Friday 9 September 2016

MUDDYB KIJANA MWANAHISTORIA MBUNIFU


Photo
Muddyb
Muddy na Mwandishi

Nimekutana na kijana Muddyb katika Jamii Forums sote tukichangia mada kuhusu Azimio la Tabora. 

Muddyb akaniambia kuwa amekuwa akinitafuta muda mwingi bila mafanikio na akaomba namba yangu ya simu. 

Hivi ndiyo tulivyokutana baada ya yeye kuweka namba yake nami nikampigia. 

Muddyb bila ya kujua umri wangu kuwa mimi ni mtu mzima na siwezi kuhimili mshtuko, katika mazungumzo ya kisomi zaidi akaniambia niingie Wikipedia ya Kiswahili na niandike jina langu kwani pale yeye kafanyakazi ya kuihifadhi historia ya Tanganyika. 

Mimi huwa napita wima Wikipedia kwani si katika sehemu za matembezi yangu. 
Wakati tunazungumza lap top yangu iko mapajani na nikawa nimeingia. 

Akanambia niandike jina langu. 
Hapo ndipo nilipopata mshtuko. 

Kijana hakika kafanya kazi ya kupigiwa mfano.
Hebu na wewe staladhi hapo chini:


Wikipedia ya Kiswahili


https://sw.wikipedia.org/

Translate this page
Karibu kwenye Wikipedia ya KiswahiliWikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru. Kila mtu anaweza kuhariri makala ...
Jumuia · ‎Dini · ‎Lango:Lugha · ‎Sayansi

Mohamed Said

Mohamed Said
Ilunga - Mohamed Said.jpg
Nyuma wapili Bakari Saleh, mwisho kuliaIlunga Hassan Kapungu,
Mstari wa mbele watatu kutoka kushoto Mwanahistoria - Mwandishi Mohamed Said. Hawa walikuwa baadhi ya vijana wa Kiislamu waliohudhuria Semina Dodoma Chuo Cha Biashara 1988.
Amezaliwa25 Februari 1952 (umri 64)
GerezaniDar es Salaam
NchiTanzania
Kazi yakeMwandishi, mwanahistoria
Mohamed Said Salum (amezaliwa tar. 25 Februari1952GerezaniDar es Salaam) ni mwandishi na mwanahistoria kutoka nchiniTanzania. Ametunga vitabu mbalimbali, lakini anafahamika zaidi kwa kitabu chake cha "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes" kilichotolewa kwa lugha ya Kiingereza kwa mara ya kwanza 1998. Baadaye kikatafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa tena mnamo mwaka wa 2002.

Maisha na Kazi[hariri | hariri chanzo]

Sheikh Mohamed Said Abdallah alizaliwa mnamo tarehe 25 Februari katika mwaka wa 1952 huko Gerezani jijini Dar es Salaam - ambapo ndiko kulikokuwa na asili ya upinzani dhidi ya ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Babu yake, Mzee Salum Abdallah Popo alikuwa muasisi wa harakati za vyama vya wafanyakazi na alikuwa mmoja kati ya watu wa awali kabisa kuanzisha upinzani na kuunga mkono hoja ya kupinga utawala wa kikoloni. Mwaka wa 1947, Mzee Popo aliongoza mgomo wa kwanza nchini Tanganyikakatika majimbo ya kati nchi uliopangwa na wafanyakazi wa Tanganyika Railways. Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961, Mzee Popo aliachana na mkono wa Nyerere kama jinsi wengi walivyofanya na alitiwa kizuizini na serikali kwa ajili ya msimamo wake wa kuwa vyama vya wafanyakazi sharti viwe huru. Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya Tanganyika African National Union (TANU) chini ya Rais Julius Nyerere. Sheikh Mohamed Said ana shahada katika masuala ya Sayansi ya Siasa kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Vilevile ana Stashahada katika masuala ya Maritime Studies kutoka katika Chuo Kikuu cha Wales huko mjini [[Cardiff, Uingereza na nyingine ya BIMA kutoka katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam (IFM).

Utafiti Juu ya Historia ya Uhuru wa Tangayika[hariri | hariri chanzo]

Mohamed Said amefanya utafiti mwingi sana juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika, historia ambayo kabla ya utafiti wake ilichukuliwa kama iliyohitimishwa na ameweza kufukua mambo muhimu ambayo yalifichwa katika historia iliyokuwa ikitambulikana rasmi. Alianza kufahamika zaidi katika miaka ya themanini kupitia makala zake za kusisimua zilizokuwa zinahangaisha fikra za wasomaji kwa kufichua yale yaliyofichwam zilizoelezea mchango muhimu wa Waislamu na Uislamu katika harakati za kupinga ukoloni katika Tanganyika na khiyana waliofanyiwa Waislamu na serikali zote mbili, yaani, kabla ya uhuru na baada ya uhuru - jambo ambalo kwa wakati ule lilikuwa mwiko kufanyiwa utafiti au kuandikwa. Makala hizo zilipata kuchapishwa katika magazeti na majarida maarufu barani Afrika na katika magazeti ndani na nje ya Tanzania. Baadhi tu ya makala zake za utafiti ni pamoja na "In Praise of Ancestors" (1988), "Africa Events (London), "Abdulwahid Sykes: Founder of a Political Movement" Africa Events - London (1988), "Islam and Politics in Tanzania" (1989), Al Haq Internation (Karachi), "The Plight of Tanzania Muslim" (1993) Change (Dar es Salaam) na "The Secular Unsecular State" (1995) Change (Dar es Salaam).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

No comments: