Balozi Mkaaazi Seif Idd |
Bi. Fauziya Abdullah Saif Al Bahry
''Ukiwa na subra utauona mwisho wa kila jambo...''
Bi Fauziya,
Kilio tumekisikia,
Katika huko kulia,
Nasi twakusaidia...
Salim Bimani
POLE SANA MAMA FAUZIA KILIO CHAKO TUMEKISIKIA NASI
TUNAKUSAIDIA KULIA
Part-1
Asslam
Aleykum
Jina
langu naitwa Fauzia Abdullah Saif Al Bahry. Mimi ni mjane wa Said Iddi BAVUAI,
na nimeishi nae si chini ya miaka thalathini. Nimezaa nae nimejukuu nae, na
nimemkalia mpaka EDA. Na mpaka leo naendelea kuwa mjane wa mzee BAVUAI. Ambae
jana nimeshtushwa kusikia katika vyombo vya habari tunatangaziwa kwa jina la
mdogo wangu Fadya. Na sijui kwa nini wasinitangaze mimi mkubwa wakamtangaza
Fadya ambae ni mdogo na sisi tuko watatu Fauzia, Fadya na Firdaus lakini
wametumia jina la mtu mmoja kuwa sisi wabadhirifu.
Hii
lugha mimi ngeni kwangu kwa hakika siijui na hata sijui nini maana ya
ubadhirifu nauliza nini maana ya ubadhirifu ? Sijui. Lakini nimefahamishwa kuwa
ni wizi, kwaivo nakataa ile habari ilosema jana ambayo rikodi yake ipo na watu
wamerikodi. Mimi nakataa si mwizi, siibi, sitoiba na sijamuibia mtu yeyote
shamba la Kazole. Ni haki yetu tumerithi kwa wazee wetu, babaangu Abdallah bin
Saif amefariki, Nassor bin Saif amefariki, na ami yangu Hemed bin Saif
amefariki, na mali hii yetu. Mali tumerithi kwa wazee wetu.
Babaangu
na ami zangu wamerithi kwa baba yao ambae amefariki toka 1930 na makaburi yake
yapo pale pale kazole Muembe Amari, makaburi yapo ya mababu na ndugu na wazee
walio tangulia mbele ya haki. Sijui ubadhirifu huu nimeufanya kwenye kitu gani
? Kazole ni kwetu kazole nimeishi kazole nimekaa kazole naijua kwetu pakiitwa
Muembe Amari. Tena mie mtu wa Kazole jirani yangu Kitope, jirani yangu Mahonda,
jirani yangu Matetema. Shamba letu limepakana mpaka njia ya Mbaleni.
Hao
walozuka leo wakasema lile ni shamba lao au sisi tumefanya ubadhirifu. Mh kama
unataka kuchukua shamba chukua na kama unataka kuvunja kuta vunja lakini
nakataa mimi na aila (familia) yangu sio wabadhirifu.
Mimi
nimeolewa na mwanamme ambae ni kiongozi katika nchi sikumuona kufanya
ubadhirifu, wala hajanifundisha ubadhirifu, wala kwetu sikuuona
ubadhirifu. Niliona yeye (mume wangu) akifanya haki wizarani, maofisini, watu,
makazini sijasikia yeye akifanya ubadhirifu wa aina yoyote. Yeye akisuluhisha
na kutengeneza ndio hii siasa nilio ikuta wakati huo kwa hao waume
walotuoa.
Huyo
alochukua na kutoa amri ni Mh yuko katika ngazi ya juu na kajitangaza rasmi na
maredio yote yanajua, TV pia. Hajasema siri. Zanzibar iniskie na Tanzania
iniskie viongozi wa zamani wake zao wana nyanyaswa katika nchi hii. Wamesahau
kila kitu.
Part-2
Salam
kwa Balozi Mkaazi
Assalam
alaykum Muheshimiwa. Ndio, wewe ni Muheshimiwa Saif Ali Iddi, na mimi raia
Fauzia Abdullah Saif Al Bahry mjane wa Said Iddi BAVUAI. Kweli Muheshimiwa,
Muheshimiwa mwenye nguvu, Muheshimiwa hodari, Muheshimiwa jeuri.
Lakini
Muheshimiwa nakwambia hivi, nnavojua mimi nilivokuwa nimekaa na hao waasisi na
wanamapinduzi wa nchi hii walivonifundisha kuwa likitokea jambo lolote
khitilafu kwenye wilaya, mkoa, na mambo yanokhusu serekali huwa inachaguliwa
tume na watu huitwa na kisikilizwa pande zote mbili.
Ikiwa
unasema Waarabu wamekuja kuchukua na kuvamia shamba la Kazole, hakuna alokuja
kuvamia shamba la Kazole. Shamba la Kazole ni langu mimi Fauzia Abdullah Saif
Al Bahry. Umefahamu ?
Na
tulijisalimisha baada ya hao waasisi kutaka kutuoa na tukakubali ili kuondoke
hizi FITNA za ukabila. Kwahio Muheshimiwa unarejesha UKABILA ambao kaufuta
Karume 1964. Wewe unarejesha UKABILA.
Kwahio
wewe unakwenda dhidi ya siasa ya Uzanzibari. Kwahio nakwambia hiyo ni haki
yangu, nimerithi kwa wazee wangu, sijabadili uraia wangu, ni Mzanzibari, na
watoto wangu ni Wazanzibari, na wajukuu zangu ni Wazanzibari.
Muheshimiwa
chukua, na vunja kuta, na vunja makaburi, na vunja MSIKITI, na vunja kila
kilichokuwemo kwenye shamba kwa ujabari wako, na kwa uhodari wako.
Na
mimi Niko tayari kwa maneno haya uje kunichukua na kunifunga, unasikia ?
Nifunge Niko tayari lakini tulijisalimisha kwa kukataa hizi bughdha zenu.
Tulijisalimisha kwa kukataa hizi chokochoko, na bughdha na ubaguzi wenu, na
ndio tukakubali kuolewa na watu kama nyinyi.
No comments:
Post a Comment