Friday 9 September 2016

KUTOKA JF: MAAJABU YA HISTORIA: BI. MISKI SIMLELEO SHANGAZI YA CHIEF ADAM SAPI MKWAWA BIBI YAKE ABDUL SYKES
















Barbarosa,
Wapi mimi nimesema kuwa naona sifa?
Hata hivyo mtu huwezi kukataa asili yako kwa ajili ya historia.

Historia ina mambo ya kushangaza sana.
Soma historia ya uhuru wa Tanganyika.

Sykes Mbuwane aliingia Tanganyika kama mamluki wa Wajerumani
kuja kupigana na Chifu Mkwawa, Kalenga na Abushiri bin Salim, 
Pangani.

Mtoto wa Sykes MbuwaneKleist Sykes akajakuwa mzalendo na
Mtanganyika aliyewasha moto wa kupambana na ukoloni 1929.

Watoto wa Kleist SykesAbdulwahid, Ally na Abbas wakaja kuasisi
TANU 1954.

Lakini ukiangalia nyuma asili ya hawa wote chanzo chao ni askari mamluki
aliyeingia Tanganyika mwisho wa 1800 wakiongozwa na Herman von
Wissman 
amebeba bunduki kuja kupigana na wananchi wa Tanganyika ili
nchi hii itawaliwe na Wajerumani.

Angalia sasa ajabu ya historia.

Sykes Mbuwane alikuwa askari mamluki wa Wajerumani akapigana na
Chifu Mkwawa na Abushiri bin Salim wazalendo wa Tanganyika.


Kushoto: Kleist Sykes, na kitinda mimba Abbas
Waliosimama kushoto ni Ally na Abdulwahid akiwa katika uniform ya KAR
Picha ilipigwa 1942 Abdulwahid alipokujaaga kutoka Kenya kabla ya kwenda Burma


Kleist Sykes akapigana WW1 upande wa Wajerumani dhidi ya Waingereza
(1914-1918).

Watoto wake Abdul na Ally wakapigana WWII na Waingereza dhidi ya
Wajerumani (1938-1945).


Abdulwaid na Ally Sykes wakiwa 6th Battalion Burma Infantry
King's African Rifles (KAR) Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945)

Hapo chini ni kaburi la Bi Miski Simleleo:



Bi. Miski ni shangazi yake Chief Adam Sapi Mkwawa.

Maana yake ni kuwa Bi. Miski ni mjukuu wa Chief Mkwawa.

Huyu Bi. Miski ndiyo mama yake Bi. Mruguru biti Mussa Ngomangando,
kabila Mndengereko, ambae ndiye mama yao Abdul, Ally na Abbas.

Hilo hapo chini ni kaburi la Bi. Mruguru biti Mussa:



Kwa lugha nyepesi ni kuwa akina Mkwawa na Sykes ni ndugu wa damu
ingawa hapo mwanzo Wazulu mamluki walipokuja Tanganyika walikuwa
maadui wa Wahehe.

Kaburi la Kleist Sykes hilo hapo chini:



Hii ndiyo sababu fuvu la Mkwawa liliporejeshwa Tanganyika mwaka wa 1955,
Chief Adam Sapi Mkwawa alimualika Abdul Sykes na Dossa Aziz katika
sherehe ile iliyofanyika Kalenga.


''Mwaka 1954 fuvu la Mkwawa liliporudishwa Kalenga Adam Sapi Mkwawa mjukuu wa Mtwa Mkwawa aliwaalika Abdulwahid Sykes mjukuu wa Sykes Mbuwane, adui wa babu yake na Dossa Aziz kuja katika sherehe ya kupokea fuvu lile. Ilikuwa pale Kalenga ndipo Abdulwahid alipomuingiza Adam Sapi katika TANU kwa siri na kumfanya awe mmoja wa machifu wa mwanzo kabisa kuiunga mkono TANU. Wakati Chifu Adam Sapi anajiunga na TANU chama kilikuwa hakijamaliza hata mwezi moja katika uhai wake. Tutazieleza habari za Abdulwahid Sykes na ushawishi mkubwa aliokuwa nao katika TAA na baadae TANUna katika wanasiasa wa wakati ule pamoja na machifu tutakapofika kusanifu makazi yake pale Stanley Street kona na Sikukuu Street. (Baada ya uhuru mtaa huu ulikuja ulibadilishwa jina na kuitwa Aggrey) Ila ieleweke tu kuwa kwa wakati ule wa siku za mwanzo za harakati kuanzia enzi za TAA baadhi ya machifu hawakuitazama TAA na baadae TANU kwa jicho zuri sana. Hofu kuu na ndiyo hofu aliyokuwanayo mshirika wao Muingereza katika ule mfumo “indirect rule” wa Lord Lugard ni kuwa TANU imekuja kuwanyang’anya madaraka yao.''

Wanamajlis,
Mnasemaji kuhusu maajabu haya ya historia ya Tanganyika?
Wapi wanahistoria waonyeshe kidole cha lawama?



No comments: