Thursday, 22 September 2016

TOWN CLERK MZUNGU ALIVYOKERWA NA KADI ZA TANU KUUZWA OFISINI KWA MARKET MASTER ABDUL SYKES, 1954














Mindi,
Mwalimu Nyerere 
alipata kusema watafutwe wazalendo waliojiunga na TANU
kati ya 1954 - 1958 kwa maneno yake alisema kuwa kile kilikuwa kipindi kigumu.

Maneno haya aliyasema Tabora mkutanoni katika sherehe za kuadhimisha miaka
20 ya Azimio la Busara la Tabora mwaka wa 1958.

Kisa cha Mwalimu kusema maneno yale katika hotuba yake ilikuwa kutokana na
swali alililoulizwa na Ramadhani Singo.

Huyu Ramadhani Singo alikuwa mlinzi wa Nyerere Tabora wakati wa mkutano
ule wa Kura Tatu, akiwa na Mwalimu mchana na usiku akikesha nje ya nyumba
ambayo Nyerere alifikia.

Mwalimu Nyerere alipokutana na wana TANU wa Tabora kundi lile la akina Singo,
Singo alimkabili Nyerere akamwambia, ''Mwalimu mbona umetusahau wenzio?
Angalia hali zetu zilivyokuwa...''

Hii ilikuwa mwaka wa 1988.

 Kundi zima lile la TANU waasisi pale Tabora waliokuwa hai walikuwa mbele yake na
kwa hakika wote walikuwa hali zao taaban kwa kuwaangalia tu.

Singo katika ujana wake alikuwa na sifa ya kupigana na ujasiri na hii ndiyo sababu
ya yeye kupewa kazi ya ulinzi wa Mwalimu Nyerere na bila shaka ndiyo huu ujasiri
wa kumkabili Nyerere na maneno yale aliyomwambia.

Ndipo Nyerere alipopanda jukwaani kulihutubia taifa akasema maneno yale.
Turudi kwa Shariff Abdallah Attas.


Shariff Abdallah Attas alikuwa na mengi katika historia ya TANU siku zile za mwanzo.

Kuna kisa cha Mzungu, Town Clerk ambalo Kariakoo Market ilikuwa

chini yake na huyu Mzungu ndiye alikuwa ''boss,'' wa Abdul Sykes 

na Shariff Attas.

Kisa hiki ametuhadithia Shariff Attas siku ile ya Eid.
Anasema Mzungu zimemfikia taarifa kuwa Abdul anauza kadi za TANU ofisini kwake.

Mwingireza akamvamia Abdul ofisini kwake na akazikuta kadi tena Abdul kazitoa
mwenyewe katika mtoto wa meza akaziweka juu ya meza yake huku maneno yakimtoka
kuwa asimtishe TANU ni chama halali na mtu yeyote anaweza kuwa na kadi za TANU
popote.

Abdul anamjibu Muingereza Town Clerk ''boss,'' wake kwa ile ''perfect English,'' yake.
Sifa moja kubwa ya Abdul Sykes ilikuwa kuzungumza Kiingereza vizuri.

Mawazo Shomvi, huyu alikuwa mchezaji mpira wa Yanga katika miaka ya 1960 ananambia,
''Mimi iko siku nilikwenda ofisini kwa Abdul Sykes nikamkuta anazungumza Kiingereza na
mtu, nilipigwa na butwaa jinsi alivyokuwa anazunguza vizuri lugha ile.''

Muingereza na Abdul wakabwatizana hadi nje ya ofisi watu wakajazana kumtazama Abdul
anavyopimana ubavu na Mzungu.

Shariff Attas akamgeukia Kleist akamwambia, ''Baba yako alikuwa jeuri wakati mwingine.''

Wafanyabiashara wa Kariakoo Mshume KiyateShariff Mbaya Mtu na wenzao wakakutana
ghafla kufanya kisomo cha kuchinja ili Muingereza asije kusababisha Abdul afukuzwe kazi kwa
ajili ya TANU.

Kisa hiki pia alipata kunihadithia George Kissaka mtoto wa Mzee Kissaka ambae alikuwa
akifanya kazi pale sokoni chini ya Abdul Sykes.

George anasema baba yake alipata kumuhadithia kisa hiki.

Stori za TANU miaka ile ya mwanzo zinasisimua sana na kama alivyosema
Baba wa Taifa, kile kilikuwa kipindi kigumu sana.

[​IMG]
Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950

Ingia hao chini kwa historia zaidi ya Kariakoo Market wakati wa kupigani uhuru wa Tanganyika:

No comments: