Saturday, 10 September 2016

KUTOKA JF: VITABU MUHIMU KUMUELEWA NYERERE NA HISTORIA YA TANGANYIKA


Barafu,
Kuna vitabu ni muhimu sana mwanafunzi wa historia ya Tanganyika kuvisoma.
Kitabu cha kwanza ni cha Bergen (1981).

Kitabu cha pili ni cha Sivalon (1992)
Kitabu cha tatu cha Njozi (2002) lakini hiki kilipigwa marufuku na serikali.

Pia kuna tasnifu ya Kiwanuka (1973)
Mswada wa kitabu cha Tewa (unadated)

Hapa unazungumzia kusoma takriban kurasa 500 za kazi ya kitafiti.

Nimeepuka kwa sababu za wazi kabisa na kwa makusudi kabisa kuweka rejea
ambazo mimi ndiye mwandishi.

Katika rejea hizi utajifunza mengi.

Kitabu cha Bergen kilikuwa kikiiuzwa Cathedral Bookshop lakini baada ya
kugundua yale yaliyoandikwa kimya kimya kimeondolewa hali kadhalika na
kitabu cha Sivalon.

Kuna jopo la wasomi wa Kitanzani likiongozwa na Prof. Shivji hivi sasa wako
katika kutafiti na kuandika kitabu cha maisha ya Nyerere.

Nimefanyanao mahojiano mara tatu nyumbani kwangu.

Katika nyaraka walizoniomba niwapatie ni mswada wa Tewa na kitabu cha
Bergen.

Mwandishi akifanya mahojiano na Prof. Shivji na Prof. Saida Othman
 

No comments: