Earle Seaton na Julius Nyerere |
Wapi utazisikia ndugu yangu habari za Abdul Sykes ikiwa wanahistoria walimsusa?
Kwani kabla ya mimi kuandika kitabu cha Abdul wewe ulimjua?
Kumrejesha kwangu katika historia ndiko kulikoninyanyua mimi na kitabu changu
kwani nilikuja na mambo yaliyowastaajabisha wasomi wengi duniani katika tasnia
ya African History.
Walisoma katika kitabu hicho mambo ambayo yalikuwa mapya kwao.
Hii ndiyo iliyonifanya niingizwe katika Cambridge Journal of African History na kuwa
mmoja wa waandishi katika mradi wa Dictionary of African Biography (DAB).
Huu ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.
Katika kitabu cha Abdul Sykes kuna mahali nimemlaumu John Iliffe kwa yeye
kutumia Nyaraka za Sykes kuandika historia ya African Association akimtumia
mwanafunzi wake Daisy Sykes binti ya Abdul, lakini alishindwa kuchukua juhudi
yoyote kumtafuta Abdul Sykes kumhoji kuhusu TANU.
Hii ya Makerere ni ndogo wala isitushughulishe inafahamika na ''contemporaries,''
wake wote si ''news,'' kwangu.
Sikiliza hii.
Siku moja Kleist Sykes, huyu ni mtoto wa Abdul Sykes kanipigia simu ananiomba
niende ofisini kwake nikaangalie kitu.
Nilipofika akanitolea barua mbili zote za mwaka wa 1953.
Moja ni ''Admission Letter,'' ya Princeton University na ya pili ni barua kutoka kwa
Earle Seaton.
Barua hizi mbili zote zina uhusiano.
Barua ya Earle Seaton anampongeza Abdul Sykes kwa kupata nafasi Princeton na
katika barua ile anamwambia kuwa akiwa New Jersey asikose kwenda UNO kusikiliza
majadiliano ya Nchi Zilizokuwa Chini ya Udhamini wa UNO.
New Jersey ni jirani sana na New York ilipo UN na ndipo kilipo Chuo Cha Princeton.
Kleist kaniahidi kunipatia nakala za barua hizo na nikizitia mkononi nitaziweka hapa
sote tuzisome.
Kwa wasiomjua Earle Seaton nitawapa kwa kifupi tu historia yake In Shaallah.
Kwanza Seaton na Abdul walikuwa marafiki na Abdul alimtia katika TAA
ili asaidie katika Constitutional Development Committee ya Gavana Edward
Twining ya 1949.
Seaton alikuwa mwanasheria akiwa na ofisi yake Moshi.
Ulipozuka Mgogoro wa Meru Abdul akamuomba Seaton aisaidie Meru Citizens Union ya
kina Japhet Kirilo kuandika petition kwenda UNO.
Kwa habari zaidi ingia:
Mohamed Said: ABDULWAHID SYKES, JAPHET KIRILO, NA EARLE SEATON, 1952
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
No comments:
Post a Comment