Kama yupo mtafiti anataka kuandika, ''ujanja,'' wa Nyerere na afanye hivyo na hakika atakuwa kaongeza elimu katika kuijua historia ya Tanganyika.

No comments: